cheichei2010
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 932
- 351
Huna cha kupoteza na ushakuwa mtu mzima na una maisha yako. Regardless ya kile alichokuambia mama na ulichosikia popote msamehe na move on with your life. Afterall hakusaidii wala hakupunguzii chochote ni kiasi cha wewe kuondoa hasira moyoni mwako kaa kwako endelea na maisha yako na iwapo yeye mwenyewe atajiona baadae huko kuwa ana makosa anaweza kukutafuta. Ila moyoni mwako ondoa hizo hasira na ishi kama kipindi ambacho ulikuwa hujamjua wala kumuona.
Kwani miaka yote ulipungukiwa na nini wakati hakuwepo katika maisha yako. endelea na hayo hayo na muone kama hana nyongeza yoyote katika maisha yako.
Unajua mambo ya mahusiano yanashida nyingi na matatizo makubwa.Katika mahusiano wanawake huwa ni wepesi sana wa kusimulia matatizo ya waume zao kuliko wanaume wanavyoweza kuvumilia na kulilia moyoni.sasa Huyu jamaa kusikia stori ya upande mmoja kishamuhukumu baba yake.
jambo moja nalokushauri mpende baba yako na umuheshimu hata kama kuna matatizo yalitokea kwa upande wake,wewe huyajui.lakini ukitaka kufukunyua utakuja kukuta kuna kitu kibaya kabisa mama yako alichomfanyia baba yako, kiasi kwamba hakutaka hata kuwa karibu na nyie, kwani alijua kupitia nyie mama yenu angeweza kuwa na access nayo.
Nachokushauri achana na kutaka kujua nni kilitokea kati yao utakua dissappointed big time.Daima maisha ya wapenzi yana unafiki mkubwa ambao hutakuja kujua yupi ni mkweli na yupi ni muongo.
nakushauri endelea kumtembelea baba yako, ikiwezekana mpeleke na mdogo wako.Baada ya muda kuna siku mzee atakuja kukuambia kitu.kwa sasa hawezi kwani anajua kuna mambo mabaya juu yake ambayo mama yenu amewajaza kiasi kwamba mnaweza mdhuru.Ukimtendea wema kuna siku atakuja jua kwamba kwa kutokuishi nanyi aliwadhulumu,haki ya malezi mpaka mmeathirika kisaikolojia.Atakuja omba radhi na mtaanza maisha mapya ya amani na upendo.
Ijapokua hili la kumtembelea baba yako kuna siku litakuja kuleta mgogoro kati yako na mama yako pengine na huyo baba wa kambo kwani hawatapenda muwe na ukaribu uliomkubwa kuliko kwao.Lakini mwisho wa siku huyo ni baba yako,hata upinduke ,ugalegale vipi.Masikio hayazidi kichwa.Utamuhitaji tu,kwa namna moja au nyingine siku moja.