Natangaza rasmi kuendelea kupambana na Lowassa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2020

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Hajakipata bahati mbaya yes,ila amekipata kwa sababu ya CHUKI ya Nape,JK na wewe mwenyewe.Usichukie mtu chukia tabia ya mtu ili usihukumu maana usije ukahukumiwa.

Tumeona namna ambavyo utawala wa JK ulivyoumbuliwa na aliyekuwa waziri wake JPM,kama ningekuwa kwenye viatu vya JK hata kufika IKULU nisingefika,maana kwa matendo na ouvu wake ndipo alipotufikisha.

Sasa kama unapambana na MAFISADI mbona JK na rafikize plus familia yake hujawagusa?Au hawa hawagusiki??Nidyo sababu CHUKI mliyojengewa na JK sababu anamchukia LOWASSA mnaiendeleza.Piga vita UFISADI na si kumchukia mtu
Simchukii Lowasa kwa sababu tu ya jina lake ama kwa sababu anatoka Kaskazini. Namchukia kutokana na ufisadi wake
 
Mzee Mchopu

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
1,033
1,250
Kwakua lowassa ndiye meremeta

Tangold
Sukari
Uda
Meremeta
Dowans IPTL
TANESCO
ESCROW. pambana nae
 
ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,058
2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika ambapo CCM imeibuka mshindi kwa ujumla wake katika nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa. Hata hivyo, mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020.

Tumewasikia baadhi ya walioshindwa wakiongozwa na Fisadi Edward Lowasa wakijigamba kuwa mapambano yanaendelea na kwamba mwaka 2020 watasimama tena kuomba ridhaa ya Watanzania. Mwaka 2020 si mbali katika maisha ya binadamu ila ni mbali kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Waliotangaza mapema kugombea nafasi hiyo hawana hakika ya nini kitatokea mbele ya safari ila kwa vile kila binadamu anaishi kwa mipango, nawapongeza wote waliotangaza kugombea uchaguzi wa 2020. Pia kitendo cha Lowasa kutangaza mapema kuwa atagombea uchaguzi wa 2020 kinatupa fundisho kuwa kumbe CHADEMA kinaendeshwa na matakwa ya mtu mmoja.

Binafsi nilianza mapambano na mafisadi mwaka 2012. Tangu wakati huo, nikiri kwamba licha ya mapambano kuwa magumu, nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa nikishirikiana na wadau wengine angalau kuwasema wazi wazi mafisadi na kuumbua mipango yao ovu. Hali hiyo ilisaidia wananchi kuamka na kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura na hivyo kufanikisha kuwaweka kando mafisadi wakiongozwa na fisadi Mkuu, Edward Lowasa. Kabla ya hapo, ilikuwa ni haramu kwa watu kumsema vibaya fisadi Lowasa na kila aliyethubutu kufanya hivyo basi alijikuta akiingia matatani.

Kwa vile fisadi Lowasa ametangaza kugombea Urais 2020, nami natangaza rasmi kuendelea kupambana na fisadi Lowasa hadi hapo fisadi mkuu atakapoteketezwa kabisa. Mapambano yanaendeleaUsikimbie kivuli chako,katika hili yatupasa twende taratibu.Hupaswi kujiapisha jf kwamba utapambana na Mh.Lowassa,njia pekee ya kuukomesha wimbo huu wa ufisadi uliodumu kwa miaka 9 sasa ni kwa wenye mamlaka kumkamata Mh.Lowassa na kumfikisha mahakamani.

Kuendelea kupiga kelele mitandaoni bila ya kuchukua hatua,ni uthibitisho kuwa Ufisadi wa Lowassa ni propaganda za kisiasa zinazopigwa na wale wenye hofu ya mambo waliyomtendea.

Mkishindwa kumchukulia hatua ndani ya miaka 5,hamtakuwa na sababu tena ya kuendelea na pambio yenu katika kampeni zijazo.Ni dhahiri jamii itamuona hana hatia na hakutakuwa na cha kumzuia kuingia magogoni.

Mdomo mlioutumia kumchafua Mh.Lowassa- StarTv,hautakuwa na ujasiri wa kupanua kinywa chake chenye uvundo kumshambulia mtu ambaye wenye mamlaka watakuwa wameshindwa kumuwajibisha.

Tuwe wakweli,ni wapumbavu wa aina yako tu wanaoishi kwa kujibanza kwenye kwapa za mabwana zao,huku wakiwafunga kamba za viatu na kuwapepea kwa vitambaa ndiyo wanaoweza kujitoa ufahamu na kuidanganya jamii kuwa mkwamo wa Taifa hili umeletwa na Mh.Lowassa.

Usifikiri sote ni wapumbavu wa aina yako tulioshikiwa akili.Unapowakatia viuno mabwana zako ili upate vyeo,usisahau kuwauliza ni kwa nini walipokuwa Ikulu badala ya kuwatumikia wanyonge wa Taifa hili,waliamua kuwa wajasiliamali kwa kufungua miladi ndani ya Ikulu?

Waulize miaka nane baada ya Mh.Lowassa kuwa nje ya Serikali,ilikuwaje makontena kwa maelfu yapite bandalini bira ya kulipiwa kodi?Wako wapi wanaoyamiliki?Iweje leo yabumbuluke madudu ya aibu?Kama Lowassa ni fisadi aliyelifikisha Taifa hili kwenye mkwamo wa Kiuchumi,Magufuli alilisi Uongozi toka kwa Lowassa?

Ni bora uwe mkweli kuliko kujitia upofu kwa ajili ya vyeo,Usifikili hao unaowakatia viuno wanaishi Sayari nyingine,tupo nao duniani,tunajuwa utajili wao na vyote wanavyomiliki kama matokeo ya kuliibia Taifa.Tunajuwa wafalme na wana wa wafalme wanavyomiliki na wayafanyayo.

Hata hao unaowasujudia Leo,njia zao zipo wazi.Kabla ya kufikishwa hapo walipo,Mapito yao yanafahamika,ufisadi wao upo dhahiri.

Ni aibu kuwa na mtu aliyetunukiwa vyeo eti tu alimudu kuwa mtumishi mwaminifu wa mwana wa mfalme,aibu sana.
 
Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,093
2,000
Pambana kwakweli alichokufanyia sio kitu kizuri kabisa, harafu wachangiaji wengine nashangaa mnaingilia ugonvi mnajua anapambania nini? Kafanywa vibaya mwenzenu
 
mgombea uvccm2017

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
507
500
Wadau, amani iwe kwenu.

Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika ambapo CCM imeibuka mshindi kwa ujumla wake katika nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa. Hata hivyo, mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020.

Tumewasikia baadhi ya walioshindwa wakiongozwa na Fisadi Edward Lowasa wakijigamba kuwa mapambano yanaendelea na kwamba mwaka 2020 watasimama tena kuomba ridhaa ya Watanzania. Mwaka 2020 si mbali katika maisha ya binadamu ila ni mbali kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Waliotangaza mapema kugombea nafasi hiyo hawana hakika ya nini kitatokea mbele ya safari ila kwa vile kila binadamu anaishi kwa mipango, nawapongeza wote waliotangaza kugombea uchaguzi wa 2020. Pia kitendo cha Lowasa kutangaza mapema kuwa atagombea uchaguzi wa 2020 kinatupa fundisho kuwa kumbe CHADEMA kinaendeshwa na matakwa ya mtu mmoja.

Binafsi nilianza mapambano na mafisadi mwaka 2012. Tangu wakati huo, nikiri kwamba licha ya mapambano kuwa magumu, nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa nikishirikiana na wadau wengine angalau kuwasema wazi wazi mafisadi na kuumbua mipango yao ovu. Hali hiyo ilisaidia wananchi kuamka na kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura na hivyo kufanikisha kuwaweka kando mafisadi wakiongozwa na fisadi Mkuu, Edward Lowasa. Kabla ya hapo, ilikuwa ni haramu kwa watu kumsema vibaya fisadi Lowasa na kila aliyethubutu kufanya hivyo basi alijikuta akiingia matatani.

Kwa vile fisadi Lowasa ametangaza kugombea Urais 2020, nami natangaza rasmi kuendelea kupambana na fisadi Lowasa hadi hapo fisadi mkuu atakapoteketezwa kabisa. Mapambano yanaendelea
Na mimi natangaza vita na wewe! 2017 nikishika UVCCM lazima uondoke Lumumba kuombaomba
 
Zeyn

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
345
250
Waliojaa ndani ya CCM hupambani nao?
Itakua haina maana sasa.itaonesha kama una chuki tu na mtu na sio kukemea ufisadi
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Simchukii Lowasa kwa sababu tu ya jina lake ama kwa sababu anatoka Kaskazini. Namchukia kutokana na ufisadi wake

Hutakiwi Kumchia mtu wala kumuhukumu maana hukumu mwachie aliyemuumba.Nimelkwambia chukia tabia yake.Leo tumeyajua madhambi ya aliyekuwa MUKULU wetu lakini hatumuhukumu tunasema atakayemuhukumu ni aliyemuumba.Kama ungetenda haki hata hawa ungewachukia na kusema kwa nguvu zote kwamba unachukia ufisadi:

JK ,Ritz,Chenge,Mama wa pesa ya Mboga aka Anna Tibaijuka,Ngereja,Mzee wa Tembo,aliyekuwa waziri wa Chui na simba,nk nk ningekuona wa maana sana.

LAkini kumnanga mtu mmoja haisaidii kuonyesha chuki binafsi.Jitahidi usiwe kama vuvuzela.Kama umeamua kupiga vita UFISADI na RUSHWA basi vaa miwani ya mbao piga kote kote.Fisadi siyo Lowassa tu.Kuna waliokwapua kuliko Lowassa na unawajua.
 
Ufisadi wa Liwasa ulikuwa na athari kubwa katika taifa. Ndo maana nimeamua kupambana na hilo fisadi papa. Kwa hilo tusameheane. Sitarudi nyuma
 
Bova

Senior Member
Jul 29, 2015
120
195
Waaapiiii... Nape si alipata kusema walinukuliwa vibaya??

Ama mimi ndo nilimnukuu vibaya Nape?
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Waliojaa ndani ya CCM hupambani nao?
Itakua haina maana sasa.itaonesha kama una chuki tu na mtu na sio kukemea ufisadi
Ni ukweli ambao hawapendi kuusikia wala kuusikiliza
Ufisadi wa Liwasa ulikuwa na athari kubwa katika taifa. Ndo maana nimeamua kupambana na hilo fisadi papa. Kwa hilo tusameheane. Sitarudi nyuma

Hakuna hicho kitu.Kama kwa miezi mitatu tumeweza kuona upotevu wa matrilioni ya shilingi kwa miaka mitano iliyokwisha tumepoteza kiasi gani?Je watanzania wangapi wamekufa mahospitalini?Je si RAIS wetu mpendwa alituambia kwamba hakuna pesa ya kulipa MADAKTARI wala kununua vifaa vya hospitali wakati wachache wakijineemesha kwa pesa za walipa kodi?

Ndugu yangu hakuna UFISADI ulioyumbisha TAIFA kama alioufanya RAIS wetu mpendwa kwa kuachia wachache wkisepa na matrioni ya MAKONTEINA na safafri zisizo na TIJA.

Jitahidi kuita koleo kolea na si kijiko kikubwa.DHambi ni dhambi hakuna dhambio ndogo wala kubwa.

Wakatai Polisi wakihaha na wapinzani na vibaka huku wakilinda watawala mafisadi,wala rushwa,majangili leo unamsimanga mtu mmoja.

In short nasema ni CHUKI mlizoambiwa mfanye na JK sababu walikosana wao nanyie mnafanywa kama ni walewale.Badilika piga kotekote.Vinginevyo nyamaza kimya kama hauoni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom