Natarajia kuvuna samaki sato natafuta mteja/wateja Mwanza

Natarajia kuvuna samaki sato natafuta mteja/wateja Mwanza

Hongera sana mkuu. Ningekuwa mimi hapo napiga hesabu za kumpandisha cheo huyu mke wangu.
 
Ndio,kifupi samaki wote asilimia 99 mnaokula aina ya sato ni wakufugwa,hakuna samaki sato wa ziwani anaevuliwa kwa wavu au ndoano utamvua kwa uzito wa zaidi ya tani.
Huu ni uongo wa Hali ya juu sana humu Musoma tunakula Sato OG kuanzia musoma Mjini mpaka vijijini ni Sato n Sangala OG
 
Habari za muda muda wadau bila shaka mnaendelea kufuatilia wagombea waliopita.Nisiwachoshe nipo jijini Mwanza najihusisha na ufugaji wa samaki aina ya Sato ziwa victoria, natarajia kuvuna makadirio ya chini Tani 2.5(2500kg+).

Hii ni kati ya wiki moja ijayo,hivyo naomba yoyote mwenye uhitaji wa kununua kwa bei ya jumla tuwasiliane.
Bei ni tsh.8500/kg.Samaki wanauzito kati ya gram 250 hadi 500gram/nusu.Samaki walio chini ya uzito huo bei ni negotiable(kwa kawaida samaki wenye uzito chini ya 200gm huwa hawakosi),Napatikana Malimbe kabla ya luchelele.

Ahsanteni na karibuni.

View attachment 3431510
Nakupongeza sana kwa juhudi hiyo ya ufugaji wa Samaki, ni moja wa mradi nao fikiria kuufanya ktk ufugaji wangu.
 
Sato watamu sana , juzi nikiwa mwanza mitaa ya lumumba nilipata supu ya kipande kwa elfu 6 . Nilishiba had jioni
 
Eti wanasema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza!
Kwahiyo biashara za mtandaoni ni mbaya ndio maana zinatangazwa,alibaba,amazon,kikuu n.k hizo bidhaa zinazotangazwa huko ni mbaya!??watanzania tunasafari ndefu sana,tunafanya biashara kwa kukariri.nikupe taarifa tu nimeuza tani 1.8 kupitia hapa,wewe endelea kukariri badala ya kujifunza,ukitaka slip za bank njoo inbox nikuoneshe ushahidi watu wenyewe akili timamu wanavyofanya biashara siku hizi.
 
Back
Top Bottom