Natamani kumsamehe baba mzazi

Natamani kumsamehe baba mzazi

umefanya vyema kumtafuta na kumfahamu.


usiache kumpitia baba yako na kumjulia hali, usisahau kuwapeleka na wadogo zako. jenga maisha yako na ondokana na chuki ulizozijenga kwa baba yako. muonyeshe heshima baba yako japokuwa unajitegemea na yeye hakutegemei.

Jamani mnavyomshauri mwenzenu awapeleke na wadogo zake mnakosea. Yeye keshajipeleka mara tatu na mzee amekiri anamtambua na anawatambua wadogo zake. Nadhani inatosha. hayo mambo ya father to son akafanye na babake mlezi walau kuna bond. Msisahau hawa watoto wako kwenye familia, wana baba yao mlezi. Mtu unakurupuka tu kuwaswaga wadogo zako wakamuone baba yao mzazi hata baada ya matokeo ambayo umeshayaona? Kuna wakati huwa tunang'ang'ania sana ukweliii ukweliii...lakini ukweli unaotekelezwa bila hekima husababisha majanga. Mdoe hapa alipofikia anahitaji hekima sana maana anaweza kujikuta ameharibu furaha na amani ya familia iliyomlea kwa sababu ambazo kiukweli zinazuilika kwa kusamehe na kusonga mbele.
 
Aise usimtafute ukamuuliza, mimi nina experience na mambo haya, wewe soma upate kazi au ujiajiri upate pesa yeye ndo atakuja mwenyewe.

Hatuendi hivyoo,because money is not everything in this world,what if akikosa kazi wala asiwe mfanyabiashara i mean awe wa kawaida sana,itakuwaje?
 
Ila mkuu uamuzi wa kumsamehe mzazi ni busara zaidi, dhambi zake muachie mwenyewe wewe jisafishe tu kwake, usimuhukumu

Hebu pitia huu uzi hapa kwa hisani ya everlenk
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=735486

Asante utafiti kwa kuleta huu uzi,pole sana mdoe kwa unayopitia,hongera kwa kuwa na shauku ya kumjua baba yako,ila usijali wala usikate tamaa mpaka hapo yatosha,Tangaza msamaha si kwamba anastahili la hasha ni ili na wewe upate amani ya moyo,muombe Mungu nguvu ya kulitekeleza hili,mpe heshima yake kama baba bila kuhoji chochote,si ajabu siku moja naye akafunguka kwanini alifanya hayo,na zaidi muombee kwa Mungu,mtunze mama na mdogo wako.

Mungu akusaidie,nimeona hapo juu umesema kesho utaenda kumtembelea ni vizuri sana ila angalizo kuwa makini sana shetani naye yuko kazini hata ukikutana na jambo lolote la kukera,ama yeye dady wako akaongea lisilofaa take it easy,unapokuwa kwenye hatua ya kusamehe vikwazo vingi sana hujitokeza,Mungu akutangulie kwa kila jambo.
 
Last edited by a moderator:
Mdoe nakushauri kazana na maisha yako usimtafute kamwe. Si alisema nyie ni zawadi ya mama? Mtunze mama yako na baba mlezi aliyewalea kipindi chote hicho. Kwanza mlezi wenu akiona sasa mmepata maisha mnampa heshima aliyewatupa atakasirika sana. Sijui baba yako ni kabila gani ila wako wengi wa aina hiyo. Mimi nina shemeji yangu anayejiheshimu na wa heshima kabisa hata waliosoma naye au kuwa naye karibu wanamsifia. Shemeji huyu aliolewa na Mkibosho miaka ya tisini. Wakajaliwa mapacha ila.pacha mmoja akawa na mapungufu hadi leo. Yule mkibosho alimkimbia na kumwachia pacha hao miezi minne na shemeji hakuwa na ajira kipindi hicho. Ni story ndefu. Ndugu tulimchangia shemeji kama mjane. Mungu si athmani shemeji yetu alipata kazi akalea watoto na shule nzuri pacha mmoja alisoma na yuko sekondari shule nzuri pia. Cha kushangaza yule ---- Mkibosho alimfuata pacha mmoja shuleni akajitambulisha na mtoto akamkana mbele ya waalim na kuondolewa nduki. Alipotueleza ndugu tuliafikiana tu kuwa kwa usalama wako Philip Gaspar Mboya wa Bank of Tanzania asisogelee wale watoto na ukoo tumeshawapa. Ulimwambia shemeji kuwa watoto ni zawadi yake na alipokuambia muwabatize ulisema utafurahi wakibatizwa bila wewe kuwepo. Mungu si athmani dmsheneji sasa ni Mkurugenzi taasisi fulani na maisha super sana. Mdoe usife moyo kazana piga moyo konde. Msimfanye mama yenu audhike kwa kuwa kinguvu ulimtafuta baba yenu. Moyoni ataumia sana. Just stick to your mom and your God given father. Baba si kufyetua mbegu bali ni kutunza. Anayekutunza ndiye baba yako na si vinginevyo.
 
Wababa wa hivi ni kuwa shit tu yaani hakuna kumtafuta kamwe. Mpende akupendaye. Yaani ningekuwa beneti na baba mlezi yatosha. Tit for tat. Ningekuwa Steve Job kabisa.
 
Mimi ni Kijana wa miaka 30. Nimezaliwa katika familia masikini, mkoani Kilimanjaro. Nimeanza kujitambua nikiwa na umri wa miaka mitano nikiwa mikononi mwa bibi wa mama yangu. Sikujua ni kwanini niliishi na bibi wa Mama lakini Baada ya muda, Mama alikuja kunichukua na Nikaenda kuishi nae wilaya nyingine mkoa wa Kilimanjaro ambapo nilianzishwa masomo ya elimu ya chekechea na msingi. Mama yangu ana watoto wane, mimi nikiwa wa pili.

Mtoto wa mwisho ni mtoto wa baba yetu mlezi, ambae nilikuja kubaini kuwa Yule sio baba yangu mzazi, ila ni mlezi kufuatia vijimaneno vya mjomba na Mama yangu mdogo aishie kijijini. ( Wewe mu-uru, . Wewe mkibosho, nk. Wakati Baba tuliekua nae ni Mzigua) Nilikuja kubaini hilo nikiwa kidato cha nne.

Nikaanza kupata Kiu ya kumjua baba yangu mzazi.
Baada ya kumaliza kidato cha sita, hamu ya kumjua baba yangu mzazi ilizidi. Nikamfuata mama yangu mdogo (R.I.P. mama mdogo), ambae alikua akiishi moshi maeneo ya Pasua.

Sikutaka kumbughudhi Mama yangu kwasababu niliona tabu zote alizopitia katika kutulea na kutusomesha. Nilijua wazi Mama mdogo atakua anamjua vizuri dada yake (Mama yangu), na anaweza kuwa na clues muhimu kumpata baba yangu. Alikataa sana, ila mama ni mama.

Nilijua niseme nini na nimshawishi vipi na hatimae alinipa details za baba yangu japo hakujua alikoishi. Kutokana na details nilizopata, ikiwa ni pamoja na sehemu alizofanya kazi, nilifanikiwa kumpata mtu ambae alinipeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.

Nilimuona na nikajitambulisha. Niliposema tu nilipotokea alinijua mimi ni nani. Akanitaja jina. By then I was around 16. Nilikaa kidogo na akanipa namba za ndugu zangu kibao niwatafute. Niliwatafuta baadhi na nikajenga nao ukaribu. Nilidhani baba, pamoja na kutokua na uwezo (Amestaafu), angetambua uwepo wangu.

Ila zaidi ya mimi kwenda kumsalimia na kuwa kama mgeni yeyote tu wa kawaida anaekuja na kuondoka, hapakua na la ziada. Hakutaka kujua naishije, niliishije, nini malengo yangu, … no dad to son talk at all. Mategemeo yangu ya kumuona na kuongea na Baba yalipotea kabisa. Nilimtembelea kama mara tatu na baada ya hapo nikakaa kimya kuona kama atanikumbuka japo kwa ku beep.

Baada ya muda, niliamua kumchunguza mama taratibu kujua kulikoni. Nilianza kwa kumuambia kuwa namjua Baba yangu mzee …(Nikamtaja jina). Alishtuka kidogo hatimae akaniambia kua ni kweli, huyo ndie baba yako. Baada ya siku kadhaa, Mama aniliita faragha.

Akaanza kunisimulia mambo ambayo baba alimtendea, iliniuma sana. Ilifika kipindi mama anaomba ridhaa kwa barua kwa baba kuwa tupelekwe jando (Ikumbukwe kuwa walishaachana miaka mingi nyuma), baba anajibu kwa barua kuwa “Hao watoto ni zawadi yako nimekupa. Fanya chochote unachotaka”.

Sijui nini chanzo cha ugomvi wao, sijui nini kilipelekea wao kuachana, sijui ni kwa nini tuliishi maisha ya shida sana na mama aliteseka sana peke yake kutulea na wakati baba alikua na uwezo, ila kwa vyovyote vile, baba alitakiwa kuonyesha kuwa altujali wanae.

Ameniona mimi tu, Mdogo wangu alienifata nae ni mwanae, ila wala kumuulizia hamuulizii. Niliwahi kumuuliza kuwa anamtambua mdogo wangu kuwa ni mwanae akajibu kuwa Anamtambua.

Mada ambayo wana Jamiiforums nataka wani shauri ni uamuzi ninaotaka kuuchukua sasa.
Nimemchukia baba yangu ever since nimemuona. Ila inawezekana kuna mengi mengine ambayo siyajui kati yake na mama yangu. Nafikiria kwenda kuongea nae aniambie mambo mengi sana kati yao na kwanini ametususa kiasi hicho.

Japo sidhani kuwa ni uamuzi sahihi kwani niko na baba mlezi ambae kwangu mimi amebeba thamani yote ya neno Baba. Natamani nimsamehe ila sina pa kuanzia. Namuona kama womanizer kwasababu ana watoto sita nje ya ndoa yake, mimi na mdogo wangu tukiwa wamoja wapo.

(Hakuwa amemwoa mama, inavyosemekana alimdanganya, akamzalisha kumbe ameoa). Je, ni uamuzi sahihi kwa mtoto kum face baba yake na kuhoji ukweli wa yaliyojiri kati ya baba na mama?

Kwanini he was irresponsible kwetu tukiwa wadogo? Lengo ni kupata sababu yakumsamehe ili nafsi iwe na Amani kila nikimkumbuka, Badala ya chuki na hasira.

Niwieni radhi kwa uzi mrefu na mchanganyiko wa lugha.

Bila samahani brother. Hata ungekuwa mrefu aje,uzi huu ningeumaliza tu! a very welcoming movie. kila mstari unakuvuta kusoma mstari unaofuata. Umeupanga swadakta. Hongera.

#NOW , kwa upande wangu,naomba nikusaidie hivi;
Baba ni damu yako. it's a very unique and vital issue ambayo kwa namna yoyote,nakushauri uendelee na procedures za kutafuta suluhu na mstakabari wako na mzee wako.

Nijambo la kheri na baraka sana kama juhudi hizo zitafanikiwa. Namuomba Mungu aweke mkono wake zifanikiwe. Itakuwa furaha sana na Faraja mno. Nina ushahidi wa hilo,Baba yangu alimtafuta babu mwaka 2000 ilhali Babu alimwacha Bibi tangu mwaka 1971(ingawaje mazingira ya mahisiano kati ya bibi na babu hayakuwa #harsh sana),lakini ukweli unabaki kuwa,bibi alitelekezwa na kazi ya malezi ikawa ngumu(just like your mother got trouble rearing you).

Pamoja na hayo,zingatia kwamba,in #case mzee asipoonesha responce nzuri(despite your good approach to him), usimbembeleze. Achana naye(lakini si kwa kumkashifu au namna yoyote mbaya),mteme kiaina tu kwa kukata mawasiliano.

WATAONGEZEA WENZANGU WENGINE HUMU.
**Naomba Kuwasilisha**
 
Jamani mnavyomshauri mwenzenu awapeleke na wadogo zake mnakosea. Yeye keshajipeleka mara tatu na mzee amekiri anamtambua na anawatambua wadogo zake. Nadhani inatosha. hayo mambo ya father to son akafanye na babake mlezi walau kuna bond. Msisahau hawa watoto wako kwenye familia, wana baba yao mlezi. Mtu unakurupuka tu kuwaswaga wadogo zako wakamuone baba yao mzazi hata baada ya matokeo ambayo umeshayaona? Kuna wakati huwa tunang'ang'ania sana ukweliii ukweliii...lakini ukweli unaotekelezwa bila hekima husababisha majanga. Mdoe hapa alipofikia anahitaji hekima sana maana anaweza kujikuta ameharibu furaha na amani ya familia iliyomlea kwa sababu ambazo kiukweli zinazuilika kwa kusamehe na kusonga mbele.

hata ushauri wako huu ni vyema pia. ila zingatia taarifa zilizopo ni za upande mmoja na hao wadogo zake siku za usoni wanaweza mlaumu kaka yao kwa kuwaficha baba yao mzazi. pia umri wa wadogo zake pia auzingatie.

huwezi jua pia kwamba huyo baba mlezi ndio chanzo cha matatizo yote. nawaza tuu...
 
Kuna uzi humu ulishawahi letwa unaitwa "NGUVU YA MSAMAHA"

Kiukweli, story yako imeniuma sana kujua mzazi anaweza act like no body to his sons.

Anyway nakuombea ufanikiwe katika uamzi wako maana uko sahihi kabisa.

Msamha utafungua vitu vingi katika maisha yako na ta baba yako na mwisho familia nzima.

Pole sana, Mwenyezi Mungu kusaidie.
 
mkuu samehe,,,, wengi wamekushauri.....4give and 4get,,,,, tambua mama yako analo moyoni,, ukiweza kumpelekea sukari au kitochi, do it u r the man at all.... best wishes sir.
 
Kwani wewe unataka baada ya kumsamehe nini kiendelee? Kama ni suala la kuwa na mahusiano na huyo "Sperm Donor" tayari ameshaonesha kuwa hana mpango (kwa maneno - kwa mama na kwa vitendo - kwa kutokuonesha interest na maisha yako na ya mdogo wako). Sasa wewe unachotafuta hasa ni nini? Hivi hao wambea wasingekwambia kuwa wewe siyo mtoto wa huyo BABA yako unayemwita wa kulea ungekuwa unahangaika na huyo "Sperm Donor" sasa hivi? Wewe kubali tu kuwa yaliyotokea yametokea na huwezi kubadilisha historia bali unaweza kujifunza kutokana na historia ili usije kurudia makosa kama ya huyo "Sperm Donor" kwa watoto wako wa baadaye.
 
Mbele ya mtutu wa bunduki,hakuna mtu itaongea uongo,kama unayo mkuu,mfate umuhoji kulikoni awatelekeze!
 
kwa maelezo yako mpaka sasa baba yako anaonekana kutokukukubali....cha msingi ww fanya yako maadamu ameshajua upo siku akikuhitaji atakutafuta
 
Hata hivyo una Moyo sana kumtafuta huyo baba yako mi ningempotezea tu hana issue yoyote maana mpaka nimefika 30yrs hana time na mimi.
Wazazi kama hao ndio baadae ushatoboa wanaleta mambo ya kiseng.e sijui we mwanangu sijui ilikua hivi kama ni mm nitakuchapa Makofi kwakweli.
 
Back
Top Bottom