Naendelea kusisitiza, kuna vitu vingi sana vya kujifunza kupitia filamu (movies)

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Hizi muvi unazoaziangalia ndio zimekupa picha kwamba CIA ni lidude likubwa sana. Hizi muvi ndizo zinakupa maarifa kuona kila kitu kinawezekana.

Kupitia muvi, wanaeneza uchoko, na kwa bahati mbaya watoto wako wakiziangalia, baadaye wanakuwa machoko. Kila propaganda duniani, huanzia kwenye muvi. Muvi zinaleta umoja na muungano. Sehemu zinakuwa na fujo, ila linapokuja suara la muvi, wanaungana.

Watu wanatumia mpaka bilioni 500 kutengeneza muvi, unadhani wanaweka nini humo? Kwenye maisha yangu, sidharau muvi kamwe. Mara ya kwanza nawaona wale mbuzi wanaopanda ukuta, nikasema huu ni uongo, ila nikataka kujiridhisha, kweli nikawaona. Wapo huko America Kaskazini.

Kwa sababu Wabongo tusharogwa na tuna fikira mbovu, hatutaki kupata elimu kupitia muvi. Wenzako washajua hupendi kusoma vitabu, hivyo wanakurahidishia vitu kwa kukuweka kwenye muvi. Muangalia muvi sawa na msoma vitabu. Hawapishani kwa sababu kinachowekwa kwenye kitabu, kile kile kinawekwa kwenye muvi.

Nilipojisikia uvivu kusoma kitabu cha Romeo And Juliet shuleni kwa sababu mimi na mashairi hatupatani, nikaangalia muvi yake, nikajibia mtihani na kufauli freshi. Wabongo wanadharau muvi sana, halafu Wazungu wanapenda sana muvi. Muvi zinatoa maujinga yako kichwani.

Umeangalia Escape From Sobibor, Sarafina na vinginevyo, umeingiza maarifa bila kujua. Leo ukiambiwa miaka ya tisini kulikuwa na ubaguzi mkubwa Afrika Kusini na wanafunzi wengi kuuawa, ukiangalia muvi ya Sarafina unapata majibu.

Ujinga wetu unatufanya kuangalia muvi ni upumbavu.
Husomi vitabu.
Huangalii muvi.
Unahisi ubongo wako utakua?
Utaona kila ninaloliandika ni jipya.

Ukiangalia muvi ya Gifted Hands ya Ben Carson utajifunza mengi sana. Ukiangalia The Pursuit of Happyness utajifunza mengi kuhusu utafutaji na utatiwa moyo utafute zaidi. Lakini ndio hupendi muvi. Poor Tanzanians😟
Kupitia muvi nimejifunza mengi mno. Nimeijua dunia. Nimejua hustling.

Ubongo wangu hauwezi kuwa sawa na wewe Wengine wakisikia muvi wanafikiria mapigano tu. Muvi za Wachina na Wakorea wanaweka historia za mataifa yao kupitia muvi. Sometimes natamani nikushtue upende kuangalia sana muvi ila naamua tu kukuacha uendelee kubaki hivyo ulivyo.

Tafuta muvi zile zinazohusu vita baridi, angalia uone CIA na KGB walivyokuwa wanapambania nchi zao.
Wewe umekaa tu kama sanamu, unaona muvi ni uongo. Unataka mpaka maisha ya Julius Nyerere yawekwe kwenye muvi ndio uangalie? Poor Tanzanians.

Braza na my sister penda kuangalia muvi. Siku hizi sio maarifa hufichwa kwenye vitabu tu, mengine mengi hufichwa kwenye muvi. Leo nikikuuliza kwa nini muvi ya James Bond: Goldfinger ilizuiliwa kuangalia Tanzania miaka hiyo hujui. Yaani upoupo tu bro. Penda kuangalia muvi ujifunze mambo mengi.

Siku hizi Wazungu wameishiwa ideas hivyo wanachukua hadithi za maisha ya kweli ya watu, matukio na kuyaigizia muvi. Wewe umekaa tu na kujisemea "Muvi maigizo tu na uongo" Dunia inakuacha kwa kasi kupitia maujimbe mengi ya muvi, badala ya kukaa na kusikitika na kujiuliza why umezaliwa Afrika, unakaa na kuwa proud. Yaani unaachwa unaona sifa.

Sikitika bro. Sikitika sana. Tena usikitike mno.
 
Vitu vingi vimefichwa kwenye vitabu bahati mbaya Tanzania hatusomi vitabu.
 
Acha kuipamba hiyo CIA wewe .. Filamu ya kwanza ilitoka hata hiyo CIA unayoipamba haikuwepo.
 
Mfano vitabu vipi hivo..
Inategemea mkuu kwa yanayoendelea duniani kuna NEW WORLD ORDER NA MORALS AND DOGMA halafu kuna vya self esteem kuna THE POWER OF POSITIVE THINKING NA HOW TO START LIVING AND STOP WORRYING kwenye hela kuna RICH DAD POOR DAD NA THINK AND GROW RICH ni baadhi ya vichache nilivyovisoma ila vina mafunzo mengi sana ndani yake vitabu ni tiba ambayo bara la afrika wameidharau mpaka sasa nishakuwa addicted na vitabu.
 
Napoleon wa Ufaransa sikuwahi fuatilia hostoria yake.
Baada ya kuangalia movie yake ndio kidogo nimemfahu.
 
Inategemea mkuu kwa yanayoendelea duniani kuna NEW WORLD ORDER NA MORALS AND DOGMA halafu kuna vya self esteem kuna THE POWER OF POSITIVE THINKING NA HOW TO START LIVING AND STOP WORRYING kwenye hela kuna RICH DAD POOR DAD NA THINK AND GROW RICH ni baadhi ya vichache nilivyovisoma ila vina mafunzo mengi sana ndani yake vitabu ni tiba ambayo bara la afrika wameidharau mpaka sasa nishakuwa addicted na vitabu.
Hapo mkuu nimekuelewa sana tena sana.
Asante pia kwa kunifungua kwa hili.
Maana wengi wanasemaga ishu ya vitabu ila hawatuambii ni vitabu gani..🙏🙏🙏👊👊👊
 
Back
Top Bottom