Natamani kuifunga jela mifupa yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kuifunga jela mifupa yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Apr 18, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake.

  Salaam ndugu zanguni wapendwa ndani ya jukwaa hili la JF, ni matumaini mpo na siha njema kabisa. Leo nami najikita kwenye jukwaa la ili. kwa machache ambayo yalikuwa yanapita kama taswira ya picha ya kutisha mbele ya macho yangu, kiasi yakwamba naogopa hata kulala, maana hilo jinamizi ninalo liona kila nikifumba macho linatisha kweli kweli.

  Wengi watashtuka na kichwa cha makala haya, “Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake.” Naam ni kweli kabisa ndugu zanguni, natamani kweli na si uongo, kwani leo nimekaa na kutafakari mengi sana, haswa enzi zile za “Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa...” Nakumbuka sana enzi zile ambazo ndio kwanza tumepata uhuru, enzi za matumaini mapya, enzi za kufurahia uhuru tulio upata toka kwa Mwingereza, aliyepewa dhamana ya kutuangalia mpaka pale tutapopata uwezo wa kujitawala, enzi za kujivunia utaifa wetu.

  Ni dhahiri kuwa usiku ule wa Desemba 9, 1961 wakati ilipokuwa inashushwa bendera ya Mwingereza na kupandishwa ile ya Tanganyika, wengi walitokwa na machozi ya furaha kila aliyeshuhudia alikuwa na yakini kuwa ule ulikuwa ndio mwanzo wa maendeleo ya nchi yetu Tanganyika.

  Maendeleo ambayo yangekuja kuonekana katika hali bora zaidi za kiuchumi kwa taifa na mtu mmoja mmoja, nyumba bora zaidi, kilimo cha kisasa zaidi, usafiri bora zaidi na juu ya hayo elimu bora zaidi na kwa wote.

  Kwa kweli matumaini yetu yalikuwa makubwa sana, kiasi ya kwamba wengi walikuwa wakitokwa na machozi ya furaha na matumaini. Matumaini ambayo leo hii yamekuwa ni ndoto za Ali Nacha. Wengi watashangaa hivi leo X-Paster anataka kusema nini, mbona hatumuelewi? Ni kweli kabisa unaweza usinielewe, kwa sasa ila kama utatafakari na kuchambua maisha ya Mtanzania tangia kupata uhuru mpaka leo hii, basi utashindwa kutambua, wapi tulipotoka na wapi tunaelekea na wapi tumesimama.

  Lahiti tungalijuwa kuwa Uhuru ule ungetuletea mashaka haya nina ukakika kabisa mashujaa wetu wasingetumia mali zao na muda wao kuondoa ubaguzi wa kikoloni na hata ingekuwa tumepewa uhuru bila ya harakati basi hakuna ambaye angesheherekea kama ilivyokuwa siku ile ya uhuru.

  Nakumbuka sana, baada ya uhuru mwaka 1961 viongozi wa nchi yetu tukufu walifanya mengi kwa nia ya kuendeleza nchi hii. Hapa kuna machache niliyoweza kuyakumbuka baadhi ya hayo ni kama ifuatavyo:

  1961 - Uhuru wa Tanganyika

  1962
  - Jamhuri ya Tanganyika

  1964
  - Muungano Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa nchi mpya iliyokuja kujulikana kwa jina la Tanzania

  1967 - Azimio la Arusha

  1971 - Madaraka mikoani

  1980’s - Vita dhidi ya wahujumu Uchumi

  Bila kusahau U.P.E, vijiji vya ujamaa, maduka ya kaya, elimu bure, kutaifisha majumba, mashamba n.k.

  Kwa wakati ule nyimbo nyingi zilitungwa kupongeza kila hatua iliyochukuliwa. Kwa bahati nzuri miaka yote ya sitini na sabini iliwashuhudia Watanzania chini ya utamaduni wa kuheshimu na kuthamini sana viongozi wao, hivyo moyo wa uzalendo ulijitokeza wazi wazi.

  Hali hii ilijitokeza hasa pale wananchi walivyozitii hata amri ambazo bila shaka hata serikali iliona tabu kuzitekeleza, mfano kuanzishwa vijiji vya ujamaa, kutaifisha majumba, mashule na mashamba ya katani, pamba n.k.

  Tuliambiwa na tukaamini kuwa Tanzania haiwezi kuwa huru hadi Afrika yote iwe huru. Serikali yetu tukufu ikiongozwa na fikra sahihi za mwenyekiti ilitumia kila uwezo uliokuwa nao kufikia lengo hili. FRELIMO, MPLA, ANC, SWAPO walifaidi sana msimamo wetu huu.

  Tuliambiwa Idd Amin ni nduli anayetumiwa na mabwana zake ili kuzorotesha harakati za ukombozi wa Afrika. Tulikubali hili watu walitoa mali na roho zao kuikomboa ardhi yetu na kumpa adhabu kidogo ndani ya mipaka ya nchi yake.

  Haya yalifanyika bila mtu yeyote kuhoji kwa vile wengi walidhani kufanya vile ni katika harakati zile zile za kutuletea maendeleo.

  Wazalendo wale ambao enzi zile walijulikana kama Makabwela, yaani watu wa kipato cha chini, leo hii tunajulikana kwa jina la Walala Hoi, na haswa wanaoishi mikoani wanaweza zaidi kuona kile ninacho kizungumza... Si ajabu uko mikoani na haswa ukitembea siku ya soko au gulio ukamwona dalali akiuza kitanda cha kamba... karne hii.

  Mimi bado najiuliza sababu ya huu umasikini ni nini haswa. Tulikuwa tunaambia kuwa ili nchi iendelee tunaitaji mambo manne, Ardhi, watu, siyasa safi na uongozi bora… Je hivi vyote kweli hatuna hata kimoja…!?

  Nasema tena kwa sauti kubwa kabisa , serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere haikuwa nzuri kwenye mipango ya uchumi, ni bora tungeendelea kutawaliwa na Mwingereza, kuliko serikali hii iliyo hasisiwa na Mwalimu Nyerere. Nadiriki kusema kuwa Wakoloni walikuwa bora kuliko Nyerere kwa mipango ya uchumi mizuri kwa ajili ya nchi hii. Hao wakoloni tulio waondoa ndio hao hao waliotuletea mazao mbali mbali ya kiuchumi, kama vile Pamba, Katani , Chai, Kahawa, Korosho na kadhaa wa kadhaa, na haya mazao yaliletwa ili kutegemeza uchumi wa nchi hii, na ni kweli waliona mbali, kwani mazao hayo mpaka leo hii ndio yanasaidia nchi yetu, lakini cha ajabu serikali iliua mashamba yote makubwa na hata hao wakulima wadogo wadogo wa mazao hayo, serikali haikuwajali.

  Kipindi cha utawala wa Nyerere kwa kweli ni kipindi ambacho serikali yake ishindwa kuendesha uchumi wa nchi. Hata pale alipo amua kuanzisha Azimio la Arusha kama njia ya kujikwamua kiuchumi, bado hatukuona nafuu yoyote ile kwa mlalahoi, au makabwela. Na Kwa bahati nzuri mtoto yule aliyejulikana kwa jina la Azimio la Arusha alimfia mikononi kabla hata mzazi wake hajafariki. Hata ile siyasa ya Ujamaa na kujitegemea aliyopanga na wachumi wake uchwara, nayo ikapata ugonjwa wa kifaduro. Nayo akaishuhudia ikimfia mikononi.

  Sera za ujamaa na kujitegemea kwa kweli hazikuwa sera nzuri hata kidogo. Na hata alipo ambiwa kuwa sera ni mbovu, badala ya kufuata ushauri wa kitaalam, yeye akatumia sura na maumbile yake akichanganya na uongozi wake na umahiri wa kuzungumza na kuvutia kuzitetea sera zake mbovu mpaka nchi ya Tanzania ikaangamia. Kusema kweli Mwalimu Nyerere alikuwa ni mahiri sana kwenye kutoa hotuba za kuvutia na zenye kuleta matumaini mazuri, maneno yake kwa kweli yalijaa ushawishi wa hali ya juu sana. Lakini ukija kwenye matendo ya zile hotuba nzuri hakuna hata kijiji kimoja cha maonyesho kuonyesha kuwa alifanikiwa kwenye sera zake. Hivi leo hakuna kijiji hata kimoja ambacho kinafahidika na sera zile za ujamaa na kujitegemea.

  Nakumbuka aliyekuwa rais wa Kenya enzi hizo (Jomo Kenyatta) aliwahi kumwambia wanahabari kuwa "kama unataka watendaji wazuri katika sekta ya mbalimbali njoo Kenya na kama unataka wahutubiaji wazuri kila eneo liwe la siyasa, uchumi, biashara, kilimo n.k basi kwenda Tanzania kamwambie Nyerere akupe anao tele”

  Ni kweli kwani ile siyasa ya ujamaa iliwaharibu sana viongozi wa taifa ili. Nyerere alitengeneza wahutubiaji wazuri si watendaji na wachapa kazi wazuri kwani karibia wote walipitia vyuo vya siyasa. Alipenda sana watu ambao kazi yao ni kuimba kwa nguvu hadi kufoka mate mdomoni kwa kusema "Zidumu fikra za mwenyekiti..." . Na wala sishangai maana hata leo na hata hao walio upande wa pili wenyewe wanajiita vyama vya upinzani wengi wanaiga tabia ya Nyerere ya kuwa wahutubiaji wazuri kuliko kuwa watendaji na wachapa kazi.

  Na kwa kawaida sehemu yoyote ile maendeleo hayawezi kuja hivi hivi, lazima yafanyiwe kazi ili yapatikane. Kazi hiyo haitegemewi kufanywa na mwingine yoyote isipokuwa watawala na watawaliwa (serikali na raia).

  Watawala ndio wenye jukumu la kupanga na kuratibu mipango na kutafuta njia za kusaidia utekelezaji wake ili watawaliwa waweze kufanya hayo ambayo yameshapangwa. lakini watawala wetu wale walikuwa kama wafalme, kazi yao ilikuwa kunyoosha vidole tu, bila kuonyesha mifano hai.

  Mpaka leo hakuna ambaye anaweza kutuambia, ni ugonjwa gani uliotupata Watanzania, baada ya kutaifisha mashirika na mashamba. Tulikuwa na mashirika mengi tulio yaita ya Umma kama vile Viwanda vya nguo vya Urafiki, Sunguratex, Mwatex na kule Musoma pia kulikuwa na kiwanda cha nguo, ila sina uhakika kama bado kipo, tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama, Tanganyika Packers, kiwanda cha viatu kule Morogoro, na kile cha dar, pia kulikuwa na RTC na Ugawaji na mengine mengi. Yote haya leo ni marehemu na makaburi yake yashafutika kwenye ulimwengu wa Mtanzania.

  Serikali yetu baada ya kutaifisha mashirika na makampuni na kukuta pesa nyingi kwenye hayo mashirika, wakaona bora kuanzisha vikundi vya sanaa vya mashirika ya umma. Vikundi ambavyo vilikuwa si vya uzalishaji mali, bali vilikuwa vinapata ruzuku kwa asilimia mia 100% kutoka kwenye hayo mashirika. Vikundi vingi kufikia mwishoni mwa miaka ya themanini 1980 vingi vilianza kudolola. Mashirika mengi yalianza kupungukiwa na uwezo wa kuviendesha vikundi hivyo kwa sababu nayo yalikuwa taabani kifedha.

  Huwa najiuliza wakati mwingine, ni vipi bidhaa kama Pamba, Katani au bidhaa kutoka kwenye mashamba au makampuni ulio dhurumu, yaani umuuzie yule yule uliye mnyang’anya, hivi inaingia akilini kweli!?

  Fikra zangu zika ambaa ambaa,mpaka zile enzi ambazo JKT walishirikiana sana na askari polisi kulinda viongozi na kukamata raiya, kisa wamemkuta na dawa ya meno au kipande cha sabuni ya mchubuo (tulikuwa tunaita sabuni ya pundamilia). Ukikamatwa na dozen moja ya sabuni ni muhujumu uchumi, hakuna ruhusa ya kuweka wakili wa kukutetea...!

  Nakumbuka ili kuangalia TV, mpaka kipindi cha sikukuu ya sabasaba kwenye banda la Yahaya Hussein, hii ni kwa wakazi wa jiji la DSM, Sijui uko mikoani hali ilikuwaje. Nakumbuka sana zile nyimbo za kina marehemu Mzee mzima Pepekale, Rechereau (tamka Rosherou) au Tabu Ley, Franco Luambo Makiadi Mzee wa o.k Jazz na wengine wengi.

  Zaidi ya hapo kila kitu kilikuwa kwa foleni, nchi nzima shule za sekondari za kuhesabika kwa vidole vya mkono. Chuo kikuu kimoja tu, kama kimejaa basi, subiri mwakani au ndio basi tena. Ilifikia wakati hata ukiwa na gari zuri basi wewe ni bepari kila kitu kwa kibali, ukiona gari aina ya Benz basi hiyo ni mali ya Ikulu, watu binafsi si rahisi kumiliki gari kama hiyo yaani hata kuvaa suti ni ubepari. Nakumbuka mwaka mmoja aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu salim Ahmed Salim, alikuwa Mtwara anahutubia wengi wa wale walio hudhuria walikuwa wamevaa majunia ya mbolea kama nguo.

  Baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi maiti akitegemea miujiza ya kufufuliwa, alisha sahau kuwa enzi za wafu kufufuliwa zilisha pita... Akasingizia kuwa anan’gatuka mapema. Kumbe alikuwa ameshindwa kuendesha uchumi wa taifa ili.

  Ndio maana leo hii kila nikikumbuka madhira ya utawala wake inanifanya nitamani kwamba mifupa yake ipelekwe gerezani. Kwani ni yeye aliyeasisi siyasa na sera mbovu dhidi ya taifa ili la Tanzania, na mpaka leo hatujainuka tena.
   
 2. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ni kufuru kufirikia kufunga jela mifupa ya Nyerere ambaye hata elimu ya bure aliweza kutoa. Leo hii wanafunzi wake wamegeuka kuwa mafisadi na tena wanatuambia elimu ya bure haiwezekani wakati inawezekana. Nitamuenzi Nyerere kwa hili la elimu kwa wote!
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Elimu ya bure hata wakoloni walitoa.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Wacha uongo wewe wakati wa mkoloni kulikuwa hakuna elimu bure.

   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hilo X-Paster niliwahi kusema. Ukweli Nyerere katawala nusu ya uhai wa nchi tokea Tanzania ipate uhuru. Kwenye makala yako, ungeendeleza miaka iliyofuata baada ya yeye kutokuwepo ndio ungekuwa na hoja ya msingi na hapo ndio ungekuwa fair. Miaka yake takribani 25 na hii 25 ya hawa jamaa watatu wapi ni nafuu. Ukilinganisha na hawa jamaa huenda ukabadilisha usemi wako na kutamani kumfufua aje atawale tena.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  big crap ever here in JF
   
 7. b

  bnhai JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hivi hoja inakuwa crap kwa sababu imetofautiana na mtazamo wako au haijakufurahisha. Km ni crap huhitaji kuandika neno CRAP just show using arguments hiyo CRAP.
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Absorutere....
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  :):):)
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  wewe unafikiri mwenzako mzima kweli?

   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Unataka kunambia wale wote waliosoma enzi za ukoloni walikuwa wanalipa, kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne, na kuendelea mpaka la nane!?

  Wewe wa wapi wewe!?
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hebu onyesha ugonjwa wake. Wengine wanapenda kufikiri na huamini kwenye fikra zao mpaka pale watakapoambiwa wanachofikiri si sahihi. Sasa kama wewe unamng'ang'ania kuwa anaumwa halafu humpi tiba (arguments), nani anayehesabika kuwa mgonjwa? Hoja haifukiwa na neno CRAP.
   
 13. A

  Albimany JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  WATANGANYIKA wengi walidanganywa na NYERERE,aliwaaminisha yakua amani ya nchi hile aliileta yeye, wakati hatukumbuki vita kabla ya kutawala yeye.

  Na jengine ni hilo la ELIMU nchi nyingi kama sio zote duniani elimu ya premary ni bure sasa sijui lipi litufanye tumuone nyerere ni wakipekee.

  Muungu amuongezee adhabu huko aliko(Amin)
   
 14. J

  John W. Mlacha Verified User

  #14
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  hakuna Mungu wa aina hi, hata usali hadi uso utoboke
   
 15. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  Ukishamchukia mtu hata siku moja huwezi ona jema hata siku moja, huoni hata hii lugha unayotumia kuwasiliana ni moja ya mafanikio ya mwalimu, Hayo mawazo yako unajitafutia laana tu na itawatafuna watu wote wenye mawazo kama ya kwako-Kama umesoma naona elimu yako haijakusaidia
   
 16. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Na wewe siku utakapoenda huko aliko utamkuta ndo anaandikisha wanaoingia sijuu utajiteteaje shame on you people.

   
 17. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mtoa hoja ana hasira na Baba wa taifa maana alivunja mfumo wa uchifu wakati babu yake alikuwa chifu so benefit zote za uchifu zilijivua gamba,aha aha...utajifunga mifupa yako mwenyewe aha aha!
   
 18. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  BURE KABISA!
  huyu ni kama jamaa yangu mmoja ambaye familia yao ya kifisadi iitaifishiwa mali enzi za nyerere, ye kila kitu kuhusu Nyerere anachukia tu!
  UPUMBAVU WAKE HAUFIKII HATA AKILI UA BABU YAKO!
   
 19. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Sielewi kama wewe sio moja wa wale wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati ule waliosema "afadhali serikali ya mkoloni" na mwalimu akashughulika nao kikamilifu.
   
 20. S

  Sirikali Member

  #20
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Nimekaa na waislamu wengine sana hapa Tanganyika na wale wa zenjbar, katika hoja zao juu ya mwalimu nimegundua wanachuki naye binafsi.
  Nasema mnachuki binafsi na mwalimu na kasumba yenu ya kibaguzi iliyojaa katika dini yenu ya kiibilisi.
  Marais watatu waliofuata baada ya mwalimu, wamelifanyia nini hili taifa zaidi ya kuliangamiza.?
  Mukikutana na mwinyi na jk mnawakenulia meno kwasababu ni waislamu wenzenu. Msidhani wakristu ni wajinga kiasi hicho, tunaona na kuwatazama tuu, siku ya siku ndio mtajua kwamba hamvumiliki.
  Angalia vita kubwa mlioipiga zidi ya mkapa, bado hamjachoka tuu.
  Mnaendelea vijembe zidi ya pinda.
  jk analifahamu hili vizuri na ndio maana hathubutu kuwayumbisha wakristu kwasababu anajua tutakachomfanya, lazima mjue hakuna anayewafagilia kwa akili zenu za kipuuzi.
  mnakenua meno na mwinyi wenu aliyetaka kuifanya tanzania nchi ya kiislamu, nyerere aliliona hilo na kumpiga vijembe hadharani.

  Nyerere atabaki kuwa Baba wa Taifa hili na tutamuheshimu milele yote.
  Nakwambieni hakuna atakayedondosha chozi hata mwinyi na jk watutoke leo kwa udini mnaouendeleza hapa nchini.
   
Loading...