Sichukii kutofautiana mawazo na mtu katika jambo lolote,mana unaweza kudhan jambo flan ni kwa maslah ya taifa na ukawa na sababu ambazo kwako ni za msingi lakin mwenzako akaona vinginevyo kwasababu zinazomshawish yeye..ila nachukia unapotumia hila kuzuia wazo la mwingine hata kama linamantiki na kumnyima nafas ya kushawish wengine juu ya wazo lake/kudiscourage wengine hata kumuunga mkono, tena unafika mahali unajifanya hamnazo hata kama unaelewa kinacho. Walichofanya Makamba na Madam Anna sielew kina mantiki gan..Madam Anna kama jins alivyomezeshwa, kakurupuka akianza kwa kunukuu kanuni za bunge anazotaja kua zinaendana na katiba kua; wabunge wakitaka kuleta motion ya ktokua na imani na PM ni lazima waandike barua iliosainiwa na wabunge wasiopungua 20% ambao kwa idadi ya bunge letu ni wabunge 70 then wawasilishe kwa speaker 14 days before intended date of vote..after that akakurupuka"zoez linaloendelea la kupigishana sahihi ni batili kwakua mimi sina taarifa". Sasa taarifa ipi unayotakiwa kupewa mama zaid ya barua yenye saini sabini ambazo ndio zinatafutwa kwa hilo zoez unaloita batili?au hizo sahihi zinapatikanaje basi ili zoez la zitto lisiwe batili kwa mujibu wa kanuni zako?kama kanuni inatoa mwongozo wa namna ya kuandika barua yenye sahihi sabini pasipo kuzikusanya bungen ungefafanua. Hata hivyo huyu mama honestly nimefika mahali nashindwa kumlaumu kwan mara nyingi hua namuona kama hana uwezo wa kufikiri kwa haraka. Akipandikizwa kitu mradi ni cha chama chake nae huenda hewan bila kujiongeza. Lakin Makamba anaelewa kabisa alichofanya sio. Na unafiki wake uko hapa;mara ya kwanza hoja ya sain zitto aliitoa bungen na kutoa wito kwa kila mbunge mwenye nia njema na nchi, na anaeona kua ubadhilifu ulioripotiwa na CAG kufanyika katika wizara mbali mbali unamkera na unastahili hatua kuchukuliwa basi atie sain yake kwe hiyo barua kesho yake asubuh ambapo yeye Zitto alieleza atakua akikusanya sahihi hizo nje ya bunge. Hapa ndio mana hata kina Deo walitia sahihi .
Sasa yeye (Makamba) anapokuja kulalama eti mara nyingi tumekua tukiimba kua tunataka bunge la umoja na huku akijifanya kama hajui hilo zoez la kutia saini linaendaje,nakuhoji kama Madam ana taarifa ya zoez linaloendalea,tena anenda mbali na kudai kua anasikia kwe vyombo vya habari kuhusu hilo zoez!!!!???
Huu ndio unafiki kwan maombi ya saini yalitolewa bungeni na utaratibu uliwekwa wazi. Isitoshe saini zenyewe zilikusanyiwa bungeni na si kwe ofice za CDM.
Ye angekua muwaz tu na msimamo wake kua walichofanya mawazir wa ccm haoni kama kinawafanya kustahili kuwajibishwa au labla anaona kuwawajibisha kwa kupitia kumpigia vote of no comfidence PM ni excessive measures na haina maslah kwa taifa mi ningemuelewa kwakua huku ndio kutofautiana mtazamo kuhusu jambo fulani. Au angekaa tu kimya kwan kuna mtu angemuuliza?
Kama kweli maana nyingine ya Parliament ni kundi la mabundi basi hiyo ni tafsir sahihi na waliotia sahihi ni wachache wenye bahat mbaya waliolazimika kuchanganyika na mabundi katika kutetea nchi yao.
Ukitofautiana na mtazamo huu kwa dhati sikulaumu kwan n haki yako. Nawasilisha.