Natangaza 'kumdharau' January Makamba rasmi!


Mwe mwe mwe mwe mwe.
Makamba kumbe mafia eh?
Hadi kumtishia binti wa watu maisha?doh na halima maskini akanyweeeea
inaonekana ana mjua sana.
 
Sijui niseme SNITCH lakin nisihukumu mapema mnoo!! Anaweza toa maamuzi magumu huwezi Kujua. Hata Zitto alilaumiwa sana na wanajamvi pia kuna kipindi lakin mnazidi kuona misimamo yake na hoja zilizoenda shule. Tumpeni nafasi anaweza akambana mzee wa kaya kooni mkageuka tena wote loh.
 
ama mnakumbuka vizuri, J. Makamba alikutana na Mwanamama wa Kimarekani mtoto wa Rockfeller .... ambaye alihoji jinsi misaada inavyoliwa na Majoka makuu ya JK, akidai Tanzania as the land of corrupt yaan FISADISTAN kwa ujinga wetu tumewapa tunaodai ni wawekezaji, wakala kamaviwavi jeshi wakashiba, wakaingia ubia wakala bia na kula kona.
Sukali mbeya aliiacha mia 600 sasa 2300, mkate 400 sasa 1200
 
Tatizo letu Watanzania tunaridhika kirahisi.

Mimi nilishasema zamani tu kwamba katika vitabu vyangu January Makamba na Mizengo Pinda si wabunge, na kwa hivyo sizitambui nafasi zao nyingine zozote zinazotokana na ubunge.

Hii ni kwa sababu hawakuchaguliwa kwa kura hata moja ya wananchi, na wala hawakuainishwa kwa namna yoyote katika katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kama kuna mtu anaweza kuniambia Makamba na Pinda ni wabunge wa aina gani kama ilivyoainishwa kikatiba naomba anielimishe hapa.

Kudharau katiba ndiko kunatupa matatizo haya ya uongozi dhaifu.
 
Reaction ya J.Makamba imemshushia hadhi kubwa na tumshukuru Mungu amemuweka wazi kuwa ni mtu wa namna gani' Mungu ni kweli hamfichi mnafiki humuumbua mchana kweupe. January alikuwa anapima kina cha maji ili aone kama ana influence au hana i.e impact ya with and without JM. Hata bila backing yake wabunge 73 wameshasaini yeye ameumbuka na tumemgundua siyo mwenzetu ni kizazi cha kifisadi hicho. We shall never ever trust this ufisadi offspring!!! AMEJIMALIZA RASMI!!!
 
mkuu ulitegemea makamba aseme nini hali ya kuwa hicho chama dicho kilicho lea wazee wake hadi kupatikana yeye?
 
Januari hana uzalendo, MCHUMIA TUMBO tu
Wazalendo wa kweli tutawaona kwenye hizi harakati za kuikomboa nchi yetu
 
Mbegu ya mhogo mchungu ukiipanda usitegemee kupata mhogo mtamu. Bora kuhangaika kupata mbegu ya mhogo mtamu itakayokuzalia mihogo mitamu. Vinginevyo ukitegemgea mhogo mchungu kuzaa mhogo mtamu utaishia maumivu ya kichwa kutokana na sumu yake.
Kumbe unasema huyu hafai maana ni product ileile ya maghambas?????Kwa hiyo CDM jipangeni kupeleka mtu bora Bumbuli tumvue huo ubunge wa CCM!!!!! Hakuna mwana harakati huko Bumbuli?????? Jitokeze au mnamwogopa huyo dogo??????????VIVA CDM VIVA UKOMBOZI WA BUMBULI!!!!!

 
Hujamjua? anabadili maneno yake kwa kujua kuna mabadiliko ya baraza la mawaziri na hizo mbwembwe ni katika kumfurahisha bwana mkubwa ili asimsahau ktk ufalme wake.
 
hii ni kawaida kwa siasa za afrika...
unafiki,chuki na kejeli zimetawala ktk demokrasi ya Tz
Mkuu Maziku Masunga Jr (one post) je umekuja hapa na agenda ya kutetea huo uozo kuwa ni halali????? Kwa kuwa hali hiyo imetawala Africa hivyo tukubali kuwa dharau, unafiki, chuki na kejeli ni haki ya MAKAMBA TUVUMILIE????? Hueleweki!!!!

 
Alisifiwa akajiona mtu wa maana hata hivyo sijawahi kuwaamini ccm hata sekunde achilia mbali ahadi zao hata familia zao na koo zao

Ndani ya CCM hakuna mwenye unafuu. Wote wameathirika tu. Virusi vya ufisadi vimewakamata vibaya sana. Kitendo cha wabunge wao (kuondoa wawili waliosaini) kupiga kelele kubwa na kuingia mitini kutoiwajibisha seriukali, ni uhaini wa hali ya juu. Ni wauaji wakubwa wa wananchi. Lkn wakati unawadia watajuta. Januari Makamba has no exception. Wala Mh Halima hapaswi kumpooza. Ukweli ni ukweli tu. Mi naona aliona Zitto anapanda chati akaona wivu ndo kisa cha kuomba mwongozo wa Spika. Alitaka sifa aendelee kupata yeye tu. Ni mnafiki mkubwa tu. Huwezi kuomba mwongozo wa kukwamisha jambo linaloleta ukombozi wa nchi. Utaifa kwanza, uswahiba na ukereketwa baadae. Nchi hii ikineemeka hata yeye ataishi kwa raha maana hata tegemezi kwake watapungua sana. Ni mnafiki hasa.
 
Hapo kwa Januari hakuna mtu. Hata hao wananchi wa Bumbuli sijui walitumia kigezo gani kumchagua. Huyo ni Mnafiki mkubwa anatafuta umaarufu tu hana lolote. Walichangia kumchafua Dr Salim ili mshikaji wao aingie Ikulu na kutuletea serikali ya Kishkaji.

JK anamchango mkubwa sana katika kumuharibu Januari maana waliona Ikulu kama ni ya familia yao.


For your information Msitu umeshika moto manyani yote yanatawanyika. Mpaka kieleweke.
 
Speaker, read between the lines. J.Makamba is so strategic tofauti na unavyomfikiria. In short huyu jamaa yuko behind the move (anaifurahia). Kwa taarifa yako anatamani hao mawaziri wapigwe chini ili apewe chaka. Aliona akishabikia waziwazi move ya Zitto watu wata doubt! Huyu jamaa ndani ya moyo wake kuna vi mikono vinashangilia!!!
 
Binafsi simfaham January, ila kupitia hiki japo kagusa hisia za wengi ila sioni tatizo. Haimaanishi ni lazma afuatane na upepo wa kila aina hata kama anaona sio sahihi bas afuate mkumbo. Nampongeza kwa kusimamia anachokiamini kuliko ambovo angekosa msimamo.
Kutofautiana mawazo kwa hoja ni ishara ya ukomavu, co uchawi, wizi, mtoto wa nyoka nk...ana mabaya yake ila na ss tuwe wakomavu, co lazma tukubaliane katika jambo....
 
Nakuunga mkono kwa hilo, mimi sijawahi kumuona January Makamba kama kiongozi makini bali ni mnafiki, aliyejaa tamaa ya madaraka, mbinafsi, mchoyo, mpenda sifa na mambo mengine mengi mabaya. Kuweni makini sana na kijana huyo kila afanyalo ana lengo lake binafsi sana sana kujijenga kisiasa, kutaka ummarufu na kutaka kuwaangamiza wenzake ili ikibidi yeye ndio achukue nafasi zao.

Harakati zake siziungi mkono, nafahamu fika ni zao za mafisadi wakuu wa nchi hii na mwanasesere wao wanayemtumia na kumuendesha kwa rimoti.
 


Nimeishiwa kauli
 
mara nyingi humu watu bila kuelewa au ufinyu wa uelewa kuhusu j makamba huwa wanamtetea na kumwita mzalendo kwa machache anayoongea au kufanya..lakini mi najua kila afanyalo sio kwa manufaa ya taifa..ni kwa ajili yake..iko hivi,kwanza jan anatam bulika kama mfuasi mtiifu kwa el na ra..alikusanya mill 300 kushinikiza wajumbe wampitishe kura za maoni agombee ubunge na kumchinja shellukindo(ant ufisadi)..lengo moja kupunguza nguvu ya wapambanaji dhidi ya ufisadi na pili ilikuwa uwaziri hasa nishati na madini na hana amani na ubunge kabisa sababu si levo yake (aonavyo) na kwa kuwa alifanya kazi karibu na kikwete ikulu,alihisi si rahisi kukosa uwaziri..hata email ya mwamy ilimwanika..ukaribu wa mzee wake na kikwete ilikuwa pia kete yake..aliamini angetajirika sana kama william mganga kupitia hasa sekta ya madini na gas..baada ya kuona hamna dalili alihamishia hasira kwa ngeleja(wanajuana)..ndio maana nasema huwa ana react kwenye masuala yenye interest zake..endeleeni kumfatilia mtajua zaidi..
 
Yaani Chura azae samaki!?
Kwanza uwezo ni mdogo. Kumbuka hotuba za Rais zilizowahi kulalamikiwa ndani ya JF.

Pia kumbuka e-mail iliyozungushwa ndani hapa ikionyesha hata utupu wa dada ulitumika kumunadi! AIBU TUPU!
 
Wakuu hakuna haja kuendelea kumtaja humu jamvini mwana hizaya huyu na msaliti mkubwa wa wapiga kura wa BUMBULI,na watanzania kiujumla.
 
Elimu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ,ndugu January ina utata..
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo hiyo ,mama Diana Chilolo ni DARASA la SABA,halafu anadai ni KIDATO cha SITA!
Hii nchi imeishiwa wasomi?Mwisho wenu hauko mbali.
Samahani kama nimetoka nje ya mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…