Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Natamani kujua kwanini alinificha jambo hili

Aisee pole sana ndugu.
Nahisi kigagasiko, ngoja nitulie kwanza ntarudi kwa "ushauri wa busara" baadae.
 
Pole sana.Mwenza mmoja kuwa na mtoto/watoto kabla ya ndoa imekuwa kama fashion.Kukuficha hajafanya jambo jema.Je ingekuwa wewe mwanamke ndiyo mwenye mtoto?Sipendi kuhalalisha ubatili wala kutoa hukumu.Kaa naye umbane hasa na akupe ukweli.Chekecha na utoe maamuzi.yako mkuu.Mapenzi hayana mjuvi zaidi ya mwingine.
 
Pole sana, but take this from me, kama kweli unampenda huyo jamaako then change huo msimamo wako wakutaka kuolewa na mwanume asikuwa na mtoto unajua hakutaka kukuambia pengine kwasababu anakupenda sana na kwa wakati munaanza uhusiano wenu alihisi angekupoteza hata kabla hamjafika mlipo sasa,

si unajua some times we did wrong things for the good ones. My self had the same issue with my women but the time alipokuja kujua ali argue sana and i gave her the good and the bad reason kwa nini nilimficha akanielewa, na huwezi amin anampenda mtoto kushinda hata mama mzazi wa huyo mtoto.And who knows pengine ndio mtoto pekee mungu amemjalia huyo jamaako na hatokuja kupata mwengine. So at least try to be reasonable.
 
Kwa nyakati hizi hautakiwi kuchukulia mambo 100% utajiua bure. Dont trus anyone except yourself or else utaumia bibie.

Badilisha mwelekeo kwa kukubali ukweli kuchunguza hata haukusaidii chochote.
 
labda alikuficha sababu anakupenda, na kwakufahamu msimamo wako angekwambia ukwel asingetimiza lengo lake!
haya ukishaujua ukwel AMUA SASA
 
Kwani mtoto ana tatizo gani miaka hii ukitak mwanaume acye na mtoto shughuli ipo. Labda niulize mfano WW ndo ungekuwa na mtoto hlf huyo mwanaume hakutaki ungejickiaje? Coni Km mtoto ana tatizo ktk mahusiano. Il à sie washauri tu maamuzi juu yako
 
Bado wewe mwenyewe ndio unaweza kuamua kama unaendelea na huyo jamaa yako au unamwacha. Hujaweka wazi hapa kama huyo jamaa ana shida nyingine zaidi ya hiyo ya kua na mtoto, Wewe ndo unajua uzuri wake na ubaya wake na inawezekana kweli alipata huyo mtoto kwa kukucheat.

KI uhalisia kabisa, mimi ndio kama huyo mtoto unaemkataa wewe, utofauti tu ni kwamba mimi sikukataliwa, Mungu aendelee kumbariki mwanamke huyu ambae alikubali kunilea kwa upendo zaidi ya ule alionao kwa watoto aliowazaa. Siwezi kueleza zaidi

lakini mama yangu mzazi aliondoka mapema (RIP) leo hii mama yangu huyu (kutoka lwa Mwenyezi Mungu) anafaidi matunda ya kunilea ikiwa ni pamoja na mimi kusomesha wadogo zangu. Jibu unalo mwenyewe, kusuka au kunyoa.
 
Kwnza pole sana, mimi mwenyewe mpaka hivi ninavyo andika Haya mahusiano yangu ni kama sijui kama yanaweza kuendelea, ila nimemwachia Mungu, naomba nikushauri kufuatilia jambo hilo na kama ukikuta ni kweli, fanya maamuzi kwa kuzingatia mazuri na mabaya ila kuishi na mtu ambaye ana mtoto na mbaya zaidi hakukwambia inauma sana
 
Kwnza pole sana, mimi mwenyewe mpaka hivi ninavyo andika Haya mahusiano yangu ni kama sijui kama yanaweza kuendelea, ila nimemwachia Mungu, naomba nikushauri kufuatilia jambo hilo na kama ukikuta ni kweli, fanya maamuzi kwa kuzingatia mazuri na mabaya ila kuishi na mtu ambaye ana mtoto na mbaya zaidi hakukwambia inauma sana

Kesi yko ikoje dadaaa
 
Pole sana kwa hili lililokupata, ni mitihani katika maisha.

Mimi napenda nikushauli mambo yafuatayo

1. Maamuzi ya Maisha yako unayo wewe.

2.Umekuwa katika mahusiano kwa miaka minne hajakuambia, hii inakufundisha Mambo makubwa mawili a) Mpenzi wako anakupenda sana hivyo alihisi angekuambia ungemwacha Siku hiyohiyo
b)Amekusaliti ametembea na MTU mwingine, hivyo dhambi ya usaliti inamtafuna hivyo hawezi kukuambia.

3.Wewe unaonekana kumpenda MTU ambaye hujui kama yeye anakupenda sana, ndo maana alikutishia kukuacha ulivyomuuliza, hana cha kupoteza hata asipokuwa na na wewe,


Mwisho keep in your mind that ur the architecture of ur life, sisi tunajaribu tu mengine utaamua mwenyewe.
 
Huyo bado hajui kwa nini hadithi nyingi za mama wa kambo hazipendezi. Msamehe bure ili wana wa damu yako wapite kwenye mikono ya dunia salama.
^^
 
ila mimi nakulaumu, ulitegemea jamaa angekua anapozea wapi kipindi chote hicho?, its your fault lady.
 
Dada unaonekanika una roho mbaya kwel...kwan kama mpezio alipata mtoto kabla ya mahusiano yenu tatizo liko wap..maana ake hajakusalit..alafu mtoto ni zawad mungu anakuzawadia!

my dear unanihukumu bure...wala sijasema nachukia huyo mtoto.Ila unapokua muwazi kwa mwenzanko af ye akakuficha inauma esp.ukizingatia huyo mtoto kazaliwa ndani ya mahusiano yetu.Kama mtu anaficha hili nadhani nexttym ataficha kinda zaidi ya hili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom