Tujenge mnara wa kumbukumbu kwa ajili ya mapacha Maria na Consolata

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,135
729
Kwanza kabisa niungane na Watanzania wote katika kuomboleza msiba mzito wa wapendwa watoto wetu Maria na Consolata.
Kutokana na jinsi wazazi, Walimu na hasa mapacha walioungana Maria na Consolata kuonyesha bidii ya kipekee ya kutafuta elimu hadi kufikia chuo kikuu, nashauri yafuatayo.

1.Marehemu watunukiwe digrii ya heshima ambayo watapokea wazazi kwa niaba.

2.Ujengwe mnara wa kumbukumbu kuenzi juhudi za Maria na Consolata katika kutafuta elimu kwa ajili ya kuja kuwa walimu kwa wenzao.

Naomba tupaze sauti zetu ili mashujaaa hawa kumbukumbu yao idumu kizazi hadi kizazi.

Karibu tupaze sauti zetu.
 
Digrii inamsaada upi mkuu kwa wazazi
Inawezekana una mawazo ya msaada wa pesa. Lakini ujue kutambua juhudi za mtu kuna maana sana katika maisha ya huyo mtu. Msaada sio pesa tu kutambuliwa kunafungua milango kwa watu wenye nia njema kuendeleza kipawa cha mtu, kinamwongezea kujiamini n.k.
 
Kumbukumbu ipi....?kwamba walisoma mpaka chuo..?Hao ni Mapacha wa mwisho walioungana?Je wakitokea wengine tutaendelea kujenga minara ya ukumbusho..?Maswali ni mengi tu..Fafanua
Ni .mabalozi wa campaign ya DISABILITY IS NOT INABILITY.
Kuanzia wazazi hadi wenyewe wameishi hiyo kauli. Je hujasikia hapa kwetu walemavu wakifichwa na wazazi? Hujaona ombaomba kwa watu wenye ulemavu ambao wangeweza kujitegemea?
Hujasikia baba akimkimbia mkewe kisa kazaa mlemavu.
Kumbukumbu hiyo ni mwanzo wa Campaign hiyo.
 
Akili zingine hizi mhhh!
Ukute mawazo kama haya ndio mtu anakuwa rais wetu.

Matokeo yake ndio kama kina lisuu wanapigwa risasi ben haonekani kkt inataka kufutwa.
Basi tu ili mradi zero thinking and wastage of time.
 
Ni .mabalozi wa campaign ya DISABILITY IS NOT INABILITY.
Kuanzia wazazi hadi wenyewe wameishi hiyo kauli. Je hujasikia hapa kwetu walemavu wakifichwa na wazazi? Hujaona ombaomba kwa watu wenye ulemavu ambao wangeweza kujitegemea?
Hujasikia baba akimkimbia mkewe kisa kazaa mlemavu.
Kumbukumbu hiyo ni mwanzo wa Campaign hiyo.
Chanzo cha yote uliyataja ni umasikini.
Inua jamii yako kiuchumi utawaona vilena wote wanapelekw shule
 
Back
Top Bottom