Natoa Siri, moja ya sababu ya Vita vya Ukraine ni kama yanayotokea sasa muungano Zanzibar na Tanzania bara

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,997
3,949
Nataka Kusema, mgogoro uliopo Sasa kati ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza kuja kuleta madhara baadae kama ilivyokuwa madhara makubwa ya vita ya Ukraine na Russia, ambazo awali zilikuwa nchi moja na Mtawala wa Soviet union aliye na asili ya Ukraine kufanya maamuzi ya kupendelea Ukraine wakati akiongoza.

Hapa hakuna porojo, sikilizeni Rais wa Muunganiko wa kisovieti kama ilivyo Zenji na Tanganyika aitwaye Nikita Khrushchev yeye alikuwa na asili ya Ukraine na alizaliwa Ukraine, wakati yupo madarakani kwakuwa alikuwa mzaliwa wa Ukraine alilitwaa eneo la Crimea lililokuwa eneo la Haki la jamhuri ya Urusi na kulifanyia sehemu ya Ukraine nyumbani kwao alipozaliwa.

Sasa baada ya Soviet Union kujifia nchi zote zilizoungana zilitengana na hapo Ukraine akawa akidai Crimea ni eneo lake, na Urusi akisema hivyo hivyo jambo lililoleta vita. Sababu ikiwa Rais aliyekuwa madarakani kwakuwa hakuwa mrusi alifanya umafia wa kuhamisha eneo.

Tundu Lissu anayosema Leo yana ukweli kabisa, kwani maeneo ambayo ni Mali ya Tanganyika kipindi hiki Cha muungano na Rais anatokea sehemu ingine anaweza akafanya vitu bila kujali Kwa kuwa yeye Hana asili ya Tanganyika. Hivyo huko baadae kuja kuleta mgogoro kama ulivyo wa Urusi na Ukraine kuhusu Crimea.

Hivyo tujadili HOJA, nyakati zitapita na haya mambo yatarudi baadae.
 
Back
Top Bottom