Nauchukia udaktari. Wanafunzi msiusomee. Hauvutii kama Ubunge, Uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauchukia udaktari. Wanafunzi msiusomee. Hauvutii kama Ubunge, Uwaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kieleweke, Jul 7, 2012.

 1. K

  Kieleweke Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza combination yake unapoingia form five ni Physics, Chemistry na Biolology (PCB), au Chemistry, Biolology, Geography (CBG).

  Anyway siku hizi University zimekuwa kibao hivyo maadam una Biology na Chemistry basi kuna kila linalowezekana ufike form six na baada ya hapo usomee udaktari.

  Zamani Chuo kilikuwa nikimoja tu hapa nchini yaani Muhimbili. Sasa vimeenea kila kona. Kuna Kairuki, Kuna Bugando nasikia Ifakara nako kumefunguliwa. Du viko tele.

  Turudi kwenye yale masomo yaani Biology, Chemistry, Physics. Hakuna aliyepita sekondari asisimulie kuhusu masomo haya. Na ndiyo yanayoongoza kwa wanafunzi kufeli. Hivyo ni masomo magumu kuliko maelezo.

  Najua kuna watu wanayatandika A au B lakini inabidi uwe kichwa kwelikweli.

  Serikali inajua ugumu wa msomo hayo, inajua wanafunzi wanayachukia. Inafanya kampeni nyingi kusisitiza wanafaunzi wasichukie masomo ya sayansi.

  Lakini wakati serikali inasisitiza tukimbilie masomo haya, tunaona madaktari ni moja ya fani chache za sayansi zinazoongoza kwa migomo. Kuanzia mwaka 2000 hadi leo si chini ya migomo sita.

  Lakini sijawahi kusikia meneja wa kamouni akigoma. Sijawahi kusikia Waziri akigoma. Sijawahi kusikia mahakimu au majaji wakigoma. Tena wale wasiogoma masomo waliyosoma utaona wengi ni yale kama history, geography, Kiswahili, English, French kwa kifupi yanaitwa arts.

  Sasa kwa nini kama ninasoma nijihangaishe na masomo maguumu ya kuumiza kichwa wakati najua nikianza kazi nitaumiza kichwa tena kugoma na kuamziwa nichague kuendelea na kazi au nifukuzwe kazi.

  Hivyo, nimeamua sitaki udaktari kwa sababu ambazo sasa hata mtanzania wa umri wa miaka sita najua. Udaktari na migomo ni pete na kidole.

  Nataka kazi zile ambazo zitanifanya niwe na nyumba Mbezi_Beach (Dar), Capri_Point (Mwanza) na sehemu ya mji wowote ambako tunapaita "Uzunguni".

  Nitakuwa wa ajabu kumshawishi mwanafunzi asomee udaktari. Asomee wa nini? Umsaidie nini?

  Niseme nisiseme> Ninataka mwanafunzi asome awe mbunge au Waziri. Na ndiyo maana na wao siku hizi wanafunga safari nyingi kwenda kutembelea Bunge ili siku moja waje wawe wabunge waachane na njaa ya kugomagoma ya udaktari.

  Cheers
   
 2. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  message imefika
   
 3. Kenneth Mwazemb

  Kenneth Mwazemb Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We kijana umesema kweli kabisa, tatizo lililopo ni kwamba udaktari ni fani ya kale mno na ina watu wake. Sayansi kawaida wasomi wake wanakuwa na vichwa moko kidogo kwasababu ya kubundia. Mtoto mmoja aliulizwa swali akimaliza shule angependa afanye kazi gani au awe nani alidai anataka awe fisadi akijua kuwa kuitwa fisadi Tanzania ni heshima kwani mafisadi ndiyo wenye fedha nchi hii, wanatembelea ma-VX, wanaheshimika na wanaitwa waheshimiwa.
   
 4. Advicer

  Advicer JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Usitukane fani kama uliopt physics and chemistry.ingawa co magumu kama muwazavyo.
   
 5. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wapo ambao watatoa kejeli , ila ukweli utabaki ni wachache ambao si madaktari ila vichwa vyao
  vinaruhusu kusomea udaktari au fani kadhaa za sayansi ,yafaa nini kuonekana mzuri darasani tangu
  utotoni hadi kidato cha nne mnapoanza kuachana , lakini , mwisho wa siku uliyekuwa unampita ndo
  anakuja kuthaminiwa zaidi
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  hujui tofauti ya profession na cheo au nafasi ya uongozi .... Udaktari ni profession na ubunge/uwaziri ni vyeo tu au uongozi ambavyo huingii darasani kusomea.... anyway go back and review your IQ
   
 7. m

  mtanzania1989 JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 2,138
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Wapo ambao watatoa kejeli , ila ukweli utabaki ni wachache ambao si madaktari ila vichwa vyao
  vinaruhusu kusomea udaktari au fani kadhaa za sayansi ,yafaa nini kuonekana mzuri darasani tangu
  utotoni hadi kidato cha nne mnapoanza kuachana , lakini , mwisho wa siku uliyekuwa unampita ndo
  anakuja kuthaminiwa zaidi
   
 8. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza ubunge au uwaziri sio professional hvyo duniani kote hakuna chuo kinachofundsha non professional!
  Pili sio kosa kuwashauri wanafunzi ila hujawashauri vizuri na kwa uwazi! Kwanza, binafsi nimesoma arts tokea form three hadi form six na chuo kikuu nasoma kozi za social science. Nautambua ugumu wa science na nautambua ulaini wa arts! Lakin mwisho wa siku wanafunzi wa science vyuoni wanapewa motivation kubwa zaidi kuliko wa kozi nyingne, mfano, wakati wanafunzi wa social science wakiwa hawana mkopo kabisa (kuanzia mwaka huu), wanafunz wa education wakipewa 50% wao wa science wana 100% plus pesa za field na kununulia vifaa vya kujifunzia pamoja na pesa za books and stationary!
  Pili, vijana weng unaowaona wanazunguka na bahasha town wakitafuta ajira karibia wote hawajasoma kozi za science, wanafunzi karibia wote wa kozi za science wana uhakika wa ajira baada ya masomo yao!

  Kuhusu wanascience wengi kutokuwa na maisha mazuri kama wanaarts wengi jibu nadhan ni rahisi, wanascience hawana hayo maisha kwa sababu hawana elimu ya social science! Sidhan kama wanascience wanafundshwa namna ya kuishi na watu (social interaction), sidhan kama wanascience pamoja na kupata mshahara mkubwa zaidi ya watumishi wengine wengi tu wanajua how to run their social life!
  MBALI NA HAYO MACHACHE KOZI ZA SCIENCE NI NZURI SANA NA BINAFSI NAWASHAURI WANAOZISOMA KUZISOMA KWA MOYO ILI NCHI IWE NA WANASCIENCE WENGI!

  Kuhusu mgomo wa madaktari mi nadhani hayo ni mapambano ya kuiboresha sekta ya afya ili iwe bora na yenye manufaa kwao wenyewe na kwa jamii kwa ujumla na sio busara kuutumia kuwadiscourage wanaosoma masomo ya science!
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hata walimu wa science wanalalamika kukosa 'semina' kulinganisha na wenzao wa arts.
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Iko wapi chuo cha ubunge?
   
 11. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  ukweli ni kuwa serikali ni legelege!
   
 12. C

  Cape city Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  U are talking nonsense...
   
 13. L

  Lorah JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wasisome udaktari serikali ya CCM itaagiza madaktari nje hahahaha hivi mbona hawafiki jamamani kweli Serikali ya CCM ni DHAIFU NA RAIS NI DHAIFU...
   
 14. D

  Deofm JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Profesa Shaba aliwahi kumweliza Nyerere hili, alipojifananisa maisha ya shuleni na mh Daudi mwakawago na baadae kulinganisha maisha yao ya ajira. Nyerere alimpeleka shaba ulaya akachunguzwe kwa nini analewa hivyo. wazungu wakamwambia hawajawahi kuona kifaa kama hicho, wakaomba wabaki nae lakini Nyerere alikataa akamrudisha hapa bongo ambapo alikuwa hapate pesa ya kutosha hata bia hivyo aliendelea na gongo hadi maisha yake yakaharibika.

  hatari kwa taifa, watoto wetu wanataka maisha mazuri kwa jasho kidogo, haya yanapatikana kwenye usanii, uongozi na sheria, kwa hiyo serikali inapobishana na madaktari hadharani inawafanya watoto waogope kuwa wanasayansi.

  Vipi kuhusu ile posho ya sh, 200,000/= kwa siku, wahesimiwa si wanalipwa nje ya mishahara yao?

  Tupunguze hizi tuongeze motisha kwa wanasayansi vingineyo nchi yetu kila kitu tutaomba India. Maendeleo ya kisanii hayalisaidii taifa. Rais Museveni alizungumza hivi majuzi alipoona kuwa sekta ya sanaa imekuwa kwa 8% na ile ya kilimo kwa 1%.

  chonde chonde rais wetu, ingawa wewe ni MSANII, lakini usiwabugudhi wanasayansi hivi, kwani ukiendelea hivi utakumbukwa kwa karne nyingi zijazo kama MSANII MAARUFU DUNIANI.
  :A S cry:
   
 15. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Mimi baba yenu nina ushauri tofauti na wewe mtoto! Soma Science halafu achana nayo tafuta nafasi za kisiasa. Si mnaona wabunge maprofesa wa science wamo bungeni. Bilal ni nuclear scientist/physicist and I can dare say that he has never and will never practice nuclear physics!!!
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hujawahi kusikia meneja wa kampuni amegoma, sawa. Je, umeshawahi kusikia mganga mkuu wa hospitali amegoma? waganga wakuu ndio wanaofukuza madaktari waliogoma. Meneja ni sawa na mganga mkuu.
  Kama udaktari umekushinda ni udhaifu wako mwenyewe na sio kosa la taaluma ya udaktari. Huna skills za kuuza ndio maana, wenye skills wanaenjoy profession yao fresh tu...
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  haya matatizo ya sasa si ya kudumu yanapita. Tunahitaji madaktari tena sana. Tusiache mbachao kwa msala upitao. Naungana kabisa na Albert Einstein aliyewahi kusema " In the middle of a crisis, lies the opportunity". Hii ni fursa kwetu kama nchi kukabili changamoto zilizopo for better!
   
 18. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ubunge na uwaziri hausomewe wewe! Wengi wa wabunge namawaziri wana professionals zao.
  Madaktari wapo, waandisi wapo, wanasheria wapo, n.k.
  Mkitambua hilo, mtajadiliana vyema.
  Turudi tulikotoka - zamani siasa / uongozi ilikuwa kazi ya watu wenye busara, wazee, na wasioweza kuzalisha. Watu wenye nguvu zao walishughulika na kazi za uzalishaji mali, katika kuzalisha waligundua vitu vingi ambavyo ndo sasa hivi vinatusaidia kama vitendea kazi.
  Mambo yalipoharibuka - hata watu wenye nguvu, professionals zao waanza kuonja kazi za kiuongozi / kisiasa - wakawa wanakimbia professionals zao.
  Nakumbuka wakati wa ujana wangu nilikuwa napenda kumtembelea Daktari mmoja mzee, alikuwa na hospitali yake. Kwa kweli alikuwa akinieleza mambo mengi kuhusu serikali yetu enzi zile. Moja na kubwa alonieleza na siwezi kulisaau alisema hivi ....
  "Rais wetu ndo aliiharibu nchi, wasomi wengi alikuwa anawateua kuwa mabalozi, aliingiza siasa sehemu za kazi lakini kwa uficho mkubwa"
  Wasomi hawa walipoonja raha ya kukaa bila kufanya kazi ndo waambukiza watoto wao kupendelea kazi raisi raisi kama za kusimama majukwaani na kubwabwata maneno ya kukopi na kupest. Wanashinda na vitabu vya wana-falsafa wakikariri vimisemo mbalimbali ili wakisimama kwenye mikusanyiko waweze kushangiliwa - WIZI MTUPU
  Someni masomo ya sayansi muwe watenda kazi kama mtakavyokuwa mmeteuliwa na Mungu.

   
 19. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kumbe tuko wachache tunaotambua hilo.
   
 20. K

  Kieleweke Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu sema kwa mujibu wa IQ yako ni mahala gani kwenye post yangu nimesema Ubunge, Uwaziri ni profession?

  Unadhani wakati ninapost sikujua kwamba ubunge si proffession ya kupata chuoni? Nimeandikapost kistaa nikijua mpo mtakaokurupuka kana kwamba nimesema hivyo ni profession.


  Wewe, unatakiwa kujibiwa majibu mengi, lakini jibu lako la kwanza ni kama la hao wawili, ila kwa sababu hujagusa neo IQ basi hayo ya IQ yanamgusa yule mwenzenu na si wewe.

  Napenda watu wasiomungunya maneno. Hapa nakupa 100%


  Mkuu, hayo hayana tofauti na wakati ule wa JKT ambapo mtu aliyetoka kozi kama ualimu alikuwa hakai kambini bali anapata kitengo cha kufundisha shule za jeshi. Hebu muulize mwalimu yeyote kama anapenda ualimu kwa kuwa jeshini kuna unafuu au kama kulikuwa na unafuu.

  Lakini ndiyo ajira hizihizi wanazogoma ambazo napenda mnipe majibu kwa nini tusikimbie


  Mkuu,
  Kuwa muangalifu unapojibu hoja hii. Madaktari wanafundishwa aina fulani ya phsychology ili kuweza kumkabili mgonjwa na hata ndugu za mgonjwa.

  Kuna jamaa humu kasema kuna kijana aliambiwa unataka ukiua ufanye kazi gani, kijana akasema nataka niwe FISADI. Na kama unavyosema ili uwe fisadi ni lazima uwe na SocialNetwork kubwa.


  Mkuu,

  Mwenye macho haambiwi ona na mwenye masikio haambiwi sikia. Mizozo ya madaktari unweza hata kuandika kitabu na kikanunuliwa na hakitakuwa chini ya page 150.


  Nakubaliana na wewe kuhusu future ya maisha yangu. Lakini mimi nimeongea ni terms of majority. Zaidi ya nusu ya wabunge ni wanasheria na ukiongezea fani zingine za arts zikiwemo practical arts kama zile za akina John Komba, Sugu, MajiMarefu nk. Bado hujawataja watangazaji kama Marehemu Amina Chifupa, Jenister Mhagama nk ndipo utapata picha ya ninachokisema.

  na hao ndiyo waliojaza majumba kule Mbezi_Beach ambapo la bei ya chini si chini ya milioni 700.
   
Loading...