Natamani kusema ila nashindwa

ketete

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
792
793
Kwa muda mrefu kifua kimebana sana kwa mambo yanayoendelea kwenye Nchi ile, sijui ni mimi mwenyewe???

Katibu wa chama cha Nchi ile anasema kila mkoa umeunganishwa kwa lami asubuhi nimeona akisema kwenye "VTI " ,sijui hajui kwamba hata mkoa wa "MAGOKI" bado haujaunganishwa.
Uongo huu ukiendelea unatupeleka wapi???

Natamani kusema kwamba huyo NDUTU wamwache tu ila walekebishe mapungufu yao. Kwani ukweli bado upo na unaonekana.

Hivi wapinzani wa Nchi ile ndio wanamakosa sana?? Hata kuwaweka ndani na wasifanye kazi zao ,natamani kumwambia MKULU angewaachia tu kuwaachia ni moja ya busara kubwa.

MKULU ,hivi ,huko ofisini kwingineko rushwa imekomaa kwa kasi sana, ni ajabu hata watu wako wamesahau kuwa unatumbua.

Nchi ile inakoelekea "kuzuri" bahati mbaya pambio na wimbo wako MKULU watu hawauelewi, hivyo unakwenda na wasiotaka kwenda, utafika nao wasikotaka wafike.

Nchi ile elimu yake imevurugika ni heri mitaala ya miaka ile..... Siku hizi eti mwenye D mbili kidato cha pili, eti kafaulu!!!! Sijui wanakwenda wapi !! Ningeshauri wangerudisha tu mfumo wa wastani kama kipindi kile......

Nchi ile kuna wasomi DHP wasio tambua usomi wao ili kuisaidia Nchi ile bali wanafanya yao kupata teuzi tu na kumwogopa MKULU, wengi ni vigeu geu, hawana misimamo, wanachokisimamia leo ndicho watakachokikana kesho ,nawaza sana ......
.
.
.
Natamani kusema.... Ila nashindwa, maana yapo mengi naamini mtanisaidia tu

Natamani Nchi ile ingewaheshimu na kuwapa stahiki zao watumishi waajiriwa maana kilio chao ni kikubwa sana, vyama vyao havina meno......

Acha nivute pumzi......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa muda mrefu kifua kimebana sana kwa mambo yanayoendelea kwenye Nchi ile, sijui ni mimi mwenyewe???

Katibu wa chama cha Nchi ile anasema kila mkoa umeunganishwa kwa lami asubuhi nimeona akisema kwenye "VTI " ,sijui hajui kwamba hata mkoa wa "MAGOKI" bado haujaunganishwa.
Uongo huu ukiendelea unatupeleka wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo mkoa si ndo ule anaotoka mheshimiwa TTOZI anayemuumiza kichwa bosi wa NGEBU mheshimiwa IGANDU na kuisumbua serikali ya mheshimiwa MPJ? Hapo unategemea nini?...
 
Back
Top Bottom