Natamani kumpata kila msichana apitaye machoni mwangu? Why? Ushauri ...pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kumpata kila msichana apitaye machoni mwangu? Why? Ushauri ...pls

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by PMNBuko, Jan 25, 2011.

 1. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wapendwa... Habarini za jioni?!

  Imekuwa ni kasumba yangu na pengine hata kwa wanaume wenzangu (ambao wako wazi kuzungumzia ukweli kuhusu wao) kwamba, kila akipita mwanamke/msichana mrembo (Asiye ndugu yangu) karibu au hata mbali kidogo, namgeuka na kutamani nimtongoze, na anikubalie. Natamani kumpata kila binti mrembo anayekatiza machoni mwangu. Wakati fulani nimetimiza azma hiyo, na nimefanikiwa na pengine najilazimisha kuacha kumfuatilia kwa lengo la kumtongoza. Mke ninaye na ni mrembo. Nina mpenda naye ananipenda tena sana. Binafsi, siifurahii tabia hii na ningefurahi kama ningepunguza kasi hii hasa ukizingatia hali halisi ya sasa kwani magonjwa ni mengi sana, hasa VVU/UKIMWI. Je, nifanyeje ili niepukane na tabia hii?? Je ni tatizo la kiafya? Tafadhali wanaJF nipeni ushauri unaonifaa kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu... Nashukuru!!
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,338
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  hii kali mkuu ila wanaume wengi tuna hisia kama hzo labda hata wanawake nao wapo hivi sema m sijui labda watatueleza
   
 3. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pole sana
  Yafaa umrudie mungu wako ktk imani yako ili kuepukana na khali hiyo. Kuna maandiko yanayosema kuwa

  "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake, ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe " 1kor 6:

  "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenye........" 1kor 7:2-5
   
 4. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Punguza tamaa kaka
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu. Labda sijui... ujasiri kwa wanaume? Lakini kuna tabia kuzidi kipimo, huenda kuna chanzo!!
   
 6. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ndo maana mmepewa UTASHI
  mbwa,paka ndo wanaparamiana tu tena kwa adabu ...mpk hamu imshike na si kudanda danda tu..IWEJE WE BNADAMU USHINDWE KUHIMILI HAMU /TAMAA ZAKO?
  kuwa bnadamu kakangu
  usijiendekeze....unakoelekea utamtaman mpk dadako...ehh ndo manake sa km hauna kiasi na wala kujizuia unashindwa wat do u thk?
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Banjuka tu Kiongozi - Maisha Mafupi .... Akikatiza tongoza tu!

  YouTube - DNA - Banjuka
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  usijiendekeze
   
 9. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hiyo ipo akilini.... usijitie katika vishawishi..., keep yourself busy na mambo mengine ambayo hayakuweki karibu mara kwa mara na hawa warembo kumbuka "A Zebra can Never Change Its Stripes" Once a Kiwembe Always a Kiwembe......
   
 10. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!! Hadi kufa??? Umeniogopesha.
   
 11. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka sina uhakika kama hapa kwetu tuna matherapist ili ningekushauri kwa kuanzia ukaanze kuonana nao kama watakuwa wanapatikana maeneo uliyopo.

  Haya mambo yanatokana kimsingi na mambo makubwa mawilli

  • Hereditary trait kwa maana ya ni kitu cha kiukoo au trait ya ukoo wenu...ukichunguza utagundua huenda babu alikuwa hivyo, baba akawa hivyo, baba wadogo e.t.c. it is like family or clan thing and it tend to run in your family. Hapa mjomba huhitaji sana therapist zaidi ya kumhitaji "Mpakwa mafuta wa Jehova" akuwekee mikono na kuvunja malaana yote ya ukoo yasikufatilie


  • Psychological effects: it create sexual pathway in your brain survival and rewarding system na hivyo ina-affect eneo lako la ubongo ambalo liko for your higher thinking, rational thought and judgment. HAPA HAKIKA UNAMHITAJI THERAPIST AKUSAIDIE eneo hili na kuna namna ambavyo anaweza kukuweka kwenye some kind of therapy inayokusaidia ku-easy hiyo hali mpaka unafikia mahali unatulia na unaweza kuwa na self-control
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa mwanamume kamili kutamani vitu vizuri ni kawaida kabisa na ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanaume tunatamani sana na si ugonjwa. Na hiyo feeling ndio inayokufanya uendelee kuwa na mwenzio, vinginevyo hata yeye usingekuwa nae.... hawa wenzetu nao wanajua hilo!!! Ila kuna kuishinda nafsi na hicho ndio kinachokutofautisha na mnyama..... ila ukizidiwa mara moja moja kusafisha nyota sio mbaya mkubwa :heh:
   
 13. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa ushauri huu mzuri. Nitaufanyia kazi. Sijachunguza vizuri kama hata wanaukoo wangu wako hivyo. Ila ninachofahamu, baba aliwahi kuoa wake 3. Sasa amebaki na 1 tu!!
   
 14. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aahh! Ok.
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tatizo:UNA TAMAA kupitiliza!Ushauri:ACHA TAMAA!
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,338
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  piga mazoezi kijana ial kama una pumzi ya kuwaapproach ni poa tu bora usije ukabaka tu
   
 17. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sifanyi kwa kupenda directly ila indirectly. Rose nifanyeje sasa??????????
   
 18. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Well said...kama unataka kukaa na familia na kutulia hili ni jambo la kushughulikia

  Tafadhali tafuta msaada zaidi wakati huu ambao sense yako inakusaidia kuona hili kuwa ni tatizo...ukichelewa brain system yako itakufanya uone ya kuwa ni jambo sahihi.

  Kwa mfano hadi hapa kuna watu wameshakushauri kuwa endelea kukamu, ni mawazo mazuri kimsingi kwa mtazamo wao, lakini je ndido msaada unaotaka? kama sivyo weka pembeni maana utaendelea kuathirika brain system yako na hivyo kujikuta huna mahali pa kuchomoka

  Kaka inawezekana kuwa na control ya mambo haya, nitaku-PM kukupa mfano mmoja mzuri wa mtu aliechomoka kwenye hali kama hii na kile alichofanya/alichosaidiwa mapaka akachomoka hapo
   
 19. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ivuga, pumzi ninayo. Na kwa bahati nzuri au mbaya, asilimia 75 ya wale ninao waaproach wanakubali. Wengine nashindwa hata kutimiza ahadi, hadi wanaanzisha ugomvi kwa kuniambia, sasa kama ulinitongoza kwanini hunipigii simu na wala hutaki tukutane??? Hapo sasa hadi wife adaka baadhi ya sms, noma mkuu!!
   
 20. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Babu yao hapo nimekupata vizuri kabisa...hapa unazungumzia thing of nature ambayo Mungu mwenyewe alituumbia ili tuhitajiane..

  Hata hivyo kila kitu kina utaratibu wake na kinapokuwa nje na kinyume na utaratibu wake basi hapo ni tatizo zaidi......Kwa ushauri na mtazamo wangu ni bora tumsaidie PMNBuko namna ambavyo ataji-control na kutumia ile kitu ambayo ni God's own made kwa utaratibu mzuri na awe na ustawi.

  Mpaka kaja kuweka wazi jukwaani basdi ujue amechoka na aliechoka anapewa msaada....AU SIO BABU YAO??

  Namaanisha atulie na kimwana wake kama wewe ulivyotulia na kimwana wako hapo...teheteh
   
Loading...