Nationalisation is back: Utaifishaji kwa manufaa ya umma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nationalisation is back: Utaifishaji kwa manufaa ya umma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, May 2, 2012.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mwelekeo wa uchumi wa dunia sasa hivi ni kwa uchumi binafsi wa Nchi kujilinda katokana na ushindani wa nje.

  Katika matukio ambayo yanatikisa uwekezaji has a katika Nchi za Latin America, hususan Argentina na Bolivia, ni Nchi hizo kuchukua hatua mahsusi KUTAIFISHA sekta muhimu za uchumi katika Nchi zao kwa manufaa ya umma.

  Argentina imetaifisha kampuni ya uchimbaji mafuta,YPF ambayo ni kampuni ya uchimbaji wa mafuta na imetaifishwa mnamo April 16 mwaka huu.

  Kampuni ya YPF ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja na Nchi ya Spain.

  Jana, May, 1 ,2012, nayo Nchi ya Bolivia imetaifisha kampuni ya kufua umeme, TDE, ambayo vile vile ni ya kutoka Nchi ya Spain.

  Hili ni fundisho kubwa sana kwa Nchi zetu hizi, Kama Tanzania, ambazo ziko katika michakato ya "kuuza" njia kuu za uchumi kwa " kubinafsisha" viwanda na makampuni ya umma.

  Wengine wetu tulikuwepo miaka ya 60's wakati hatua hii ikifanyika, KUTAIFISHA njia kuu za uchumi.

  Leo tunashuhudia zoezi hili likijirudia kwa kuanzia Latin America.

  Kuishi kwingi, kuona mengi, and what goes around, comes around!!
  Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere must be turning in his grave today.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizi ni mada ngumu kidogo kwa vijana wa kileo. At any rate sijui kama wengi wao wana kumbukumbu ya kupitia kwenye vitabu vyao vya historia ya uchumi wa Tanzania,hapa tumsubiri prof Lipumba kuelezea.
  Hata hivo mimi naunga mkono urejeshaji wa mali ya umma,
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Well well well.....ngoja waje watu wanaojiita wenye mlengo wa kulia.............................
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  You mean mlengo wa kushoto,leftists.
  PUblic ownership is to the left.
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Oganigwe!! Mali za Riz1 nazo zitaifishwe hazina uhalali wowote zaidi ya uwizi tu
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nationalization kwenye baadhi ya sector ni muhimu na vile vile ni jambo zuri, lkn lazima liwe backed na uongozi imara. Lkn kwa uongozi wa aina ya JK ni ngumu sana kutekeleza hiyo dhana...
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  una uhakika kiasi gani kuwa utaifishaji utakuja huku pia?
   
 8. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mi swali langu ni je? ni mfumo upi rasmi tuliolalia? ambao hata mwanafunzi wa shule ya msingi autamke bayana? je sisi ni wajamaa? au sisi ni mabepari au sisi ni mixed economy? tusipate majibu baada ya uchambuzi wa wataalam wa uchumi bali tutamke bayana na kuwaaminisha wananchi na watoto wejue wazi kuwa hizi ni zama za the fitest, breviest, na kujuanest. wakiamini na kujipanga hata kama ni mfumo mbovu bado kwa kiasi kikubwa itatusaidia. Mawazo na fikra za watanzania ziko kijamaa na ndo maana kila mwananchi na viongozi humrefer Nyerere bila kukumbuka kuwa yeye alikuwa mjamaa na ndio ideology aliyoendeshea nchi na mpaka watoto waliitambua. Nchi hii ni purely capitalist na ndo maana hata ukimpa mtu uwaziri cha kwanza atawaza how to acqure capital, ndo majumba ya anasa unayoyasikia. Everybody is about capital including you. Tuwaambie wananchi baya zama za chetu haipo sasa ni kila mtu na chake, else tufanye maamuzi tubadilishe mfumo na wote tuujue. Huna clear ideology what next ni lzm uwe msanii.
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  bado sijaona njia kuu za uchumi nchi hii zinazoendeshwa (owned) na private sector ambazo zina- perfom efficiently
   
 10. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red pananigusa sana.
  unaweza kuwa na ideology lakini inakuwa ni bure kama wahusika wakuu hawana habari nayo (unaware).
  Hii nchi kama baadhi ya nchi za Kiafrika zilivyo wengi wetu tu 'vichwa maji' na ushahidi hapa ni pale Mwalimu alipoamua kutaifisha mali alafu akajaribu kuchelewesha rasilimali (natural resources) kufunguliwa kwa kila mtu ili aelimishe watu wake. Sote tunajua ni kiasi gani cha pesa kimekuwa invested kwenye vichwa vya baadhi yetu lakini kana kwamba hiyo haikutosha, walewale waliopata hiyo elimu ndio leo wanafanya tofauti na waliyoelekezwa kulinda kwa ajili ya vizazi!

  Taitizo linaweza kuwa ni kubwa zaidi ya kuwa au kutokuwa na ideology mkuu!

   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  nadhani bado sana, elimu kwanza jamanh. Just imagine in next five years gesi na mafuta ndio itakuwa kila kitu hata madini tutasahau. Je tumejiandaa vipi? Tunasomesha watu au tunasubiri expert waje?
   
 12. M

  Mkira JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Labda hii topic nayo inafaa hapa Maana UBINAFSISHAJI UNAZUNGUMZWA HAPA, WIZARA YA ARDHI IPO KWA MASLAHI YA NANI? WAGENI AU WATANZANIA? TUNAHITAJI NATIONALISATION TENA HII ITAWAHUSU VIONGOZI NA WATOTO WAO WOTE!!! kuwanyang'anya mali za taifa walizozipata kwa njia za mkato, pia kutaifisha migodi na mashamba mfano huko arumeru nk!!

  Ndugu wana JF baada ya kuisoma sheria ya ardhi ya 1999, 2001 ninakubaliana na issa shivji kaika ktabu chacke cha  "insha za mapambano ya mnyonge cha mwaka 2012"(ninawashauri mkinunue mkisome ni sh 15,000, nilimuona nacho Zitto pia!) kuwa sera ya ardhi tanzania imekuwa mbaya na imerithi mfumo wa wa sheria ya kikoloni ya mwaka 1923.


  mfumo huo ulimpatia gavana madaraka makubwa na haki ya kumiliki ardhi ili kuweza kuwanyang'anya wanachi ardhi yao kirahisi na kuiweka mikononi mwa mabepari ili wawekeze na kuitumia kama mtaji wa kuzalisha na kutunyonya.


  baada ya ukoloni, marekebisho ya hizi sheria za 2001 hayakufuata mapendekekezo ya tume ya shivji, bado ardhi haionekanai kama mtaji na pia haki ya kumiliki ardhi ya kimila haitambuliwi ila tu ile ya(maandishi) kimakaratasi ya kumilikishwa na wizara ya ardhi ndiyo inatambulika, ukimnyangánya mtu ardhi yake na ukaweza kupta miliki ya maandishi ukienda naye mahakamani utamshinda maana yeye miliki yake ya kimila haitatambulika!!!

  mfumo huu wa umilkaji ardhi ni mbaya na ni kama wa kikoloni bado ardhi inamilikiwa na rais(gavana).

  mfumo huo umeendelea kuifanya ardhi kutokuwa mtaji kwa wamilikaji wa kimila na vijijini na pia unatoa mwanya kwa wachache wakimemo wenye uwezo wa kati kama wengi humu jf kuweza kununua ardhi na kuifanyia ulimbikizaji kwa madhumni ya  (1) kucheza kamari(land speculation-hapa kuna kabila moja(watu fulani) la wajanja wenye nazo na elimu hunufaika sana hapa tz kwa kununua ardhi na kuizua wapo kila mkoa na hasa dar, tanga nk,!)

  (2) kukodisha -wenye uwezo hununua na kuikodisha kwa walio nyangánywa, mifano ipo!  (3) kuiuza kwa faida, wengi mnajua .
  (4) WENGINE WAWEKEZAJI HASA! HUTUMIA KAMA MTAJI WA KUWATUKIMISHA WATU katika ardhi na kuzalisha faida toka katika ardhi hiyo, eg madini nk?

  Hivyo basi wakati tunaenda kuandika katiba mpya suala la umilikaji wa ardhi uangaliwe kwa makini.

  Hivi ni matanzania gani ambaye hata kama amejenga nyumba yake nzuri popote hana uoga au wasiwasi kuwa siku rais au serkali wakitaka hiyo ardhi hatanyangánywa?  Huko vijijini linapotokea suala la upanuzi wa miji au wilaya mpya ni nani ambaye hana wasiwasi kuwa ardhi inayomilikiwa kimila na wazazi wetu haitachuliwa??


  Chadema angalieni suala la ardhi kwa umakini sana kabla na mtakapoingia ikulu baada ya 2015!! maana ccm wao ardhi imekuwa si mtaji wa watanzania na hata kufikia mahali pa kuwamilikisha wawekezaji katika migodi, mashamba miaka 99 au zaidi huku asilimia za umiliki wa hiyo migodo kuwa asilimia 100 kwa wageni eti sisi au serikali haina mtaji??? ccm wanataka mtaji gani zaidi ya ardhi tuliyopewa na mungu??


  Ninawaombeni mjadili suala au sheria ya ardhi bila kujali kuwa wewe unaweza kuinunua bali kuangalia walio wengi a hasa walioko vijijini.ikibidi mawazo haya yafikiriwe katika katiba mpya sina imani kama topic ya ardhi imejadiliwa kama ipo samahani.  Ninarudia wizara ya ardhi ipo kwa maslahi ya nani? wageni au watanzania?

  maana hata hizo hati kuzibata ni mbinde, mfano tangu 2010 nimeomba hati hadi leo sijapewa jibu toka wizarani??


  Wakati wa waziri magufuli alijitahidi kuahikikisha hati zilikuwa zinatoka mapema lakini baada ya kuongolewa mhhh!!!!  Ila ninarudi pale pale kuwa hata suala la hati linawanifaisha tu wenye nacho, sula la miliki za kimila nk liwepewe uzito kama ilivyopendekewza katika tume ya shivji katika omozi wa awamu ya pili.
  Lakini pia je ni kwa nini rais asitumie mamlaka aliyopewa na katiba hii kabla ya katiba mpya kuchukua kuichukua ardhi yetu toka kwa wawekezaji ili tuanze upya?? tutampata wapi rais mwenye ujasiri huo, vinginevyo tayari tu watumwa wa wakezaji na tuatendelea kuwa watumwa chini ya ardhi yetu ambayo tayari ccm wameigawa bureeeeeeeeeee kwa mika 99!!  Swali: ubinafsishaji na ugenishaji wa ardhi ya tanzania kwa wakezaji katika migodi na mashamba makubwa je ni ukombozi wa wanyonge au unyonge wa
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  mimi nina machungu sana na walioua reli ya kati
   
 14. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa wale watu makini,ni wazi kwamba privatization ni hila iliyoingizwa kiujanja na matapeli wa nchi za magharibi kuiba resources za nchi maskini. Wanafanya hivyo kwa kuwatumia kwa bahati mbaya wale tunaowaita viongozi ambao kwa kweli ni agents wao katika wizi huu.Hawa malipo yao yanapitishiwa kwenye mikopo au kile kinachoitwa misaada ya aina mbalimbali.So nationalization is plausible,and returning back what has been stolen from us.
   
 15. m

  mharakati JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  vijana nimependa mko makini kiitikadi.... Nafikiri serikali imebanwa sana na hawa WTO, IMF, WB..tukivunja hii mikataba ya sekta ya madini na kwingineko kutakua ni kukiuka masharti ya hawa mabwana ya kutaka serikali isiingilie kati uendeshaji wa moja kwa moja wa sekta za kiuchumi kwa kuimiza ubinafsishaji. Sasa na huu umaskini wetu sijui itakuaje..Argentina walikiuka haya maagizo kwa sababu hawategemei sana hivi vimisaada vya nje na wanafanya biashara nzuri na majirani zao ukiachia mbali wana soko kubwa la ndani kwa bidhaa zao za viwandani. wenzentu wanaweza huu uthubutu, sisi hatuwezi, tukimchungulia Mugabe pale, tunaogopa...
   
 16. m

  mharakati JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Ambacho huwa sielewi hii mikataba kwa nini iwe ni 3% au wapewe Tax holiday ya miaka 5-10 wakakti wakianza tu wanazalisha? kwani haya makampuni yalikua yenyewe peke yake yaani mi nikiwa na bidhaa si nangojea mwenye kuafikiana nae bei ili nimuuzie sasa kwa nini tulilazimisha hii mikataba ya sekta ya madini haraka haraka bila ya kujiandaa na wawekezaji hawakuepo kwa nini serikali isingekopa ndani au nje ili imiliki angalau hata 40% ya uzalishaji wa haya madini na mwekezaji apate hiyo 60% hii ingeleta maana kuliko huu upumbavu wa 3%. Ndiyo maana Nyerere alisema hatuchimbi kitu mpaka tuwe na uwezo

  Hawa akina Kigoda,(waziri mshirikishi kwenye uwekezaji) Mramba(waziri wa fedha kipindi cha huu wizi) Chenge (kama mshauri wa serikali kisheria ikiwemo sheria za kimataifa za uwekezaji nk), na Yona, (waziri wa fedha kipindi hiki cha wizi) hatutawasamehe kabisa na haya madudu ingali yakiwa yanaendelea kuitafuna nchi na kuwapa wageni faida zote na watz kuachwa na uharibifu tu wa mazingira.
   
 17. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Nationalization ipo na itaendelea kuwepo kwa mataifa yenye sera bora za ulinzi wa jamii na mali zake.
  Utaifishaji kwa manufaa ya uma ni sehemu ya ulinzi wa jamii na inatakiwa kutumika pale tu, nguvu ya mafisadi, wezi na wanyonyaji wanaomiliki njia kuu za uchumi wa taifa zinapozidi uwezo wa regulatory authorities za kitaifa.
  Pamoja na sheria kuhusu ubinafsishaji kuandikwa kwenye makaratasi, watendaji wa serikali hawana budi kuwa na sheria za asili zilizoandikwa kwenye bongo zao zikianisha wazi kuwa lazima tuwabane wageni wanaotumia rasilimali zetu kwa njia zozote zile kuhakikisha faida inabaki kwetu.
  Tunatakiwa kujua kuwa tunao wasomi wa kutosha kuanza kuiga na kuendeleza teknolojia ya uzalishaji na matumizi sahihi ya rasilimali zetu, ila tulichokosa ni watu wa kuunganisha watu hao kwa faida ya jumla ya taifa.
  Wapo wageni wengi wanaofanya mambo madogo madogo ambayo yanawapatia faida kubwa na wanatorosha utajiri wetu mwingi kupeleka kwao, huku viongozi wetu wakienda kutembeza bakuli la kuombaomba huko kwao.
  Idara za na ulinzi usalama ziamke na zijue wazi kwamba ulinzi na usalama wa jamii ni pamoja na kufanya tafiti za kijasusi na kutekeleza matokeo ya tafiti hizo juu ya namna ya kuwatumia wageni kwa faida na kuwatokomeza wale ambao hawana faida kwetu, na siyo kushirikiana na wezi kutuibia na kwenda kuficha kwao.
  Kuna haja ya kuanzisha effective social intelligence network juu ya hili na faida yake itaonekana kwa watoto na wajukuu zetu, badala ya kuacha hali ilivyo sasa ambavyo tutawaacha watoto na wajukuu zetu wakiwa watumwa katika nchi yao.
  Usalama wa taifa sasa uwe extended zaidi kwa kuwapa contract waajiriwa wengi wa makampuni ya kigeni badala ya hali ilivyo sasa ya kufuatilia mambo ya siasa na ulinzi wa viongozi wa kisiasa ambao hata hivyo hawana tishio sana la kiusalama zaidi ya malumbano ya kawaida baina yao.
  Ni muhimu na ni lazima kila mwananchi afundishwe na aelewe sawa sawa kabisa kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa jamii na mali zake ni la kila mmoja kwa nafasi yake na kwamba wenzetu wanaotuangusha lazima tuwawajibishe tu kama njia ya kujiimarisha kwa faida ya jamii kwa ujumla.
   
 18. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu nimekuelewa lakini ni lazima kuchambua sana hii issue ili kutenganisha pumba na makapi.
  Nilimpenda sana Nyerere kwa kuwa alikuwa clear thinker hata kama alifanya makosa makubwa kayika utekelezaji wake katika kuuweka uchumi chini ya himaya ya watanzania.

  Lazima tujielekeze katika kujikita kumiliki njia kuu za uchumi na faida zake kwa jamii ya kitanzania.

  Free economy haina maana ya free for all ownership.
  Hata ukienda nchi zilizoendelea kama wewe unapesa nyingi za kuwekeza , basi unashauriwa kuwa kuna mafao ambayo hutaweza kuyafaidi hadi umekuwa raia wa nchi hiyo-na wengi wanalowea huko, hasa Marekani na hata UK.

  Nimeipenda hii ya Argentina na Bolivia kwa kuonyesha utaifa wao na kwamba wao ndio MASTERS wa nchi zao na si mwingine.
  Katika Argentina , mbia kutoka Spain hakuwa anawekeza katika shirika la kuchimba mafuta,YPF , yeye alikuwa nanayonya tu na kuuza.
  Hali kadhalika huko Bolivia,mbia kutoka Spain hakuwa anawekeza katika shirika la kufua umeme, TDE, bali alikuwa anafanya biashara.
  Katika mifano yote wenye mali wamerejesha mashirika yao kwa serikali ili ifanye vizuri zaidi.
  Na hii ni baada ya kugundua kuwa waSpanish hao walikuwa wanaganga njaa tu na kutatua matatizo yao binafsi kutoka nchi zao na kuhamishia nchi hizo.

  Kwetu Tanzania inabidi tufanye mapinduzi ya kifikra ili tuweze kuenda na wakati.
  Tumeuza mashirika kama ifuatavyo BORA SHOES, MUFINDI PAPER MILLS,UBUNGO GARMENTS,SUNGURATEX,mashamba ya Katani, mashamba ya mpunga na mengine zaidi ya 400.
  Tulikuwa na imani kuwa "mjomba" wa kutoka nje atayaokoa mashirika hayo, leo yametoweka kabisa au walioyanunua wanfanya biashara tofauti kabisa na core business ya mashirika waliyoyanunua.

  Mbaya zaidi mashirika haya leo yamejikita katika kununua na kuuza bidhaa toka nje ya nchi, hasa China, kwa kuweka rehani mali ya Watanzania waliyoinunua!

  Lawama haisaidii, hatua ya kuchukua ni kuyarudisha kwa wenyewe, wananchi!
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Na hili ndio tatizo kubwa sana la viongozi wetu.
  Wanafikiri mtu wa nje , hasa akiwa mzungu, ana majibu sahihi ya matatizo yetu, no original thinking toka kwa viongozi wengi sana.
  Siasa ya kujitegemea , in practice kwa wengi ni ndoto tu ambazo wamafikiri haziwezekani bila hata kuthubutu kujaribu!!!
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanafalsafa walishasema public property is less productive!

  Sasa mnataka kuturudisha zama za mashirika ya umma,ugawaji na vyama vya ushirika ambavyo viliwafanya wachache wawe mabilionea.Mashirika kama BIMA, SUKITA, NBC, General Tyre, Urafiki, Tanganyika Packers (imebaki scraper), UFI, Mwatex nk

  Watu wachache waliyaua haya mashirika wakayaacha hoi. Angalia ATCL na TRL kila mwaka tunawa bail out wanamaliza hela ya walipa kodi.Imagine tuwe na mashirika 50 tegemezi si kodi yote itaenda huko tutashindwa hata kununua panadol!
   
Loading...