Natamani kumsamehe baba mzazi

Natamani kumsamehe baba mzazi

pole sana ila kuwa muangalifu,usikute mama yako alishakujaza maneno fulani,ambayo pangine na baba yako anafahamu.
Ushauri.
Msamehe halafu endelea na maisha yako.
Wewe nimtu mzima sasa.
Don't live with the past.

Na hili ndilo ambalo silitaki. Unamsamehe mtu ila kichwani unajua kabisa alishasema mimi ni sadaka, hanihitaji tena. Kitu ambacho sijui ni kweli au sio kweli.
 
Let it go!

he should let him go binadamu gani katelekeza watoto miaka mingi watoto wanahangaika nae lakini bado hajirudi loh! kile kitendo cha kumtafuta na kuongea nae kinatosha fanya yako kaka!
 
Ni bora ukamsamehe hata kama aligombana na mamako na akawatelekeza. Baba ni baba hata awe vipi. Msamehe na uwe unampitia kumsalimu mara moja kila mwezi na kizawadi chochote. Kwa kufanya hivyo utakuwa umemshinda shetani.

Na iwapo wewe ni wa dini ya kiislamu basi utambuwe kuwa wewe ni mtoto wa mama maana mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto wa mama si wa baba.
 
Bado haoni umuhimu wenu huyo umejisogeza karibu lakini bado mkuu Mungu mwenyewe kaona jitihada yako achana nae huyo
Focus katika kumfanya mama yenu awe na furaha na ajione blessed kuwa na nyie kama watoto wake maana nyie ni zawadi yake toka kwa Mungu
 
Sasa naelewa mtu mmoja aliponiambia mtoto siku zote atamtafuta baba au mama yake mzazi hata umpe maisha mazuri vipi.

Pole kaka lakini jambo kubwa endelea na maisha yako kuujua moyo wa mtu ni kibarua kigumu. Ukizungatia mmekutana ukubwani.
 
Watu wengi huwa tunafukunyua mambo tukidhani yatatuletea furaha ila mala nyingi huwa ni huzuni. Ulipofikia inatosha. Ulitaka kumjua ,umemjua. Endelea na maisha yako. Msamehe usijibebeshe laana yake. Baba aliye kulea ndo baba yako. Mkuu pole sana hauko peke yako wapo wengi.
 
Mpwa wangu, hayakuhusu! Nyooosha mikono juu mshukuru Mungu kwajili ya Mama, mhudumie Mama na wengine na wewe jifunze jinsi ya kuja kuitunza familia yako kwenye misingi mitakatifu. You can not change the past maana hata ukijiua yaliyotokea yataishia kukuongezea uchungu na uchungu huleta hasira na hasira huleta dhambi. Muombe Mungu uendelee kuwapenda na kuwaheshimu Wanawake wote
 
Kaöngee vizuri na baba naye atakueleza yake mwisho wa siku utajua ukweli.kisha samehee yote.
 
Tat'zo moja ni kuwa atabakia kuwa ni baba yako hata kama utamsusa na no way unaweza kumpata baba mzazi mwingine. Na ukoo wako unatoka kwake kama unavyyona mama zako wadogo wakikuita kwa kabila lake. Ni kukubali kuwa huyo ndio mzazi wako na ujifunze kusahau na kusonga mbele.
 
Bado haoni umuhimu wenu huyo umejisogeza karibu lakini bado mkuu Mungu mwenyewe kaona jitihada yako achana nae huyo
Focus katika kumfanya mama yenu awe na furaha na ajione blessed kuwa na nyie kama watoto wake maana nyie ni zawadi yake toka kwa Mungu

Thanks mkuu
 
kama hakuweza kukusaidia maisha yote hayo na ukawa fresh tu yanini uanze kujichumia dhambI ya kumchukia mtu saa hivi? mwachie mungu aisee mana yeye ndio hakimu. usimdharau wala usimuonyeshe utofauti wowote...ishi nae vizuri, hayammbo yapo na yataendelea kuwepo. wewe husikiagi mtu anawaua watoto wake? sasa huyo na baba yako nani anaafadhali? shukuru kila jambo
 
mdoe, ulifanya vizuri kumtafuta baba yako, hii ni nzuri sana;
- Hujasema kama baba yako mzazi ana mke mwingine, inawezekana ikawa ni sababu ya kushindwa kufanya chochote au kusema chochote kuhusu nyie, ujue atakuwa alishawekwa kibano kiasi kwamba anaogopa kuachwa.

- Wewe utakuwa sababu ya kumfanya baba yako aseme lolote kuhusu nyie kama watoto wake na kwa kuwa mama yenu amekwisha ingia mahusiano na mtu mwingine huwezi kulazimisha lolote.

- Angalia maisha ya wazazi wako wanaishije, kama wana hali ngumu jitahidi usaidie kadri unavyoweza;

- Mwendeleze mdogo/wadogo zako.

.................... Pole sana hata hivyo....................
 
Last edited by a moderator:
Sijui ktk dunia hii kama kuna mwanamke ktk kesi kama hii akiwa yeye ndio mwenye kosa atamuambia mwanae ukweli kuwa yeye ndio mwenye makosa...kwanini ktk kesi kama hizi the story tellers ni wanawake tu na wanaonekana wabaya ni wanaume tu???huwa najiuliza sana
 
Japo haiwezi kufanana na baba lakini nakupa mfano tu. tunaishi moshi lakini nina dada na kaka tumchangia baba wanakaa arusha miaka 30 sasa dada hajawahi kukanyaga kumsalimie baba ake hata asikie anaumwa karibia na kufa. Hao kaka inaweza kupita miaka zaidi ya 10 ndio mara anatokea. Hatupigiani simu wala hata siwajui maana pengine niliwaona mara ya mwisho mwaka 1993. Lakini ni ndugu zangu tu. Hakuna hisia zozote za ndugu baina yetu hata tukikutana ni kama umekutana na mpita njia tu. Lakini nimekubali hao ni ndugu wa damu kla mmoja ana ustaarabu wake maisha yanasonga mbele. Ninao ndugu pia tumechangia mama wanakaa hapahapa moshi na arusha na mwingine dar nina miaka zaidi ya 10 sijawaona na hata nikiwaona nimeshawasahau. Hata mama yao mzazi hawamjali. can u imagine?? lakini mimi sichimbi kuwauliza wazee ni kwanini. Hao ni ndugu zangu tu. Nimelikubali hilo na naendelea na maisha yangu. wote wao hata namba za simu sina na ni wakubwa zangu. Hivyo nataka kukwambia huyo atabakia kuwa baba yako tu iweke heshima yake. Siku ukijisikia kumsalimia kamsalimie na usimtendee ubaya na sishauri ukaanze kumchimba ujue hayo mambo kwa undani waweza umia zaidi. Pambana ndugu umsaidie mama yako mzazi asahau machungu ya mzee wako. hayo tu.
 
Huna cha kupoteza na ushakuwa mtu mzima na una maisha yako. Regardless ya kile alichokuambia mama na ulichosikia popote msamehe na move on with your life. Afterall hakusaidii wala hakupunguzii chochote ni kiasi cha wewe kuondoa hasira moyoni mwako kaa kwako endelea na maisha yako na iwapo yeye mwenyewe atajiona baadae huko kuwa ana makosa anaweza kukutafuta. Ila moyoni mwako ondoa hizo hasira na ishi kama kipindi ambacho ulikuwa hujamjua wala kumuona.
Kwani miaka yote ulipungukiwa na nini wakati hakuwepo katika maisha yako. endelea na hayo hayo na muone kama hana nyongeza yoyote katika maisha yako.
 
Back
Top Bottom