Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Uchaguzi Mkuu wa 2015 umemalizika ambapo CCM imeibuka mshindi kwa ujumla wake katika nafasi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa. Hata hivyo, mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020.
Tumewasikia baadhi ya walioshindwa wakiongozwa na Fisadi Edward Lowasa wakijigamba kuwa mapambano yanaendelea na kwamba mwaka 2020 watasimama tena kuomba ridhaa ya Watanzania. Mwaka 2020 si mbali katika maisha ya binadamu ila ni mbali kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Waliotangaza mapema kugombea nafasi hiyo hawana hakika ya nini kitatokea mbele ya safari ila kwa vile kila binadamu anaishi kwa mipango, nawapongeza wote waliotangaza kugombea uchaguzi wa 2020. Pia kitendo cha Lowasa kutangaza mapema kuwa atagombea uchaguzi wa 2020 kinatupa fundisho kuwa kumbe CHADEMA kinaendeshwa na matakwa ya mtu mmoja.
Binafsi nilianza mapambano na mafisadi mwaka 2012. Tangu wakati huo, nikiri kwamba licha ya mapambano kuwa magumu, nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa nikishirikiana na wadau wengine angalau kuwasema wazi wazi mafisadi na kuumbua mipango yao ovu. Hali hiyo ilisaidia wananchi kuamka na kufanya maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura na hivyo kufanikisha kuwaweka kando mafisadi wakiongozwa na fisadi Mkuu, Edward Lowasa. Kabla ya hapo, ilikuwa ni haramu kwa watu kumsema vibaya fisadi Lowasa na kila aliyethubutu kufanya hivyo basi alijikuta akiingia matatani.
Kwa vile fisadi Lowasa ametangaza kugombea Urais 2020, nami natangaza rasmi kuendelea kupambana na fisadi Lowasa hadi hapo fisadi mkuu atakapoteketezwa kabisa. Mapambano yanaendelea