Hapo nimekupata!Tatizo ndio lipo hapo; kwanini wabunge walisahau kuhoji hayo wakati kamati ile inawasilisha ripoti yake bungeni na wakaridhika tu na takwimu za milioni tisa mapato kwa siku na milioni 5 surplus kwa mwezi?
Kwa mtazamo wako finyu basi hata matatizo kama msongamano wa magari sio tatizo la serikali maana ni wajibu wa kila mtu kufika anakoenda bila kujali atafikaje. Pia kwa mtazamo wako hamna sababu kwanini watu wenye vyombo vya moto vya usafiri walipie matumizi halafu waenda kwa miguu wasilipie! Kwa maana hiyo hata wapita kwa miguu wawe na road licence.Angewaambia waenda kwa daladala kama huna nauli tembea kwa mguu asingekuwa dharau, lakini kupiga mbizi imekuwa dharau. Na leo serikali ikisema imeshindwa kuendesha kivuko. Watu watafanya nini?
Hivi ni wajibu wa serikali kuwasafirisha watu wa kigamboni? kama ni hivyo basi serikali hii ina ubaguzi wa hali ya juu sana. Maana kule kwetu sijaona usafiri wa serikali, tena mtu akiuugua wanamchukua kwa machela na maanisha machela ya miti miwili na fito, harafu wanatembea kilomita zisizopungua 30 kuifikia hispotali.
Sasa nauliza, hili la kigamboni ni wajibu wa nani ku make shua anafika eneo lake aliloamua kuishi. Mhhh
Mchambuzi,
Asante kwa maoni yako, hoja zako ni nzuri kwa kuchochea mjadala ingawaje hauko sahahi katika maeneo kadhaa kama ambavyo nitakuja kueleza baada ya kwanza kujibu kauli za Magufuli hoja kwa hoja.
JJ
Hiyo inaonesha chadema ni kioo cha ccm, yaani ccm wakifanya jambo hawajali kuwa wanaccm wenzao wanasema nini maana wanajua kuwa kuna maiti tupu, wakifanya kitu hutathimini kwa kuangalia chadema wamesema nini. ndo maana hata baada ya wabunge wa dar kumpinga yeye ameona kama vile ni mnyika peke yake ndio wa kujibiwa maana wakielewana na mnyika basi wengine ni takataka.hata magufuli naye alipoongea na waandishi wa habari, alisema anamshangaa sana mnyika as if mnyika alikuwa peke yake kwenye hiyo hoja.
Toka Magufuli atoe kauli nimekuwa kimya kumjibu nikiendelea na majukumu mengine jimboni na ya kitaifa. Magufuli hakujibu hoja, na badala yake ametoa kauli zisizokuwa na ukweli wowote dhidi yangu, kauli potofu zikiachwa zitaonekana milele kuwa sahahi. Kwa hiyo nimeamua kesho nizungumze na wanahabari kuweka msimamo wangu wazi ili kuweka rekodi muafaka: Mosi, nitajibu hoja kwa hoja, kwa masuala yote aliyoyasema dhidi yangu. Pili, nitaweka bayana kwanini nimeunga mkono kwa GN ihairishwe kutekelezwa, hoja za msingi zijibiwe na mabadiliko muhimu yafanyike.
JJ
Angewaambia waenda kwa daladala kama huna nauli tembea kwa mguu asingekuwa dharau, lakini kupiga mbizi imekuwa dharau. Na leo serikali ikisema imeshindwa kuendesha kivuko. Watu watafanya nini?
Kwa mtazamo wako finyu basi hata matatizo kama msongamano wa magari sio tatizo la serikali maana ni wajibu wa kila mtu kufika anakoenda bila kujali atafikaje. Pia kwa mtazamo wako hamna sababu kwanini watu wenye vyombo vya moto vya usafiri walipie matumizi halafu waenda kwa miguu wasilipie! Kwa maana hiyo hata wapita kwa miguu wawe na road licence.
Kwa hiyo unadhani hiyo sh. 100 itatosha kuendesha hicho kivuko? Kwani tatizo ni nauli kuwa ndogo au ni ubadhirifu kwenye mapato ya kivuko?
Haya sasa mnaona Mnyika naye anaanza kucheza Politics ktk swala kama hili. Alichosema Magufuli hakihitaji kujibiwa mwache akushangae, wewe tetea maslahi ya wananchi kama unaamini yamekiukwa na zungumza unataka iwe nauli za guta zipunguzwe au makosa yako wapi. Hizi habari za kurushiana maneno mkuu wangu hazifai hata kidogo maana Magufuli anaifanya kazi yake kama Waziri kofia ya pili mlomvika na sii kama Mbunge...
Mnyika sisi wanajanvi tunakutaji hapa.. na binafsi naamini kabisa kama sikukusikia vizuri ulichogomba ni matumizi ya matusi ktk lugha ya waziri lakini kama unasema Tsh 100 inatosha kuendesha mradi wa Pantoni kigamboni bila shaka utakuwa umepewa report mbaya sana na kusema kweli binafsi siamini hata wanaposema mapato kwa siku ni Mil 9. Hii sii kweli kwa sababu kila siku ina mauzo yake na huwezi kabisa kunambia kila siku mauzo yanalingana kuwa millioni 9 kisha ati salio surplus ni Millioni 5 kwa mwezi sijui baada ya matumizi yote ama kabla ya kulipa mishahara - Profit and loss account.
Sasa najua wewe unajua zaidi ya hayo nakuomba uje hapa utwambie kwa nini unaamini Tsh 100 inatosha kuendesha mradi ule bila kukisia isipokuwa kwa kutumia takwimu za mapato na uendeshaji wa kivuko hicho..
Hapa umetoa ushauri wa maana lakini unatafuta hasira nyengine za wenye kufaidika nayo.Kama Mnyika alivyokosa hekima kuhusu sakata la kivuko na hapa watu wa maana katika JF wanaweza wakakuwacha mkono wakifikiria nani anayefaidika na misamaha ya kodi na nani wanaoumia zaidi.· Ibaneni serikali juu ya misamaha ya kodi kwa mwaka ambayo inakaribia asilimia 20 ya bajeti nzima ya mwaka, na muelekeze suala la subsidy ya kigamboni huko, sio kwa magufuli.
Ndio maana nikawarudisha watu nyuma wakumbuke kwamba UDA ilikufa kwa sababu - WALISEMA -Nyerere sio mchumi huwezi kutoza watu Tsh 1 kwa usafiri japokuwa dollar ilikuwa Tsh17 hiyo ilikuwa kama senti 6 kisha ikapandishwa hadi Tsh 5 (sent 30) bado haikutosha leo hii watu tunalalamika na kuongezeka Tsh 200 ili kufikia senti 13 ya dollar... gharama za kuendesha Pantoni au gari Tanzania ni ghali sawa au kuliko Ulaya kwenyewe..Tanzania kila sehemu ni wabadhirifu sana, na hata hivyo kiuhalisia nauli hiyo haitoshi kuendesha kituo. Sh100 ni sawa cent 5 za EURO, ha ha ha na ukumbuke mafuta yananunuliwa kwa dolaaaa ama eurooooooo. Na hayauzwi bei rahisi kulingana na umasikini wako ama wangu.
Serikali ilikuwa wapi muda wote wa miaka 14 isipandishe nauli kama walivyokuwa wanapandisha sehemu nyingine? Why now?Magufuli si suluhisho ukweli nauli ya shs 100 haiendani na wakati;
Why not now? maana ukifikiria hivyo basi hakuna siku inayotakiwa kufanya mabadiliko..Mzigo ukikuelemea unautua na Magufuli hakuwa wizara hiyo kwa miaka yote 14..tatizo letu nini hatutaki kulipa kwa sababu kasema maghufuli au kwa sababu ambazo yeye kazisema na kawakilisha hadi bungeni.. Kila waziri ana mtazamo wake ktk maswala wengine hawakujali na ndio maana Pantoni kibao nyuma zimekufa haraka nyingine karibu kuua watu..Serikali ilikuwa wapi muda wote wa miaka 14 isipandishe nauli kama walivyokuwa wanapandisha sehemu nyingine? Why now?
Why not now maana ukifikiria hivyo basi hakuna siku inayotakiwa kufanya mabadiliko..Mzigo ukikuelemea unautua na Magufuli hakuwa wizara hiyo kwa miaka yote 14..
Mchambuzi,
Asante kwa maoni yako, hoja zako ni nzuri kwa kuchochea mjadala ingawaje hauko sahahi katika maeneo kadhaa kama ambavyo nitakuja kueleza baada ya kwanza kujibu kauli za Magufuli hoja kwa hoja.
JJ