Nauli za daladala kupanda Dar

Tunajua nishati ya mafuta imepanda kwenye soko la dunia, lakini hiyo bei waliyopendekeza is even more than too much. Ni matarajio yangu sumatra watafanya kazi yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutushirikisha sisi wadau wakuu wa wenye mabasi. Asante.
NB; Ila hayo ni madenkezo tu nikionacho mwa mjibu wa mleta thread.
 
Mkiandamana tena kupinga nauli hizi tutaua twice as much, tulia tuliii, nchi itawalike bila mizengwe.

Mnataka kuanzisha chokochoko kwenye Kisiwa cha Amani?
 
Wabongo tutia akili. na hao wanaoitetea ccm litawapa nao bila kujua. Serikali imeshindwa kazi
 
Sipati picha hapa., nini wajibu wa serikali..? Nilidhani ni kutetea maslahi ya wananchi na kuplan for their better lyf bt under these circumstances.........
 
mimi naombea maisha yawe magumu zaidi hasa kwa mikoa ya LINDI, MTWARA, PWANI, RUVUMA nk. ili watu wakule waamke kutoka usingizini, na wafahamu kuwa pesa zinazolipwa dowans ni zao.
 
No more talking. It's action time. Mi sasa actions kwa kwenda mbele. Mtanisoma tu....
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema kuwa inatarajia kutangaza viwango vipya vya nauli nchi nzima kuanzia Januari 31, mwaka huu. Hayo yalibainishwa wakati wa kikao cha pamoja baina ya Sumatra na wadau wa usafirishaji Mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki wakati wakitoa mapendekezo yao kuhusiana na viwango vipya vya nauli.
Meneja Ufundi na Usalama Barabarani wa Sumatra, Aaron Kisaka, alisema hatua hiyo inafuatia maelekezo ya sheria ya Sumatra namba 13 inayoruhusu mamlaka hiyo kutafuta maoni, habari na kufanya uchunguzi wa viwango vipya vya nauli vinavyoweza kutumika kwa maslahi ya wasafiri na wasafirishaji.
Alisema utaratibu wa Sumatra katika kubadili viwango vipya vya nauli unafanyika mara moja kwa mwaka au pale ambapo faida juu ya mtaji inakuwa chini ya asilimia tano au chini ya asilimia 25 na kwamba kufikia mwisho wa mwezi huu, mamlaka yake itakuwa imetangaza viwango vipya vya nauli, lakini akasema kuwa viwango hivi vinazingatia pia ubora wa miundo mbinu ya barabara husika.
Nao wadau wa usafirishaji wa Tanga waliohudhuria kikao hicho ambao ni Muungano wa Wasafirishaji Abiria Tanga (Muwata) na Umoja wa Wenye Mabasi Mkoa wa Tanga (Taboa), walisema kuwa ombi la kutaka kubadili viwango vya nauli ni kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji katika utoaji huduma.
Wasafirishaji hao walisema wamekuwa katika wakati mgumu kumudu mfumo wa utoaji huduma kutokana na kupanda maradufu kwa bei ya mafuta siku hadi siku, kuongezeka kwa bei ya vipuri, soko huria la vyombo vya usafirishaji sambamba na upandaji holela wa kodi mbalimbali nchini.
Tunakubaliana na maelezo yaliyotolewa na wadau wa usafirishaji kwa Sumatra kwa lengo la kuishawishi mamlaka hiyo kuridhia upandishaji wa viwango vya nauli.
Hata hivyo, jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa wakati wa mchakato wa kutafuta maoni ya wadau, ni ukweli wa hali halisi ya usafirishaji nchini.
Ni kweli kwamba gharama za usafirishaji zinapanda mara kwa mara, lakini wapo baadhi ya wasafirishaji ambao hawaelezi ukweli halisi kuhusiana na hali ilivyo katika sekta ya usafirishaji.
Baadhi yao wamekuwa wakieleza kuelemewa na gharama hasa kupanda mara kwa mara kwa bei ya mafuta, ingawa wakati mwingine wanachokizungumza hakiendani na hali halisi.
Tatizo lililoko ni kwamba wasafirishaji wengi wanataka kupata faida kubwa kuliko hali halisi ilivyo.
Wasafirishaji kadhaa wa mabasi hasa yanayotoa huduma katika miji kwa mfano katika jiji la Dar es Salaam, wamekuwa wakikaidi kutoza viwango vya nauli vilivyopangwa na Sumatra kwa madai kuwa wanaingia gharama kubwa za uendeshaji.
Hali hiyo inashangaza kwa kuwa Sumatra kabla ya kupanga viwango vya nauli, hufanya utafiti pamoja na kukusanya maoni ya wadau hivyo, viwango vya nauli inavyopanga vinaenda sambamba na hali halisi.
Kwa kuwa Sumatra imesema kuwa itaendelea kukusanya maoni ya wadau katika mikoa mbalimbali nchini, itakuwa vizuri ikiwa mamlaka hiyo itashauriana na wadau hao kuhusiana na namna ya kila upande kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa kwa lengo la kuwawezesha wasafirishaji kutoa huduma bora kwa wateja.
Inabidi ufike wakati wasafirishaji watoe huduma kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu bila kusubiri kubanwa na mamlaka husika.
Itakumbukwa jinsi wenye daladala na mabasi walivyokuwa wakilalamika kutokana na kubanwa na kampuni ya uwakala ya Majembe Auction Mart kuhusiana na kukiuka sheria za barabarani.
Tunaamini kuwa mashauriano yanayoendelea baina ya wadau wa usafirishaji na Sumatra yataleta mwafaka kabla viwango vipya vya nauli kutangazwa.
Ni matarajio yetu kuwa viwango vipya vitapangwa kulingana na hali halisi iliyopo na bila kuwaumiza wananchi ambao kila wakati wanaendelea kubeba mzigo kutokana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za huduma na bidhaa.
CHANZO: NIPASHE
 
Nilishawahi kuuliza hili swali lakini sijajibiwa.

Hivi Tanzania hakuna watu wajasiri kama Akina Kambona, marehemu Bibi Titi n.k?
Au TPDF hakuna mzalendo yeyote aka'organize mambo ili alikomboe Taifa hili?
 
Nilishawahi kuuliza hili swali lakini sijajibiwa.

Hivi Tanzania hakuna watu wajasiri kama Akina Kambona, marehemu Bibi Titi n.k?
Au TPDF hakuna mzalendo yeyote aka'organize mambo ili alikomboe Taifa hili?

Hao wanajeshi si wanapanda bure? Wanaitwa MAWE, unadhani wana akili ya kufanya rev wakati washapewa kombat mpya?
 
Taaaaaanzaaaaaaania Tanzaniaaaaaaa Nakupendaaaa kwa moyo wooooooooooooooooooooooooteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Nchiiiiiii yanguuuuuuuuuuu tanzaniaaaaaaa Jinaaa lakooo nitamuuu sanaaaaaaaaaaaaaa
:loco::loco::loco::loco::loco::loco::loco::loco:
 
Unafahamu maana ya amani wewe? Katafute kamusi ujielimishe kwanza. Kwasababu tu watanzania walikuwa wavumilivu wa kureact haina maana hiyo ndio amani. Imani itakuwepo vipi kama mwenzako anakula paja la kuku halafu hapo hapo anakunyang'nya hata huo mchicha wa kuchemsha unaokula? I think the mesage on your avatar should seriously be applied to you!!
 
Kwa mfumo huu maandamano hayatakwisha.
Ccm itatumaliza kwa risasi.
Mabasi mengi ni ya wakubwa serikalini sio siri na wala hamna kificho
 
EEee mungu wa israel na isaka tunusuru nchi hii tupe akili na mawazo ya kuwachinja wale wote wanaopelekea haya kwa kuanza na mmiliki wa DOWANS pamoja na wengine wote ambao kwao Nauli kupanda na umeme sio tatizo kwani wanatumia bure na zinalipwa na serikali kwa kutumia Kodi zetu walalahoi.

Hutawasikia wakichangia kitu kwani kwao sio la muhimu maana maumivu hakuna eee baba yetu tusikie na utupe nguvu.

AMEN.
 
mbona huduma zenyewe ni mbov?kwani kusafiri ni anasa,watu wanasafiri kwa 7bu bwana,mbona hawa wana2tesa,kuna mabas ukipanda mvua iknyesha,unalowa kama upo chni ya mpapai,PUMB*V ZAO
 
Back
Top Bottom