Naumia sana kubaguliwa na wazungu kila wakati

Kuna huu ubaguzi upo kila mahali watu hawataki kuuzungumzia tu, Matajiri kuwabagua maskini! Kwa sasa hadi kuna sehemu za starehe za matajiri tu, wanachofanya ni kuongeza bei ya vitu na viingilio/membership! Maskini anadharauliwa kila kona ya dunia hii. Hata huo ubaguzi wa rangi msingi wake mkubwa ni umaskini, hao wabaguzi wengi wanaassociate rangi na umaskini. Hao wachina wenyewe kwa wenyewe wanabaguana, wenye rangi pale wanawabagua wale wenye rangi iliyopigwa najua. Mchina mfupi, mnene and mwenye sura mbaya ni ngumu sana kupata kazi ya kueleweka kwao, wanaishia kufanya kazi mbovu mbovu zenye kipato kidogo.
 
Ni mwaka wa 10 sasa nipo nje ya Tanzania
Ubaguzi Kwa baadhi ya maeneo ni changamoto sana hasa Maeneo ya Asia
Na eastern Europe,

Hasa uturuki nilishangaa sana hata kupanda bus ukiwa mwenyewe mweusi kituoni dereva anaweza akapita,
Urusi ndo nimekaa sana kabla ya kwenda Thailand na mwishowe hapa Finland

Ubaguzi sijui wazungu tuliwakoseaga nini

Britannica
Ila tunavyowashobokea sasa
 
Ni mara nyingi sana mtu unabaguliwa lakini basi tu. Yaani unapanda treni ya mwendo kasi ukikaa kwenye siti wanahama wote. Nimejisikia vibaya sana aisee.

Ni zaid ya kunyanyapaliwa

Kama ni kweli wanakubagua basi inabidi uwakataze, na watii amri yako na kuacha kufanya hivyo. Kama huwezi kuwakataza na wakatii, basi hawawezi pia kukubagua, unawasingizia
 
Finland nao ni wabaguzi ila siyo kama Watu wa urusi,
Kuna NGO moja hapa Tanzania nilitaka kufanya nao kazi nikaambiwa Kama si mchaga hupati kazi. Hii niliambiwa live na rafiki yangu ambaye ni mchaga na alikuwa anafanya kazi hapo.
Kwahiyo ubaguzi uko kila sehemu Hadi sisi waafrika tunabaguana Sana.
 
Wakihama kqenye sit we lala kabisa au kama unakitabu jisomeee mpaka mwisho wa safari.

Halafu siku nyingine unategeneza false book cover tena kubwa ambayo imeandikwa
your first mother was
a
White Chimpanzee
volume 1.
halafu unakifunua mwanzo mwisho wa safari ili kila aliye kupisha apate ujumbe huo

Mdanganye tu mwenzio apigike..!!!
 
Ni mara nyingi sana mtu unabaguliwa lakini basi tu. Yaani unapanda treni ya mwendo kasi ukikaa kwenye siti wanahama wote. Nimejisikia vibaya sana aisee.

Ni zaid ya kunyanyapaliwa
Wakihama wote lala na ujigaragaze kwenye siti kabisa.
 
Mbona hata sisi kwa sisi tunabaguana! Mfano Ccm wanawabagua wapinzani mchana kweupe, tumechukua hatua gani? Waislamu wanawabagua wakristo, na wakristo wanawabagua waislamu,! Mifano ni mingi.

Hiyo ni hulka ya mwanadamu wa aina yoyote ile. Haijalishi rangi yake, kabila lake, dini yake, itikadi yake, nk.
Jambo la muhimu ni aidha kupuuza au kupambana dhidi ya huo ubaguzi.

Jamii yeyeto isiyofanana kubaguana ni Jambo la kawaida tu
 
Back
Top Bottom