Nationalisation is back: Utaifishaji kwa manufaa ya umma!

bado sijaona njia kuu za uchumi nchi hii zinazoendeshwa (owned) na private sector ambazo zina- perfom efficiently

Tuna vibwanyenye uchwara eti vinajiita vibapari....
Wanahujumu na kuua reli ili wafanye biashara ya Malori.... only in Tzanzania haki ya Mungu!
 
Wanafalsafa walishasema public property is less productive!

Sasa mnataka kuturudisha zama za mashirika ya umma,ugawaji na vyama vya ushirika ambavyo viliwafanya wachache wawe mabilionea.Mashirika kama BIMA, SUKITA, NBC, General Tyre, Urafiki, Tanganyika Packers (imebaki scraper), UFI, Mwatex nk

Watu wachache waliyaua haya mashirika wakayaacha hoi. Angalia ATCL na TRL kila mwaka tunawa bail out wanamaliza hela ya walipa kodi.Imagine tuwe na mashirika 50 tegemezi si kodi yote itaenda huko tutashindwa hata kununua panadol!

Lakini wenzetu Argentina na Bolivia wameamua kuyarudisha yale mashirika waliyoyauza kwa wageni ili wa-reinvest.
Je sisi tuliyoyauza yanaendeleaje?
Mengi ni magodown ya mali toka China na kwingineko.
 
Mbona hata uko UK na USA mabenki yalikuwa na mengine hadi leo bado yako "natioalised" katia % fulani baada ya mdororo wa uchumi na kuonekana eti they were too big to fall. Yes pesa zawalipa kodi zikakomboa mabenki ya mebapari.

Kwa hiyo sio Bolivia na aregetina tu.
 
mfumo wa serikali za america ni tofauti na za kwetu huku...sasa serikali yetu ya hapa itaifishe viwanda alafu msimamizi wake awe mkullo?? ni bora nione mzungu au mwekezaji wa nje anafanya kazi hapa kuliko nione akina mkullo na ngeleja wakiwa in charge....
 
Hii mada inahitaji uchambuzi wa kina. Kwa maana ya tulikuwa na nini kabla ya utaifishaji,tukataifisha tukawanavyo,tuliviendesha vipi, kwa ufanisi upi, tukabinafsisha vingi ,kwa taratibu zipi na mategemeo yapi. Na mwisho yapo katika hali gani,je malengo yalitimia?, Kama bado je tutaifishe tena?
My take ; tufanye utafiti, kuwa tulijikwaa wapi mfano mfumo,taratibu zipi zilitumika,je siasa ilitumika zaidi? nk.
 
Azimio la Arusha lilikuwa kila kitu lilizungumzia rasilimali zetu na maadili ya uongozi na hata watu wa magharibi waliolisoma waliliona kama mojawapo ya documentary bora kabisa ya kiuchumi pamoja na mpango wa irak chini ya sadam husein
Venezuela leo hii ni taifa kubwa kiuchumi Duniani na lina jeuri hata ya kubishana na mataifa ya magharibi lakini kikubwa alichofanya Hugo Chavez ni kulikopi azimio la Arusha na kulitekeleza kwa vitendo sisi tuna rasirimali je tumeshajiuliza kwanini Japan na Ujeruma hawana rasilimali yoyote lakini ndio wanaongoza kiuchumi Duniani,je ni mataifa mangapi yalioyofata masharti ya IMF leo hii yana uchumi mzuri matokeo yake tumekuwa tunatukanwa na akina Cameroon
iwapo tutakuwa na viongozi wazalendo tuna uwezo wa kuwa taifa kubwa kiuchumi duniani tuachane na propaganda za kuwa tukifanya tutazuiwa msaada angalia Cuba pamoja na vikwazo bado ni taifa linaloongoza kwa huduma za jamii Kenya walianza kuwa na bajeti inayojitegemea baada ya kuwekewa vikwazo wao hayo mashirika ya IMF na World bank yako kwa ajili ya kutukandamiza ndio maana wanataka wao ndio wawe wanatoa viongozi wa hayo mashirika angalia songas,bariki wanavyotunyonya
 
Mbona hata uko UK na USA mabenki yalikuwa na mengine hadi leo bado yako "natioalised" katia % fulani baada ya mdororo wa uchumi na kuonekana eti they were too big to fall. Yes pesa zawalipa kodi zikakomboa mabenki ya mebapari.

Kwa hiyo sio Bolivia na aregetina tu.
Nakubaliana na wewe mkuu kwa hiyo observation, lakini the "Free Trade gospel" according to the First WOrld ni dhambi kubwa kutaifisha mali za mabwana wakubwa hao.
Leo Zimbabwe inasakamwa kwa kuwekew vikwazo vya kuua uchumi wake kwa kosa la kurudisha mali yake.

Argentina na Bolivia wameonyesha njia kuwa matazamio ya wananchi wake ndiyo lazima yapewe kipau mbele na si matakwa ya makampuni ya nchi za dunia ya kwanza.
Nakubaliana na wewe kwa kunote kuwa wao wakitaifisha kwa manufaa ya wananchi wao(nchi za dunia ya kwanza) ni sawa, tukifanya sisi kwa manufaa ya wananchi wetu basi ni kosa na dhambi!
That is economical hypocrisy.
 
Mi naona ni viongozi wamekosa ubunifu wa kuinua chumi zao sasa ili kuendelea kupata support ya wananchi waliochoka wanadhani kutaifisha ndo jibu.
Ni kiwewe tu cha kukosa majibu ya uchumi. Dunia ya leo hata nchi kubwa zote zinajaribu kuvutia wawekezaji. Ukishafanya upuuzi kama huu unategemea nani atakuja kuwekeza? Na kama watakuja they will demand a very high return because of the higher risk, ndivo wawekezaji walivo na higher return to investor implies low return to the host.

Dunia ya sasa huwezi kuishi kivyako hasa nchi masikini(!!) kama hizi Bolivia na Argentina. Nchi ni lazima kujenga a stable and predictable policy badala ya kubabaisha na baadae unakimbilia kutaifisha then unaita tena wawekezaji.

IMF, WTO na other players kwenye Int'l businesses wanasema this is unacceptable and they will pay for there actions.
Ni habari nzuri kwa wapiga kura in short term but in the long run hizi policy they are economically futile.
 
Mkuu scenario unayijenga ni ile yamazingira endelevu kwa maanamya uwekezaji.
Nafikiri mtoa posti hapo juu hajasoma mazingira ya Argentina na Bolivia na sababu zilizopelekea kutaifishwa kwa makampuni y YPF na TDE ya Uhispania.

Sababu walizotoa ,serikali za Argentina na Bolivia, ni waekezaji hao kukosa KUWEKEZA, kwa maana ya kuingiza mitaji katika kampuni husika.
Kimsingi kampuni hizo zilikuwa sana sana zinafanya trading tu, na si kuwekeza.
Haya ndiyo mambo tunayoyaona hata Tanzania leo kwa makampuni mengu tuliyoyabinafsisha.

Pengine nakubaliana na wewe kuwa viongozi wetu wanakosa ubunifu katika kuendesha uchumi wetu, na wengine wanafikiri uwekezaji na wawekezaji lazima watoke Ulaya, Marekani au Uchina.

Watu kama Mengi kwa kiwango fulani lazima iwe benchmark ya muelekeo wa uwekezaji nchini.
Tuelewane kitu kimoja, kuna mawazo potofu kuwa capital inaweza toka nje ya nchi tu.
Mtaji na fedha iliyokusanywa na NICOL inaondoa mawazo hayo.

Kama tunataka kuendelea kiuchumi ni lazima tujiondoe katika ukoloni wa kujitakia katika mashirika kama WTO, IMF na hata WORLD BANK.
Kama mtu anafikiri naota basi anisaidie kuelezea jinsi wakubwa hao wanavyoweza kutukopesha kuanzisha viwanda mama vya kuzalisha chuma na vinginevyo ili tushindane kikamilifu na viwanda vya West.
Sana sana tutakopeshwa kulima just enough to be alive to serve the west na kubaki soko la bidhaa zao.
Watanzania tuamke kifikra.
 
Ereer! Mnataka kufanana na mabwana wakubwa eeh? tazama Zimbabwe ulete majibu ya kilicho wapata. Tetea maslahi ya walio wafundisha mnachojuwa kwanza ili mfanikiwe!
 
Nakubaliana na wewe mkuu kwa hiyo observation, lakini the "Free Trade gospel" according to the First WOrld ni dhambi kubwa kutaifisha mali za mabwana wakubwa hao.
Leo Zimbabwe inasakamwa kwa kuwekew vikwazo vya kuua uchumi wake kwa kosa la kurudisha mali yake.

Argentina na Bolivia wameonyesha njia kuwa matazamio ya wananchi wake ndiyo lazima yapewe kipau mbele na si matakwa ya makampuni ya nchi za dunia ya kwanza.
Nakubaliana na wewe kwa kunote kuwa wao wakitaifisha kwa manufaa ya wananchi wao(nchi za dunia ya kwanza) ni sawa, tukifanya sisi kwa manufaa ya wananchi wetu basi ni kosa na dhambi!
That is economical hypocrisy.

Ndio sasa TANESCO yetu imeuliwa .TaNESCO imekuwa cashier za kuwalipa likes IPTL na songas.Hapo wakubwa wanasema Yes hizo ndio reform za uchumi at the expense of Tanzanian . Tanescoitauja kukamuliwa hata na mtu (So called wawekezaji )just kwa kuleta Megawat za "vibaba" as if huo umemewa vibaba wa siju MGW 80 ,100 TANESCO wakiwezeshwa hawawezi.

Mkopo wowote wa kufufua na kuimarisha TANESSO utapata vikwazo lakini GOT ikiweka gurantee kwa IPTL ni rahisi kupewa green light ya mkopo.
 
Ndio sasa TANESCO yetu imeuliwa .TaNESCO imekuwa cashier za kuwalipa likes IPTL na songas.Hapo wakubwa wanasema Yes hizo ndio reform za uchumi at the expense of Tanzanian . Tanescoitauja kukamuliwa hata na mtu (So called wakezaji )ust kwa kuleta Megawat za "vibaba" asif huo umemewa vibaba wa siju MGW 80 100 wakiwezeshwa hawawezi

Mkopo wowote wa kufufua na kuimarisha TANESSO utapata vikwazo lakini GOT ikiweka gurantee kwa IPTL ni rahisi kupewa green light ya mkopo.
Kwa manufaa ya umma, ni wakati muafaka sasa kutaifisha IPTL na SONGAS ili wananchi wafaidi bei za chini katika bei ya nishati ya umeme.
 
Wanafalsafa walishasema public property is less productive!

Sasa mnataka kuturudisha zama za mashirika ya umma,ugawaji na vyama vya ushirika ambavyo viliwafanya wachache wawe mabilionea.Mashirika kama BIMA, SUKITA, NBC, General Tyre, Urafiki, Tanganyika Packers (imebaki scraper), UFI, Mwatex nk

Watu wachache waliyaua haya mashirika wakayaacha hoi. Angalia ATCL na TRL kila mwaka tunawa bail out wanamaliza hela ya walipa kodi.Imagine tuwe na mashirika 50 tegemezi si kodi yote itaenda huko tutashindwa hata kununua panadol!

bado sijaona njia kuu za uchumi nchi hii zinazoendeshwa (owned) na private sector ambazo zina- perfom efficiently

mimi nina machungu sana na walioua reli ya kati

.........kwa maana nyingine hivi sasa tuna uchumi bandia.............
 
Mkuu scenario unayijenga ni ile yamazingira endelevu kwa maanamya uwekezaji.
Nafikiri mtoa posti hapo juu hajasoma mazingira ya Argentina na Bolivia na sababu zilizopelekea kutaifishwa kwa makampuni y YPF na TDE ya Uhispania.

Sababu walizotoa ,serikali za Argentina na Bolivia, ni waekezaji hao kukosa KUWEKEZA, kwa maana ya kuingiza mitaji katika kampuni husika.
Kimsingi kampuni hizo zilikuwa sana sana zinafanya trading tu, na si kuwekeza.
Haya ndiyo mambo tunayoyaona hata Tanzania leo kwa makampuni mengu tuliyoyabinafsisha.

Pengine nakubaliana na wewe kuwa viongozi wetu wanakosa ubunifu katika kuendesha uchumi wetu, na wengine wanafikiri uwekezaji na wawekezaji lazima watoke Ulaya, Marekani au Uchina.

Watu kama Mengi kwa kiwango fulani lazima iwe benchmark ya muelekeo wa uwekezaji nchini.
Tuelewane kitu kimoja, kuna mawazo potofu kuwa capital inaweza toka nje ya nchi tu.
Mtaji na fedha iliyokusanywa na NICOL inaondoa mawazo hayo.

Kama tunataka kuendelea kiuchumi ni lazima tujiondoe katika ukoloni wa kujitakia katika mashirika kama WTO, IMF na hata WORLD BANK.
Kama mtu anafikiri naota basi anisaidie kuelezea jinsi wakubwa hao wanavyoweza kutukopesha kuanzisha viwanda mama vya kuzalisha chuma na vinginevyo ili tushindane kikamilifu na viwanda vya West.
Sana sana tutakopeshwa kulima just enough to be alive to serve the west na kubaki soko la bidhaa zao.
Watanzania tuamke kifikra.

Agreed.......Wale waliojiita wawekezaji halafu wakaishia kutofanya kile tulichotegemea kama Taifa....waturudishie mali zetu....

......Pia Tunataka Serikali itakayoamini na kuwawezesha wawekezaji na wajasiliamali wa ndani kama wewe Mkuu...........ingekuwa hivyo hata hao Wajapan waliopo nchini wangeondoka zao tu......kwani uwezo wa kujenga mambo makubwa tunao............
 
Vizuri sana, ni mawazo endelevu na yaletayo tija kwa taifa. Hatuna haja na kukaa na mijizi, eti kisa UN imesema! Ni upuuzi. Tuwe tayari kula tembele nyumbani, na kukataa kuhahidima samaki utumwani, hali twaenda shindia chunga.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mi swali langu ni je? ni mfumo upi rasmi tuliolalia? ambao hata mwanafunzi wa shule ya msingi autamke bayana? je sisi ni wajamaa? au sisi ni mabepari au sisi ni mixed economy? tusipate majibu baada ya uchambuzi wa wataalam wa uchumi bali tutamke bayana na kuwaaminisha wananchi na watoto wejue wazi kuwa hizi ni zama za the fitest, breviest, na kujuanest. wakiamini na kujipanga hata kama ni mfumo mbovu bado kwa kiasi kikubwa itatusaidia. Mawazo na fikra za watanzania ziko kijamaa na ndo maana kila mwananchi na viongozi humrefer Nyerere bila kukumbuka kuwa yeye alikuwa mjamaa na ndio ideology aliyoendeshea nchi na mpaka watoto waliitambua. Nchi hii ni purely capitalist na ndo maana hata ukimpa mtu uwaziri cha kwanza atawaza how to acqure capital, ndo majumba ya anasa unayoyasikia. Everybody is about capital including you. Tuwaambie wananchi baya zama za chetu haipo sasa ni kila mtu na chake, else tufanye maamuzi tubadilishe mfumo na wote tuujue. Huna clear ideology what next ni lzm uwe msanii.
Wananchi waambiwe mara ngapi. Sera ya chama kilichoko madarakani ni kujenga uchumi unaoendeshwa na sekta binafsi. Sera ya CCM ni kuondoa serikali au umma kumiliki njia kuu za uzalishaji. Na tumeona ikitekeleza sera hizi kwa kuuza mashirika na taasisi za uzalishaji kwa watu binafsi. Na kwasababu wananchi wameendelea kuchagua ccm ina maana wamependezwa na sera hizi za ccm.
 
Wanafalsafa walishasema public property is less productive!

Sasa mnataka kuturudisha zama za mashirika ya umma,ugawaji na vyama vya ushirika ambavyo viliwafanya wachache wawe mabilionea.Mashirika kama BIMA, SUKITA, NBC, General Tyre, Urafiki, Tanganyika Packers (imebaki scraper), UFI, Mwatex nk

Watu wachache waliyaua haya mashirika wakayaacha hoi. Angalia ATCL na TRL kila mwaka tunawa bail out wanamaliza hela ya walipa kodi.Imagine tuwe na mashirika 50 tegemezi si kodi yote itaenda huko tutashindwa hata kununua panadol!

Unasomeka mkuu, ila lazima tukubali kwamba pamoja na kua ubinafishaji ulikua haukwepeki sisi tuliufanya kwa haraka sana na bila kujiandaa. Yaani kila prescription ya hawa IMF, WB tuliifuata hadi nukta bila kujali athari zake za muda mrefu. Serikali ingewaomba wananchi kufunga mkanda na kubinafsisha taratibu huku tukitafuta washirika kwanza kwa yale mashirika na viwanda muhimu tukiwa na malengo ya kuja kuuzia hisa wazawa baadae..kwenye madini na nishati tungekopa ndani na nje kumiliki opearations za madini kama wenzetu Botswana na siyo kutegemea tu royalties za 3%.
 
Mkuu hizi ni mada ngumu kidogo kwa vijana wa kileo. At any rate sijui kama wengi wao wana kumbukumbu ya kupitia kwenye vitabu vyao vya historia ya uchumi wa Tanzania,hapa tumsubiri prof Lipumba kuelezea.
Hata hivo mimi naunga mkono urejeshaji wa mali ya umma,

Mi swali langu ni je? ni mfumo upi rasmi tuliolalia? ambao hata mwanafunzi wa shule ya msingi autamke bayana? je sisi ni wajamaa? au sisi ni mabepari au sisi ni mixed economy? tusipate majibu baada ya uchambuzi wa wataalam wa uchumi bali tutamke bayana na kuwaaminisha wananchi na watoto wejue wazi kuwa hizi ni zama za the fitest, breviest, na kujuanest. wakiamini na kujipanga hata kama ni mfumo mbovu bado kwa kiasi kikubwa itatusaidia. Mawazo na fikra za watanzania ziko kijamaa na ndo maana kila mwananchi na viongozi humrefer Nyerere bila kukumbuka kuwa yeye alikuwa mjamaa na ndio ideology aliyoendeshea nchi na mpaka watoto waliitambua. Nchi hii ni purely capitalist na ndo maana hata ukimpa mtu uwaziri cha kwanza atawaza how to acqure capital, ndo majumba ya anasa unayoyasikia. Everybody is about capital including you. Tuwaambie wananchi baya zama za chetu haipo sasa ni kila mtu na chake, else tufanye maamuzi tubadilishe mfumo na wote tuujue. Huna clear ideology what next ni lzm uwe msanii.

Unasomeka mkuu, ila lazima tukubali kwamba pamoja na kua ubinafishaji ulikua haukwepeki sisi tuliufanya kwa haraka sana na bila kujiandaa. Yaani kila prescription ya hawa IMF, WB tuliifuata hadi nukta bila kujali athari zake za muda mrefu. Serikali ingewaomba wananchi kufunga mkanda na kubinafsisha taratibu huku tukitafuta washirika kwanza kwa yale mashirika na viwanda muhimu tukiwa na malengo ya kuja kuuzia hisa wazawa baadae..kwenye madini na nishati tungekopa ndani na nje kumiliki opearations za madini kama wenzetu Botswana na siyo kutegemea tu royalties za 3%.

Hii mada imekaa vizuri sana , ni ya kisomi somi kidogo ndiyo maana toka mwanzo niliona mchango wa wasomi kama Prof Lipumba ni muhimi.
Mimi huwaga najiuliza,
Hivi katika Wizara au Idara ya Mipango na Uchumi wa nchi hivi vitu wataalamu wetu wa uchumi hawavioni?
Au wao ni kuhudhuria makongamano ya World Bank, IMF na mengine kuchichotea vi-alwansi tu.
Tena siku hizi kuna maprofesa na madokta wengi tu wa uchumi, wanafanya nini?

Hatuna ma Think Tank jamani? au vyeti ni vya kutandika ukutani na kutamba kwenye mabaa tu!
 
Hivi Mkuu Lole Gwakisa!

Naomba ufafanuzi kidogo, kuna stori nimekuwa naisikia eti kwenye historia ya uchumi wa taifa flani hivi, hiyo nchi ilifilisika kabisa hadi hazina yao iliishiwa kabisa na kubaki na vipande vichache sana vya dhahabu.
Nasikia mtawala wa nchi hiyo akaitisha mkutano mkuu wa wataalamu wazawa, wataalamu wote wa maeneo yote ya uchumi wa nchi, akawapa assignment kuwa wampe JIBU la dira ya nchi.
Nasikia hiyo nchi sasahivi ni inafanya vizuri sana na ni miongoni mwa nchi za "Ulimwengu wa kati"...!

Sasa naomba ufafanuzi kidogo, ni kwelli kuna hadithi ya namna ya namna hii??
Iwe kweli au isiwe kweli, je inawezekana kuwa na kitu cha kitaifa cha namna hiyo??
Mi nadhani kwa hali tuliyopo sasa tunahitaji muafaka wa namna hii...
 
Back
Top Bottom