Natoa ushauri wakati wa sensa ukifika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natoa ushauri wakati wa sensa ukifika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BLUE BALAA, Dec 13, 2010.

 1. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Sina uhakika sensa ya kuhesabu watu hapa kwetu Tanzania ni lini tena. Ila napenda nitoe ushauri wangu wakati ikifika watumie utaratibu ufuatao ambao utatumia muda mfupi na pesa kidogo. Mtanisamehe wana JF kama nitakuwa natoa iliterate ideas lakini pia muelewe mimi sina taaluma ya takwimu.

  Ikifikaga wakati wa sensa naonaga watumishi wa serikali wako busy sana na pia watu wengi wanakuwa involved lakini pia sina uhakika na accuracy ya sensa yenyewe. Sasa hivi kila mtu anatamka vyake kuhusiana na idadi ya watu Tanzania. Utasikia huyu milioni 42, 40, 36 na kadha wa kadha.

  MAWAZO:
  Hivi kila balazo wa nyumba kumi akiambiwa apeleke idadi ya watu wake na particulars nyingine kwa Afisa Mtendaji wa kata (WEO) Sidhani hata kama huyu balozi atahitaji kugonga hodi kwa kila mkazi kwani anajuwa nyumba zake zote zina watu wangapi, majina, idadi ya watoto na details nyingine zote. Na baada ya hapo WEO apeleke report yake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ili ziwe compiled na kutumwa takwimu.

  Mimi kwa njia hii naona sensa ingetumia wiki moja, kwa gharama ndogo sana tofauti na sasa hivi sensa huwa inatumia gharama kubwa sana za posho za watumishi, magari na mengineyo.

  Karibuni great thinkers
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  rts a brilliant idea. Naku sapoti, kuyosaki anafundisha umuhimu wa kua na matumizi chini ya mapato. Si hilo tu,hata wabunge kua na hostels dom ambapo watalala na pia watakula hapo kwa garama nafuu, pia wawe na ma bus ya bunge, ili wawe wanasafiria kwenda na kutoka dom, ili kukata garama ya mafuta ambayo hulipwa kwa kodi za wananchi, pia mshahara usizidi milion 2. Tukibana kiasi hicho lazima tutayatoa tu. Let me stick to the point sensa kwa style imekaa vizuri.
   
 3. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  I doubt uwezo wa mabalozi if they can collect and submit usefull details, I think we can not relay on mabalozi watupatia such datas.
   
 4. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  w
  why we cant stick on them? Why do you think they provide fake infos? May be you have a point, pointlize it here please, MISS NOT ENOUGH.
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,917
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Binafsi namwunga mkono mtoa hoja, ni nzuri na imeonesha njia mojawapo kufikia ufumbuzi wa tatizo la matumizi makubwa ya pesa bila sababu za msingi.. Nikirejea kwenye wasiwasi wako nakubaliana na wewe kuwa linaweza kutokea tatizo la hao mabalozi kutokuwasilisha data sahihi.

  Lakini hebu fikiria kuwa kabla ya sensa kufanyika waendeshaji wake hupewa semina namna ya kuhesabu watu na hiyo pia huigharimu serikali, Sasa basi, kama alivyosema huyu mtoa hoja, tukiwapatia semina mabalozi namna ya kuhesabu watu wao na kuwapa maelekezo yote yanayotakiwa naamini kabisa wataifanya hii kazi kwa ufasaha mkubwa pengine kuliko wale ambao huwa wanatumika mara kwa mara. Manake hawa mabalozi wana uzoefu mkubwa wa maeneo yao pamoja na kuwafahamu vizuri watu wa maeneo yao...
   
 6. D

  Diva Member

  #6
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 28, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba nichangie. Nashukuru kwa kuposti hii mada. Ilivyo ni kuwa, watu wengi si wapenzi wa mambo ya namba, au hawaelewi madhara yake kwa kutoa namba bila umakini. Uzoefu unaonyesha huwezi kabisa kuwategemea viongozi wa ngazi inayotajwa au yoyote kufanya kazi hii. Ni kazi ngumu sana ndio maana inafanywa kwa kuajiri watu kwa muda mfupi. Pia, sensa ya watu inafanyika sio tu kuhesabu idadi yao, bali kujua mazingira ya nyumba, umri, elimu, watoto waliozaliwa na kufa miaka kadhaa kabla ya kufanyika hiyo sensa nk. Sensa inatakiwa ifanyike ktk kipindi kimoja tu nchi nzima, hivyo haitakuwa sawa kuwategemea walete hizo takwimu kila mtu anapohamia, labda kama kila MTZ anapokuwa na ID kiasi kwamba ukimjumlisha alipohamia, unamtoa alikotoka. Mbali na hivyo utahesabu mara mbili au zaidi na kupata matokeo si sahihi. Baada ya kuwa sensa imeshafanyika, huwa pia tunapata kiwango cha ukuaji kwa idadi ya watu, idadi ya kaya na mengineyo kwa mwaka. Hii ndio wengine wanaitumia baada ya sensa kukadiria ukuaji kwa miaka inayofuatia. Wataalam wa elimu ya idadi ya watu (demography) wanasema kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu hakibadiliki kwa kipindi kifupi, hivyo unaweza kukadiria (projection) ya miaka inayofuata. Kwenye kufanya projections kuna kanuni mbalimbali, hizi ndizo huleta utofauti wa kukadiria huku, ndio mana wengine wanasema 46, 35 mil nk, wanapaswa waseme wametumia kanuni gani na ni kwa mwaka gani. Kwa mfano ikiwa linear growth unafanya tu asilimia ya ukuaji x idadi ya leo x idadi ya miaka unayotaka kukadiria. Lakini pia zipo kanuni za exponential, geometric nk. Kila jamii inakua tofauti na kila anayefanya projection kutegemea na mahitaji yake na assumption zake. La muhimu ni kutafuta takwimu zinazokubalika kitaifa za kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu au tafuta mtaalam akufafanulie.
  Mwisho, viongozi wetu wa vitongozi hawajafika hapo tunapofikiria. Hata nchi zilizoendelea hawajafika kuwatumia viongozi hawa, lkn kubwa likiwa si rahisi kuasimamia wafanya hili kwa muda mfupu uliopangwa ili kuwezesha projections zifanyike kimahesabu yanayokubalika. Mmoja alisema gharama ya sensa utaipima utapokuwa huna hizo takwimu (the cost of census is the cost of not having the data).
  Nadhani nimesaidia
   
Loading...