Natamka: sitapenda tena.

Natamka: sitapenda tena.

Maswa 1

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
673
Reaction score
999
Kama niliyempenda kuliko chochote amenifanyia hivi, nilimwamini nilimpa moyo wangu wote naye akanionyesha mapenzi niliyodhani ni ya dhati, lakini leo hii amenisaliti, ameniacha, kweli?! Hakuna wa kumuamini hapa duniani. Wacha nilee wanangu. Hao ndio faraja yangu pekee.
Siongelei mahusiano! Naongelea fursa. Naongelea macho yetu ktk milango ya fursa. Macho yetu maranyingi yamejiseti kuona milango iliyojifunga, yapo kuitafakari kwani imejifunga, kwanini sikujua kama itajifunga, nitatokaje ktk hiki chumba cha mateso hatimaye huamua kutulia hapohapo tukidhani mlango huo utafunguka tena. Rafiki, huo mlango acha uwe umejifunga hebu angaza macho yako kwingine uone milango iliyowazi ikisubiri upite. "Kasuka, sioni!" Utaonaje wakati macho yako yana machozi yakililia mlango uliojifunga. Amin amin nakuambia mlango mmoja ukijifunga kuna milango mingine inafunguka. Nimeishi miaka mingi sasa, nimekaribia hata nusu ya uhai wangu! Nimeona hili kwangu na kwa watu wangu. Ukifuta machozi utaona mlango mpya. Mitaji inakufa na mitaji mipya inapatikana, biashara zinakufa biashara mpya zinafunguka, unaachwa anaibuka mwingine bora akikuhitaji. Mwache aende, mfute ktk kumbukumbu zako ili umpokee vzr huyu ajaye. Unaweza ukasema Kasuka unaongea hayajawahi kukukuta, ningekupa yangu ungejiona wewe umebarikiwa kuliko wanawake wote, aah sorry kumbe wewe ni mwanaume! Naomba nikukumbushe mtu aliyezaliwa hawezi kuona, hawezi kusikia na hawezi kuongea lkn akaamua kutokukata tamaa, Helen Keller! Yeye alipoishinda changamoto hii alisema, "Watu hawaoni milango iliyowazi kwasababu macho yao yameng'ang'ania ktk milango iliyojifunga." Je mlemavu huyo ukikutana naye mbinguni utakuwa na cha kujitetea khs kutokufikia hatima yako ukiwa na utimamu wa mwili? Umeachwa ndiyo, so what? Biashara imekufa ndiyo, so what? Hujasoma ndiyo, so what? Hujaolewa ndiyo, so what? Hakuna kisingizio, amka ufanye mambo! Mungu kakuamini kukupa fursa ya kupitia magumu ili uwe shujaa atakayewatia moyo waoga na wasioamini ktk kuinuka tena. Maranyingi fursa zimevishwa vazi chakavu, vazi la magumu kiasi kwamba haziji zikiwa zinavutia. Unaijua fursa iliyomjia Mandela ya kuwa mkombozi wa watu wake? Ilikuwa imevishwa vazi la kifungo cha miaka 27 gerezani, alipotoka watu wanashangilia ubora wake, wanatamani wawe bora km yeye ila tu wasilipe gharama kama zake! Penda tena, penda maisha tena. Pitia ktk mlango ulio wazi. Fungua macho yako, hatima yako njema bado iko wazi.

Stay blessed
 
Umetamka tumekusikia. Tamko haliwezi kuuzuia moyo usipende tena!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom