Natamani kumpata kila msichana apitaye machoni mwangu? Why? Ushauri ...pls

njo nikufanyie maombi, kwa mungu hakuna linaloshindikana.


Husninyo, naomba uniombee kimya kimya, make naogopa hata tukionana unaweza kuwa unaomba mie nawaza mengine!! Anyway, that is the way I am, but najaribu kuzuia mazingira niliyomo, sijui kama nitafanikiwa. Indeed pray for me!!
 
Hapo huna la kufanya mjomba mana watoto w cku hiz ni wakali balaa unakuta katoto kadogoo ht miaka 15 hakajafikisha ila ana mkia!!! mh! ..... ucjibanie mjomba kila anayejitokeza we tia neno 2.

Mkuu. Ushauri huu, naona.... duh!!! Unawezaje kunisaidia zaidi ya hapa mkuu????????
 
Husninyo, naomba uniombee kimya kimya, make naogopa hata tukionana unaweza kuwa unaomba mie nawaza mengine!! Anyway, that is the way I am, but najaribu kuzuia mazingira niliyomo, sijui kama nitafanikiwa. Indeed pray for me!!

i will. Mmh nakuonea huruma. Kazi unayo.
Jitahidi uyashinde hayo majaribu.
Ngoja nianze leo kufunga na kuomba kwa ajili yako.
 
Naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru nyooootee mnaoendelea kunipatia ushauri kuhusu hali yangu hii. Kwa namna ya pekee naomba mniruhusu PIA nimshukuru sana mwana JF mwenzefu, NewDawnTz kwa ushauri mzuri na wa kunijenga alionipatia huyo ndugu. Naahidi kuutumia kwa manufaa yangu sasa na hata baadaye.

Rai yangu kwa wanaJF ni kwanza, uwanja huu ni fursa kwetu. Ni muhimu kuutumia kujifunza. Ni mahali pa kubadilishana mawazo lakini pia ni sehemu ya kujifunza mambo mapya na kujiburudisha. Asilimia kubwa ya maneno tunayosikia sisi binadamu siyo mapya, lakini msisitizo wa jambo fulani hutofautiana always. Unaweza kuchukulia jambo poa tu kumbe mwenzio linamkera kweli hata kama yeye ndiye mtenda. Hivyo, ushauri wa kujenga ni jambo la msingi sana. Ndiye maana Biblia/Quran viliandikwa over 2000 years ago lakini bado watu wanatafsiri vitabu hivyo, na bado wengine hawajui namna ya kuvitumia. JF ni uwanja muhimu sana. Asanteni sana ndugu zangu na Mungu awabariki. Hata hivyo, nazidi kusubiria kuona ushauri wenu mwingine kuhusu hali yangu!!!
 
ndo maana mmepewa UTASHI
mbwa,paka ndo wanaparamiana tu tena kwa adabu ...mpk hamu imshike na si kudanda danda tu..IWEJE WE BNADAMU USHINDWE KUHIMILI HAMU /TAMAA ZAKO?
kuwa bnadamu kakangu
usijiendekeze....unakoelekea utamtaman mpk dadako...ehh ndo manake sa km hauna kiasi na wala kujizuia unashindwa wat do u thk?

Twajaribu kujizuia, Lakini nyie ndio mwatutesaaaaaa!!!!, kijicho hicho mwatufinyia(Rose),vishawishi kila kukicha, mara nyele bandia, mkorogo na wowowo za kichina, hio yooote ni kutupotezea!!!! Atajizuia mpaka Liniiiiiiii!!!!!
 
Kwa mwanamume kamili kutamani vitu vizuri ni kawaida kabisa na ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanaume tunatamani sana na si ugonjwa. Na hiyo feeling ndio inayokufanya uendelee kuwa na mwenzio, vinginevyo hata yeye usingekuwa nae.... hawa wenzetu nao wanajua hilo!!! Ila kuna kuishinda nafsi na hicho ndio kinachokutofautisha na mnyama..... ila ukizidiwa mara moja moja kusafisha nyota sio mbaya mkubwa :heh:

Swafiii Mkuu, hio Nyekundu Mpya
 
mwanaume tumeumbwa kutamani, lakini tumia akili usipelekweshe na tamaa za mwili.
 
Bila shaka umesharudi. Ushauri wako ni muhimu ili nizaliwe upya. Unasemaje?

onana na watu wa psychologia, upate kanselling juu ya hiyo hali, pia rudi kwenye masuala ya dini kufuatana na unakoabudu. Nakutakia mabadiliko mema. MUNGU AKUSAIDIE.
 
Huu ni wimbo tu mungu akubadilishe.(Macho yangu yamejaa tamaa siachi msichana kupita mbele yangu, pamoja nakua nimeoa lakini sina hakika ndo udhaifu wangu, ni hurumie nisafishe ni badilishe mungu mwenye rehema) Mungu akuponye kutoka pepo la uzinzi.
 
Ndugu zangu wapendwa... Habarini za jioni?!

Imekuwa ni kasumba yangu na pengine hata kwa wanaume wenzangu (ambao wako wazi kuzungumzia ukweli kuhusu wao) kwamba, kila akipita mwanamke/msichana mrembo (Asiye ndugu yangu) karibu au hata mbali kidogo, namgeuka na kutamani nimtongoze, na anikubalie. Natamani kumpata kila binti mrembo anayekatiza machoni mwangu. Wakati fulani nimetimiza azma hiyo, na nimefanikiwa na pengine najilazimisha kuacha kumfuatilia kwa lengo la kumtongoza. Mke ninaye na ni mrembo. Nina mpenda naye ananipenda tena sana. Binafsi, siifurahii tabia hii na ningefurahi kama ningepunguza kasi hii hasa ukizingatia hali halisi ya sasa kwani magonjwa ni mengi sana, hasa VVU/UKIMWI. Je, nifanyeje ili niepukane na tabia hii?? Je ni tatizo la kiafya? Tafadhali wanaJF nipeni ushauri unaonifaa kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu... Nashukuru!!

Ufanyeje?
Fikiria kuwa huyo mkeo umpendae na ni mrembo anafanya kama ufanyavyo wewe...hiyo haitoshi kuwa sababu ya wewe kuirekebisha tabia yako? Au meshajichagulia "ajali kazini"?
Huogopi mungu,,sawa basi hata maradhi huyaogopi?
Majuto mjukuu, ndugu...Kapime kama bado uko salama huhitaji ushauri ,unajua nini cha kufanya...hata kama utakuwa umeambukizwa basi ujitahidi usiambukize wengine..kama unavyotamani kuendelea kuishi na wengine vile vile.
 
Ufanyeje?
Fikiria kuwa huyo mkeo umpendae na ni mrembo anafanya kama ufanyavyo wewe...hiyo haitoshi kuwa sababu ya wewe kuirekebisha tabia yako? Au meshajichagulia "ajali kazini"?
Huogopi mungu,,sawa basi hata maradhi huyaogopi?
Majuto mjukuu, ndugu...Kapime kama bado uko salama huhitaji ushauri ,unajua nini cha kufanya...hata kama utakuwa umeambukizwa basi ujitahidi usiambukize wengine..kama unavyotamani kuendelea kuishi na wengine vile vile.

Ok. Nonda, thanks for your critical suggestions and opinions.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom