Natupa line ya voda sasa

Natupa line ya voda sasa

Haya mavoda ni majambazi wakubwa. Hata mimi nahama mtandao huu wa wizi.
 
Mi nafikiri kama kungekuwa na maamuzi ya pamoja ya kuachana na mtandao kama huu ingekuwa vema! Maana sasa wanalewa sifa na kujiona wao ndo wao! Hawajui kwamba bila kupiga simu hata hiyo m-pesa inayowapa kichwa itapuputika! Mi nahamia airtel mapemaaaaaaa! Nao wakizingua naangalia kwengine maana wamenichosha! Uchafu!
 
Mimi nishaitupa line yangu ya Airtel wiki mbili zilizopita,sababu kila nikijaribu kujiunga Airtel tosha inaniambia huduma hii haipatikani kwa sasa jaribu tena baadae,kupiga simu Huduma kwa Wateja wakanijibu kuwa kuna baadhi ya line zina tatizo hili,nikasema ngoja nisubiri labda tatizo litaisha,kaa mwezi mzima hakuna mabadiliko. Kilichonifanya niitupe line ni pale unapoweka salio,mfano buku,ukipiga simu Airtel to Airtel dk mbili haziishi hela imeisha na ukilogwa ulaze salio kwenye simu umeliwa.

Nilichogundua ni kuwa zile line zote zilizoanza kutumia huduma hii ya Tosha katika hatua za mwanzo kabisa ndizo hizo zilizofungiwa,sasa sielewi hawa watu wana maana gani kutoa promotion biased namna hii.
 
Bando ya voda ilivyobadilishwa haimjali mteja na sijui kama huyo jamaa aliyetoa wazo hili ameliweka kiushindani au anataka kufanya nn.Nilikua naona kwamba haya makampuni ya simu yalikua yanarahisisha mawasiliano ila kwa upande mwingine naona lengo kubwa ni kutengeneza faida na hapa ndio naona Serikali kupitia Kale kajamaa TCRA wanatakiwa waseme kitu
wadau mnaonaje?

mimi nimeanza kuitumia airtel asubuhi...eti unapewa sec 8000 kwewmda voda halaf mitandao mingine sec 50.sijawahi ona upuuz kama huu toka nijiunge voda.bundle ndo hakuna kitu
 
voda wamenisikitisha sana, unaweka hela mara yote inapotea bila maelezo. Nimeacha kutumia line yao sasa niko na airtel tu!
 
Mgema akisifiwa,tembo uliweka maji! Ni wapuuzi sana.Wanarundika sms nyingi ,wanafikiri wote ni mabingwa wa ku chat. Nilisikia TCRA imefutwa?
 
Wote wafanya biashara. Tofauti ni ndogo sana.
Pili tuache kupenda vya bei rahisi.Tunalalamika tofaut ya shllingi mia 2 lakini tunazopoteza kwenye anasa hatuangalii.
Mie voda damu damu sijaona tofauti kubwa.
 
voda wamenisikitisha sana, unaweka hela mara yote inapotea bila maelezo. Nimeacha kutumia line yao sasa niko na airtel tu!

Hii ni kweli kabisa hata mimi inanitokea mara kibao. Yaani huu mtandao wa voda haufai kabisa kwa watu wanaoweka vocha za jero, buku au buku 2.
 
Hata mm natupa yakwangu.Haiwezekani wakate hela yangu hovyo hovyo.
 
Back
Top Bottom