Natamani Mdahalo wa Wagombea Wenza wa Urais Kenya ungetokea Kwa Tanzania mwaka 2015 au 2025 ili tujue Ugoigoi wa Watu

... hivi ni kwanini CCM hawapendi midahalo? Zaidi ya ule wa 1995 akiwemo Mkapa, Lyatonga, na Cheyo CCM hawajawahi tena kupenda midahalo! How comes chama kiongozi (since independence) kinakwepa midahalo?

Funny enough, 2015/2020 CCM ilimsimamisha PhD holder yet wakakwepa midahalo; kuna uhusiano gani kati ya CCM na kutopenda midahalo? Hebu political scientists mfanye research kupata jibu la hii kitu.
Wanajua fika wataaibibika
 
2015 Aliyekuwa mgombea mwenza angeweza mdahalo kama aliona Zuhura Yunus tu anamuonea kwa kumuuliza maswali? Ila kwa bongo haikuwa shida watu bado walikuwa na matarajio makubwa kuwa mtu huyo anawafaa kuwa rais wao.
 
Sijui kwanini tunapenda kujilinganisha na maskini wenzetu kenya.

Inapaswa tujilinganishe na huko mbele ili tupige hatua.

Kenya ni Taifa ambalo wanasiasa ndio wameishika nchi.

Uchumi wa kenya upo chini ya wanasiasa ambao ni matajiri.

Kenya sio nchi ya kujilinganisha nayo hata kidogo, imejaa ufisadi mtupu.
 
... hivi ni kwanini CCM hawapendi midahalo? Zaidi ya ule wa 1995 akiwemo Mkapa, Lyatonga, na Cheyo CCM hawajawahi tena kupenda midahalo! How comes chama kiongozi (since independence) kinakwepa midahalo?

Funny enough, 2015/2020 CCM ilimsimamisha PhD holder yet wakakwepa midahalo; kuna uhusiano gani kati ya CCM na kutopenda midahalo? Hebu political scientists mfanye research kupata jibu la hii kitu.
Midahalo itawaumbua. Vichwani ni weupe kama sufi. Ndio maana wanatamani hata watushone midomo, mitandao wafungie n.k. Kimsingi CCM wanatamani watanzania wote tuwe wendawazimu ili watawale bila bugdha.
 
Smart wapi? Mbona anaonekana kabisa ni psychopath case?
Huo ni mtizamo wako
Mimi namfahamu amekuwa waziri wa sheria na katuba under President Kibaki.
Alijizolea umaarufu alipokuwa team Kibaki kwenye kikao cha usuruhishi Kufuatia machafuko baada ya uchaguzi wa mwaka 2017.
Pannel ya usuruhishi ilikuwa na viongozi mashuhuri na marais wastaafu chini ya uwenyekiti wa hayati Koffi Annan.

Martha Karua akiwa team Kibaki alimuuliza Koffi Annan swali tata mpaka mzee wa watu akakosa majibu mazuri.

Hii ilikuwa ni baada ya one of the pannelist ambae alikuwa Rais mstaafu wa nchi fulani kuongea kwa kujiamini sana huku akijaribu kuwabana team Kibaki katik mgogolo huo.

Hapo ndipo Martha Karua alimuuliza mwenyekiti kuwa huyo msemaji aliteuliwaje kuingia kwenye team ya usuruhishi wakati hana moral strength ya kuzungumzia jambo lolote kuhusu machafuko wakati yeye alisababisha machafuko nchini mwake yaliyosabisha mauaji na kupelekea watu kukimbia nchi na kutoa mfano kuwa wakimbizi wengine wanahifadhiwa nchini Kenya kwenye kmbi za shimoni na Dadaab.

Akaendelea kusema kuwa pamoja na machafuko, Kenya haina wakimbizi kama ilivyo kwa nchi jirani bali ina displaced people.

Mzee wa watu alipoteza confidece na hakuwahi kuchangia chochote tena mpaka mwisho vikao vya usuruhishi.

Wakati huo team Odinga ilikuwa na Ruto,Profesa Anyan'ga nyon'go na wengineo


Huyo ndiye Martha Karua nimjuwae.
 
Sisi Tz kukataa midahalo ya wagombea ni kuthibitisha kuwa bado saana katika nyanja mbalimbali, na kuwa huenda au elimu zetu ni za mchongo au michakato yetu ya kupata wagombea smart ni mchongo.

Lazima kuwa jaribu wagombea wetu wapoje up stairs kwani kuna ubaya gani.

Mtu anapewa mamlaka makubwa namna hii, anaongoza watu zaidi ya milioni 50 halafu wapiga kura tumpigie tu sababu ya mbwembwe za chama chake wakati wa kampeni kweli?

Hata wabunge wetu, ilipaswa wawe wanajieleza mbele ya wawakilishi wa wapiga kura jimboni na kujibu maswali kuwa watasimamiaje vipaumbele japo viwili tu kwa miaka mitano.
 
Back
Top Bottom