Naumia sana kubaguliwa na wazungu kila wakati

Wadada hawabagui sana, maana wanaujua mziki wetu, wadada wabaguzi wapo Italy , lakin wadada wa Urusi wapo after money hata uwe mbwa ilimradi anahisi atabenefit kitu kwako haeez kukuonesha,

Kuna watu wanatangaza nyumba za kupanga au hotel ana spesfy kwamba for Italian, au Kabayan only (wafilipino) saa nyingine mnaweza ongea na mtu Kwa simu akigundua ni Niga anakublock bila sababu
Hiyo tabia ipo hata canada Toronto kuna vitongoji kama wewe sio mhindi hupati nyumba ya kupanga
 
Ni kama vile mnavyowabagua vilema, mashoga, wanawake, chadema, ccm, waislamu, maalbino nk.

Unashangaa nini?

House girl wako tu hapo ndani unamuona kama jibwa la kuokota!

Onja na wewe hiyo ladha ya ubaguzi uone inafananaje ili wakati mwingine uwe na utu kwa watu wengine!
 
Huwa nikiwaambia watu kuwa US hakuna ubaguzi kama inavyodhaniwa, watu wanaleta ligi.

Mimi sijawahi ku experience ubaguzi wowote ule ulio wa wazi kutoka kwa Wazungu.

Na ninaweza kusema kuwa katika mataifa mengi hapa duniani, ikija kwenye mambo ya ubaguzi, Marekani imepiga hatua ndefu sana katika kuhakikisha inapambana nao kikamilifu.

Mfano mmoja tu: ni nchi gani ingine hapa duniani ambapo ethnic minorities wake wamefanikiwa sana kiasi cha kuweza kushika nafasi zote kubwa za kiutawala, zaidi ya marekani?

Mayors, governors, representatives, senators, president, Supreme Court justices, cabinet secretaries, surgeons, CEOs, billionaire businessmen and women, military generals, chairman of the joint chiefs of staff, university and college presidents, academics, etc.
I agree with you. Marekani wamejitahidi sana
 
Mbona huo ubaguzi wa kawaida tu.Ubaguzi wetu huku ni mbaya mno.Maana utasemwa na wakati mwingine kutukanwa.
Hao wanaokupisha ukae peke yako bila kukusema au hata kukutukana wewe inakuuma nini?
Sina fahari ya kuzaliwa afrika,lazima niwe wazi.Tuna tofauti ndogo sana na wanyama.Ni wabaguzi,wakatili,wachoyo,waongo,wanafiki,na hatuko halisi
 
Aiseee!

Nikishasikia haya hadi kwa nchi ambayo huwa naiona kama ya mfano kwenye civilization.Huwa naona bora nifie huku huku bara la giza, nipambane na wakina jiwe.

Sipendi kabisa kubaguliwa hata kama kwa kiasi kidogo, hasahasa kubaguliwa na ngozi nyeusi kama yangu.
Mbona wewe unawabagua na kuwadharau watu wengi tu huko kwenye maisha yako ya kila siku!

Walinzi, mamantilie, wafagiaji, wanawake, vilema, mashoga, waislamu, maalbino, wasaidizi wa nyumbani n.k..

Kale kabinti kanachokusaidia saidia hapo nyumbani unakaona kama kadude tu kasicho na thamani. Unakatukana, unakanyanyasa, unakadhalilisha....

Sijawahi kuona ukiyakemea hayo! (Mkuki kwa nguruwe?)
 
Back
Top Bottom