Natoa pole kwa mapacha walioungana, Consolatha na Maria

Mapacha walioungana, Consolata na Maria bado wanaendelea kutibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam.

Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika hospitalini hapo kuwajulia hali na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Nasi Jamii forum tunamwomba Mungu ili Consolata na Maria wakapate kupona na kurejea chuoni kuendelea na masomo yao.
View attachment 693672

Wakuu hivi consolata na maria akiumwa mmoja wanaumwa wote?
Ndugu wana jf tuwaombee ndugu zetu wapone.

Yule ' Tapeli ' wa Kutukuka aliyepo nchini India amewaona hawa ' Wagonjwa ' wa kwelikweli?
 
Anawaza akifariki mmoja itakuwaje. Anaumwa mmoja na kila mmoja ana moyo wake ila kwa kuwa hawawezi kutengana imebidi walazwe wote. Akifa mmoja ndo swali linalomwazisha mwenzangu. Nami linaniwazisha maana sijui sayansi. Moyo na ubongo kila mmoja anajitegemea ila kwenye kiwiliwili kuna viungo wanashea. Ikitokea huyo mgonjwa akafariki halafu viungo vilivyoungana vinaendeshwa na ubongo wa aliye hai itakuwaje? Nawaza yule hai atajisikiaje kuona maiti ya mwenzie? Madaktari watamharakishia kifo au watamchelewesha marehemu kuoza? Nawaombea uzima hawa mabinti.
Dah.. So sad.
Mimi naamini MUNGU atawalinda tu na hawatopatwa na baya lolote
 
Anawaza akifariki mmoja itakuwaje. Anaumwa mmoja na kila mmoja ana moyo wake ila kwa kuwa hawawezi kutengana imebidi walazwe wote. Akifa mmoja ndo swali linalomwazisha mwenzangu. Nami linaniwazisha maana sijui sayansi. Moyo na ubongo kila mmoja anajitegemea ila kwenye kiwiliwili kuna viungo wanashea. Ikitokea huyo mgonjwa akafariki halafu viungo vilivyoungana vinaendeshwa na ubongo wa aliye hai itakuwaje? Nawaza yule hai atajisikiaje kuona maiti ya mwenzie? Madaktari watamharakishia kifo au watamchelewesha marehemu kuoza? Nawaombea uzima hawa mabinti.
Nimejikuta nalia.Mungu wasaidie hawa watoto maana hapa ndo akili za kibinadamu zinapoishia kufikiria.
 
Mtu akiyajuwa mapenzi ...moyo lazima uende ndivyo sivyo...yaani moyo sukuma damu ...bt Get wll soon..our twins.
 
Hh
Anawaza akifariki mmoja itakuwaje. Anaumwa mmoja na kila mmoja ana moyo wake ila kwa kuwa hawawezi kutengana imebidi walazwe wote. Akifa mmoja ndo swali linalomwazisha mwenzangu. Nami linaniwazisha maana sijui sayansi. Moyo na ubongo kila mmoja anajitegemea ila kwenye kiwiliwili kuna viungo wanashea. Ikitokea huyo mgonjwa akafariki halafu viungo vilivyoungana vinaendeshwa na ubongo wa aliye hai itakuwaje? Nawaza yule hai atajisikiaje kuona maiti ya mwenzie? Madaktari watamharakishia kifo au watamchelewesha marehemu kuoza? Nawaombea uzima hawa mabinti.
nimewaona mara nyingi sana tokea wakiwa watoto huko ikonda makete wakiwa shule hadi chuo. Wanapitia changamoto nyingi sana zinazoumiza ktk maisha ya mwanadam.majibu ya maswali yenu ni magumu kujibika.nawaomba sana mwakumbuke ktk maombi yenu kila wakati
 
So sad, Mungu wajaalie rehema wana wako.

Matatizo tunapitia ila hawa mapacha wananihuzunisha sana. Mungu simama nao.
 
Hh
nimewaona mara nyingi sana tokea wakiwa watoto huko ikonda makete wakiwa shule hadi chuo. Wanapitia changamoto nyingi sana zinazoumiza ktk maisha ya mwanadam.majibu ya maswali yenu ni magumu kujibika.nawaomba sana mwakumbuke ktk maombi yenu kila wakati

Hakika. Kibinadamu tunaomba uzima tu lakini kiuhalisia uzima, mateso na kifo tumeumbiwa sisi na kila kimoja kitahusika kwa wakati wake. Tuwaombee nguvu ya kuhimili kikombe wanachonywea sasa.
 
Back
Top Bottom