Natamani 'Jamii' ingeijua sababu iliyosababisha nikafanya vile, Japo hadi leo nashindwa kuelewa kama nilikuwa sahihi au lah!

SEHEMU YA MWISHO.

Mawasiliano yangu na mpenzi wangu aliye shule hayakuwa ya mara kwa mara kwani yeye ndie alikuwa akinitafuta pindi anapokuwa amepata upenyo wa kutumia simu huko shuleni. Hivyo hata kipindi ambacho alianza kukata mawasiliano namimi sikuweza kugundua mapema kwani kila nilivyoona hanitafuti nilijua tu ni ubize wa huko shuleni kwao na pengine angenitafuta. Sikuwa na mawazo yooyote kama tayari ameanza kubadilika. Huku mjini maisha ya mtaani sasa baada ya kumaliza shule Jasmin alirusi kwao kinondoni namimi nikabaki nyumbani. Mawasiliano yalikuwa ya kila siku na mwisho wa siku tulipanga miadi na nikaweza kula tunda kiulainii. Ulaji wa tunda ilikuwa ni kama malipo yangu kwa kazi kubwa niliyokuwa nimeifanya. Narudia kusema tena kuwa mpaka mda huo nilikuwa sija fall in love na Jasmin. Alikuwa binti mrembo wa kiasi chake, mpole, mwenye upendo wa dhati kwangu lakini bado nilitamani mda wowote aniache niendelee na maisha yangu. Nilitamani sana mabaharia wampitie ili anisahau lakini haikuwa hivyo. Tuliendelea kuwasiliana na kuongea mambo mengi sana kkuhusu kesho yetu. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwanini sasa nilikuwa nataka kumuacha binti wa watu, jibu ni kuwa, tayari nilikuwa na mtu wangu ninaempenda kwa dhati. Ningeendelea kuwa na Jasmin ila niliogopa kuwa kadri nilivyozidi kuwa nae ndivyo nilivyozidi kumuanisha na kumzamisha kabisa. Sasa kwanini niendelee kuwa nae wakati sina malengo nae?. Sikutaka kumpotezea mda wake na nilitaka kama kuumia aumie leo mapema atazoea kuliko kuja kuumia keshokutwa. Sikupenda awachukie wanaume kwa kiasi hicho ukizingatia kuwa alishawahi niambia kuwa yule jamaa aliyemtesa enzi zile shule ndie aliyekuwa first lover wake na ndie aliyeivunja bikara yake. Sasa jaribu kufikiria, bwana wake wa kwanza tu kwenye mapenzi kamtesa vile, namimi wa pili nimepanga kumtema. Kiukweli nilimhurumia na nilipanga kumtema taratibu mwendo wa kung'ata na kupuliza.

Jasmin kwao alikuwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa na alikuwa na urafiki wa karibu sana na dada yake aliyezaliwa kabla yake. Hakumficha kitu na tayari alikuwa amemueleza kuhusu mimi kama kijana mwenye busara na ndie mtu wake. Dada mtu alifahamu kuhusu mimi ila hatukuwahi kuonana zaidi ya kuongea kwa simu. Sasa tayari nilikuwa najuliakana ukweni. Baada ya kufikiria sana na kugundua kuwa sipaswi kumuacha ghafla huyu binti, nilianza kumuacha taratibu. Simpigii simu, simtafuti na akinitafuta sipokei simu na msg sijibu kwa wakati, hata nikijibu inakuwa kwa ufupi. Kwakuwa sikuwa nimemzoesha vile ilikuwa rahisi kwake kugundua kuwa Fohadi amebadilika. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndio nilizidisha kipimo cha kubadilika. Jasmin sasa akawa ni mtu wa kulalamika na kulialia kila siku, sikujali na nilishaamua kumove on. Mpaka muda huo tayari nilikuwa chuo mwaka wa kwanza na Jasmin nae alikuwa chuo. Vyuo viwili tofauti ndani ya mji mmoja..aiseeee, Jasmin alikuwa hakwepeki. Alikuwa anatamani aje chuoni kwetu siku yoyote kunitembelea lakini nilimwambia asije hadi pale nitakapomuita mimi, na kama angekuja bila taarifa labda kupitia marafiki zangu wa shuleni niliokuwa nao pale chuo nilimwambia wakimleta hostel kwangu mimi nitamuacha nao maana amekuja bila taarifa. Jasmin alikuwa ni mtu wa kulia, kuugua na kuhangaika kila siku. Ikafikia kipindi nikazoea kilio chake na nikawa mtu wa kutojali. Kwakwua dada yake alikuwa anajua kila kitu, alikuwa akinipigia mara kwa mara kuniomba nisimfanyie vile mdogo wake kwani hadi mama yao mzazi japo walimficha kuhusu sababu ya matatizo ya Jasmin alikuwa anaumia kuona Kitinda mimba wake hana furaha.

Pamoja na mateso yote Jasmin hakuchoka kunambia vile ananipenda na atapambania penzi letu. Aliwalaumu sana wadada wa chuo ambao pengine alihisi wamenibadilisha. Alinikumbusha mambo mengi mema mazuri tuliyofanyiana na kuniomba nisimtese kama bwana wake wa zamani. Sikumuelewa na wala sikujal, niliendelea kufanya yangu bila kujali maumivu yale. Mpaka muda huu Jasmin hakujua kama kipindi nakutana nae nilikuwa na mtu wangu moyoni. Kuna kipindi alikuwa anapiga simu kuhitaji penzi ila nilimzingua na nilimwambia niko busy na masomo. Kiukweli nilimfanyia mambo ya ovyo sana. Nakumbuka siku moja wakati wa mkesha wa mwaka mpya, jasmin ni wale watu wa kaskazini ambao wana desturi ya kurudi mkoani kwao kwajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Jasmin aliniomba niende kwa dada yake maana amebaki peke yake ndugu zake wote katika familia wameenda mkoani kwajili ya sikukuu, Jasmin alibaki kwajili ya ratiba ya chuoni kwao. Nilikubali na nikaenda kule kwa dada yake ambako alibaki kulinda nyumba ya dada yake. Hii ni moja ya siku niliyofanya kitu cha kipuuzi, kulala kwenye kitanda cha dada yake na je ingekuwaje kama dada mtu au ndugu yao mwingine angekuja akanikuta mule ndani, hahahaah nilifanya uboya sana, tuachane na hii story. Sasa nilivyoenda kweli nilimkuta Jasmin ameandaa chakula, tulikula na tukalala. Sasa wakati nimelala, simu yangu haikuwa na password kwahiyo Jasmin aliichukua na kukagua kila kitu na kukuta chats za madem kibao akiwemo yule demu wangu aliye shuleni. Hii siku huwa siisahau hadi leo maana kwa jinsi chatts zilivyokuwa na kwa jinsi alivyokuwa anaumia Jasmin na ule muda nimelala sina habari, angeweza hata kunichoma kisu kwa hasira. Lakini niliamka salama siku hiyo ya mwaka mpya na wala hakuonesha hali ya utofauti. Hakuniulizachochote hadi wakati ananisindikiza kituoni ndio akaniuliza yue ni nani na yule ni nani. Japokuwa nilipanga kumuacha Jasmin ila kitendo cha kumuona live katika hali ile kilinifanya niumie sana. Nilimpa uongo mwingi na akanipa hukumu ya kufuta zile namba zao mbele yake. Nilifuta na kitu ambacho sikujua ni kuwa kumbe zile namba zlizikopi sehemu na akabaki nazo. Nilifuta namba zote kabisa ikiwemo ya mpenzi wangu wa shule. Baadae nilivyoacahana nae pale kituoni niliisave upya namba ya mpenzi wangu wa shuleni maana nilikuwa nimeikariri. Sijui hata kama alikula vizuri sikukuuu kwakweli.

Badae Jasmin alianza kuwatafuta wale wadada (walikuwa 3, mpenzi wangu na videmu vingine viwili). Binafsi, mademu huwa siwambii jina langu la ukweli. Huyu atajua naitwa James, huyu atajua naitwa Jamal n.k. Mtu pekee aliyekuwa anajua jina langu ni mpenzi wangu Orginal. Baaada ya kuwatafuta wale wadada, wawili walisema hawamjui Fohadi kasoro yule mmoja ndie alisema ananijua Fohadi na yeye ni mpenzi wa Fohadi. Sasa hapo wakawa wamekutana Jasmin na mpenzi wangu. Alichofanya Jasmin ni kumwambia mpenzi wangu aniache, japokuwa mpenzi wangu ndiye alikuwa wa kwanza kuwa namimi hapo tumefikisha miaka 3 tayari ila Jasmin alimwambia aniache tu na alikuwa tayari kumpa zawadi yoyote ili aniache. Badae nimerudi getto chuo nimechoka, mara naona simu inaita na namba ya mpenz wangu ndio ipo kwenye screen. Kumbuka nilikuwa sijawasiliana nae muda mrefu maaana sikujua kama amenichunia so nilijiona bado niko salama kwake, kumbe maskini ya mtoto wa watu alikuwa anafanya utafiti juu yangu na sasa utafiti umejifanya wenyewe. Mpenzi wangu alilalamika sana, kwanini namfanyia vile kumbe ndio maana kwenye graduation nilimkwepa na kule tuition center nilimuongopea niko site kumbe nipo na Jasmin. Alilia sana sana na nilipomuuliza amejuaje akanambia Jasmin amemtafuta. Aiseee, mapenzi mabaya, Nilimpigia simu Jasmin na nikamlaumu sana sa kwa kumtafuta mpenzi wangu. Niliongea mambo mabaya kwa Jasmin kiasi kwamba akawa analia zaidi. Sikujali na sikukuu yangu ya Mwaka mpya ikawa imeingia misukosuko. Ninachoshukuru kuhusu Jasmin hadi leo ni kuwa hakuwa mtu wa kuchukua maamuzi magumu pengine angeweza ata kujifanyia kitu kibaya na nikaingia matatizoni. Sasa hapo sehemu zote mbili zikawa zinawaka moto.

Baada ya hapo nilipoteza mawasiliano na Mpenzi wangu ila bado Jasmin alizidi kunitafuta huku analia. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini niliwahi kumpa furaha tena. Dada yake aliporudi kutoka mkoani alikuta hali tofauti kwa mdogo wake na hapo nae uchungu ukamwingia akaanza kunitafuta ananitukana na kunigombeza kwa kumtenda mdogo wake na akasema chochote kibaya kikitokea kwa mdogo wake mimi nitakuwa mhusika wa kwanza. Nilihisi dalili za kupigwa kipapai siku za usoni hahahahaha. Nilidata kiukweli. Nilivyofanya sasa kwakuwa nilijua Jasmin angepata faraja kwa neno moja kutoka kwangu, nilimtext nikamwandikia I love you. Baada ya ile msg niliona calls kibao za Jasmin niliongea nae akasmile na pale nikajua nimemuokoa na huenda hali yake ikawa poa japo alikuwa amedhoofu sana. Wakuu niliogopa kupigwa kipapai. Sasa mtihani ukawa kujua mpenzi wangu anendeleaje, siwezi kumpigia simu kujua anendeleaje maana ni dent na anaishi na wazazi, sikuwa tayari kwa mikwaju 30. Sasa nikawa naishi kwa hofu sijui nini kinaendelea kwa mpenzi wangu na hakunitafuta tena. Basi nikawa mtu wa kuishi bila kujiamini, kila nikikutana na watu siwajui nahisi labda ni ndugu wa mpenzi wangu wananitafuta wanidake pengine kuna chochote kibaya kimetokea hahahahaha. Nilikuwa mtu wa mawazo kila mara. Sasa Jasmin hakutaka kudeal namimi tena, alichofannya ni kudeal na mpenzi wangu, kuongea nae, kumtafuta kwa simu ili kumuomba aachane namimi. Jasmin ni wale wadada wenye huruma sana..a wife material in deed. waliendelea kuwasiliana bila mimi kujua na uzuri ni kuwa kati yao hakukuwa na mkorofi wa kumtukana mwenzie. So waliendelea kuyamaliza kidplomasia.

Kuna kitu kimoja kilitokea hadi nikahisi naota. Kumbe katika harakati za masomo ya Olevel miaka ya nyuma sana, Jasmin aliwahi kufahamiana na kaka wa mpenzi wangu kupitia tuition center moja maarufu pale mwenge. Enzi hizo jasmin anasoma O level Moshi na Huyu jamaa alikuwa anasoma bagamoyo sasa walifahamiana wakawa marafiki wakati wa likizo tuition pale. Kipindi hicho wanafahamiana mimi na mpenzi wangu hatukuwahi hata kujuana. It was a long time before. Sasa, siku moja katika pitapita zake maeneo ya mjini ata sijui ni wapi, jasmin alikutana na kaka wa mpenzi wangu na walikuwa hawajaonana mda mrefu. Sasa katika story zao yule jamaa alimuuliza Jasmin vip mbona amedhoofu kiasi kile na hana furaha, Jasmin wa watu akaficha ficha mwisho akafunguka ni mapenzi tu. Mapenzi? yule jamaa akawa anamhusia aachane na huyo anaemtesa na Jasmin akasema hawezi kumuacha kwani ni mtu anaempenda kwa dhati. Sasa Jamaa akatamani kumjua huyo mtu anaependwa kiasi hicho, kuoneshwa picha akakutana na sura yangu akashituka akasema yaani unahangaika kisa hiki kijamaa?..Jasmin akasema namjua na huyu kijana mhuni mhuni tu na pia anamtesa mdogo wangu. Mdogo wako yupi?, jasmin akauliza jamaa akataja jina la mpenzi wangu na ndo hapo Jasmin akathibisha kuwa yule jamaa ni kaka wa mpenzi wangu. Binafsi, nilikuwa namfahamu kwa sura kaka wa mpenzi wangu nayeye alikuwa ananijua kwa sura. Kuna kipindi fulani mpenzi wangu aliniombaga nimsindikize kwa ndugu yake mmoja hivi, kweli tulienda kama marafiki wa shule na wala haikuwa tatizo kwa yule ndugu pale. Wakati nimekaa pale mara gafla na huyu kaka yake mpenzi wangu akaja. Alinikuta pale tukasalimiana ila hatukupiga story zozote japo tulikaa pamoja pale zaidi ya masaa 4. Wakati naondoka pale mpenzi wangu alinisindikiza, nikamuacha pale yule kaka mtu. Sijui alihisi nini kati yangu na mdogo wake ila nahisi alihisi kitu japo hakuwahi kufatilia na hata nilivyomuuliza mpenzi wangu alisema kaka yake hakumuulizaga chochote kuhusu mimi. So tunafahamiana japo hakuwahi kunijua jina ila mimi nilikuwa namfahamu jina. Hapa ndipo utata lizidi kuongezeka.

Sasa baada ya pale Jasmin alikuw na furaha sana, alijua njia rahisi ya kunitenganisha mimi na mpenzi wangu ni kupitia kaka yake. Mimi sjui hili wala lile kumbe kaka mtu alirudi nyumbani (ilikuwa bado ni wakati wa likizo ya mpenzi wangu), akampiga mdogo wake na kumuomba aachane namimi mhuni, malaya ninaemtesa pia Jasmin kabla hajawambia wazazi na akahidi kunitafuta ila 'anioneshe'. Wakati huo mimi sijui hili wala lile, kumbe natafutwa na Jasmin anafahamiana na kaka wa mpenzi wangu. Gafla nikapigiwa simu na mpenzi wangu akanisimulia kila kitu na kuzidi kuumia kwa yote yanayotokea. Nilimuomba msamaha lakini wapiiii, alikuwa ameumia sana na hakutaka tena kunielewa kwa chochote na alikuwa ameamua kunipotezea. Kwahiyo simu yake ilikuwa ni kuniambia kuwa ananiacha nibaki na Jasmin na nisimtafute tena maana mimi mhuni, malaya nina maduu wenglikizo inakaribia kuisha, simu ikakatwa na hapo . Hakuna siku niliyoumia na kupagawa kama hiyo (mapenzi yanauma sana aisee), nikachukua simu nikamtafuta Jasmin nikamuuliza kila kitu na nikamwambia kilichotokea kati yangu na mpenzi wangu na ndipo kwa hasira nikamwambia ukweli kuwa sikuwa nampenda na nilikubali kuwa nae ili tu amalize vizuri shule tu ajiunge chuo. Ulikuwa ni ukweli mchungu kwa Jasmin, nilidhani natibu kumbe naharibu. neno sikupendi lilikuwa ni zito sana kwa jasmin kulisikia kutoka kwangu. Sikujali kilio chake nikamwambia, nimempoteza mpenzi wangu kwajili yake sasa nayeye inabidi aendelee kufanya yake aachane namimi then nikakata simu. Ndani ya siku moja wote watatu tukawa tumeumia. Niliumia sana sana sana, Jasmin alipiga simu mara kibao sikupokea na msg sikujibu, hadi badae ilikuja namba ngeni kupokea kumbe ni dada yake akanitukana sana, akanimind sana na akaniambia kuwa niachane na mdogo wake maana mimi sina shukurani, sipendeki na sina roho ya ubinadamu. Akanionya nisithubutu tena kumtafuta mdogo wake na niendelee na maisha yangu. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisaaa.

Katika kuhangaika kumtafuta mpenzi wangu, siku moja simu yake nilipiga ikaita, ikapokelewa na sauti ya kiume. Nilishituka badae nikajua ni kaka yake. Bahati nzuri mpenzi wangu alikuwa amefuta namba yangu kwahiyo yule jamaa hakushituka chochote namimi nikazuga nilivyojua nikakata simu. Sikujaribu kuipiga tena ile simu na hapo connection yangu na mpenzi wangu ikawa imekatika. Mapenzi upofu, Jasmin aliendelea kunitafuta na kunitaka nimsamehe kwa makosa aliyonifanyia (Maskini, ilibidi aombe msamaha wakati mimi ndio mkosaji). Aliendelea kunitafuta akilia na muda huu hakuwa akimshirikisha dada yake tena maana nahisi angepigwa maana alishaonywa. Hivyo hakuwa na uwezo tena wa kulia au kuugua mbele ya ndugu zake maana wameshamuonya kuhusu mimi. Kwahiyo, alikuwa akilia na kujinyamazisha mwenyewe. Mimi huku ndo sijui ata mpenzi wangu nitampata vipi na yupo shule. Miezi ilienda ndipo siku 1 nikapokea msg kutoka kwa Jasmin, Ilikuwa ni mwezi wa 10 nipo likizo ndefu ya chuo. Aliniandikia maneno mengi ya kuumiza ila dhumuni kubwa lilikuwa ni kuniambia kuwa AMECHOKA na AMEKUBALI kuniacha niishi maisha yangu. Mwishoni pia aliandika neno moja lililonopa faraja kuwa "Fohadi, nakushukuru sana kwa kunivusha kipindi cha masomo, nimekusamehe kila kitu". Huo ndio ulikuwa mwisho wangu na Jasmin, Binti aliyenipenda kupita kiasi hatimae alikuwa ameamua kukaa pembeni kuepusha msongamano. Kama maumivu ameyapata ya kutosha na sasa alitaka kupona na kuendelea na maisha yake. Sikuijibu ile msg ila moyoni nilifurahi angalau msamaha wake utaniepusha na malipo ya hapa duniani. Na kubwa zaidi naachana ane akiwa mzima wa afya kasoro mwili tu ambao utarudi.

Baada ya wiki tatu nilimpigia simu Jasmin na kumwambia kuhusu kuupata ujumbe wake. Hapa sasa bila hasira na shida yoyote niliamua kumuelezea kila kitu kuhusu nilikotoka na mpenzi wangu na kwanini nilikubali kuwa nae kimahusiano pale sekondari. Nilimuomba msamaha kwa unyama niliomfanyia na nikamtakia kila la heri kwenye safari ya maisha yake. Alilia sana na kunishukuru kwa kumfanya kupata cheti cha elimu ya sekondari na kuingia chuo. Alinisamehe kwa moyo mmoja na akasikitika sana kuwa laiti angejua kuwa nilikuwa kwenye uhusiano toka siku ya kwanza asinge lazimisha kuni approach maana hapendi kuingilia mahusiano ya watu. Alinitakiwa maisha mema na mpenzi wangu lakini nikamwambia kuwa sipo nae tena maana kaka yake baada ya kujua kila kitu amesababisha tukaachana. Jasmin alijutia sana na akaniomba radhi lakini nilikataa msamahan wake kwani mimi ndio nilipaswa kumuomba radhi. Tuliachana kwa amani tukawa marafiki. Huku kwa mpenzi wangu alikuwa tayari amemaliza elimu ya sekondari na sasa alikuwa anajiandaa kwenda chuo kimoja pale jijini dodoma. Mimi nikiwa naenda kuingia waka wa pili yeye alikuwa anenda kuanza first year.

Siku moja nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu, baada ya mda mrefu sasa alinipigia simu kunisalimia. Tuliongea mengi sana na akasema alinichukia sana kwa kunitenda na leo amenipigia simu baada ya Jasmin kumtafuta na kuniombea msamaha. Yaani jasmin alimtafuta mpenzi wangu na kuniombea msamaha na kumwambia kuwa ametuacha tuwe wote. Alimsimulia kila kitu mpenzi wangu kuhusu sababu iliyonifanya nikamsaliti na kuwa nae. Mpenzi wangu alielewa ndipo akakubali kunitafuta japo anisalimie. Sasa Jasmin na mpenzi wangu wakawa marafiki na wakawa wanashauriana mambo mengi sana. Nilifurahi kwa swala hilo. Bahati mbaya kwangu ni kuwa mpenzi wangu tayari alikuwa ameamua kuendelea namaisha yake na tayari alikuwa na mtu wake mpya. Nilipambana sana kumrudisha katika himaya lakini wapiiiii. It was too late na tayari nilikuwa nimempoteza mpenzi wangu. Kati ya jasmin na mpenzi wangu sielewi nani alinipenda zaidi maana walichotofautiana tu ni material things, Jasmin alikuwa na uwezo mkubwa kifedha. Ila wote walinipenda kwa dhati sana sana sana sana japo moyoni hadi leo nampenda sana mpenzi wangu kuliko Jasmin. Katika historia yangu ya mahusiano sijwahi kupata mwanamke aliyenipenda kwa dhati kama wale. Nilibahatika kupata upendo wa dhati, nasema tena wa dhati ila niliupoteza. Niliumia sana kuhusu mpenzi wangu lakini hakuna kitu ningeweza kufanya kubadili uhalisia. Nilitumia nguvu kubwa sana kurudisha pendo la mpenzi wangu lakini haikuwezekana. Baada ya kuona ngumu ikabidi nirudi kwa Jasmin kwani niliamini ananipenda na angeweza kunipa nafasi kwakuwa sasa nilikuwa huru na single boy. Sikuwa na bahati Jasmin tayari alikuwa ameamua kunisahau japo alinipenda lakini hakutaka kuingia kwenye migogoro na ndugu zake kwa kunirudia. Niliwakosa wote na nimeamini mwanamke akikupenda kwa dhati yupo tayari kuvumilia kila kitu, ila akisema NO aiseeeee ni NO kweli kweli...Huwa hawarudishi moyo nyuma wale aiseeee. Walinipenda kwa dhati japokuwa sikuwa na kitu. Wema wangu kwa Jasmin uliniponza nikapoteza penzi la mpenzi wangu. Ninachoshukuru sasa kila mtu alinisamehe na kunielewa na kunitakia kila laheri. SIpendi kuacha vinyongo kwa mwanamke. Sasa hivi hatuwasiliani sana ila kila mtu yuko na serious relationship yake kasoro mimi hapa ambae nahangaika kumpata wa kujenga nae maisha.

HITIMISHO:

Historia yangu imejaa mambo mengi sana lakini mwishoni nilikosa wote. Wanawake wenye upendo ww kweli wapo, ukimpata akupendae mthamini na mtunze maana siku ukimpoteza ndio utajua umuhimu wake. Mpaka sasa hivi sina serious relatinship na nimekuwa nakutana na vimbwenga vya kila aina kwenye mahusiano. Nahisi karma inanitafuna. Na siku zote nikipataga nafasi ya kuongea nao huwa nawakumbusha kuhusu kunisamehe kwa dhati ili watoe vinyongo vyao vyote. Na wote wamesema wamenisamehe japo niliwaumiza na sasa wana furaha.

Mpaka sasa sijui kama nilikuwa sahihi au kuna sehemu nilifanya uamuzi wa makosa katika story yangu. Pengine mwana JF unaweza kuniambia ni wapi ambapo nilifeli. Chanzo cha yote haya ni Jasmin, lakini je, Nilikosea kuwa nae katika mahusiano?, je ningemuacha apotee kiafya na kielimu wakati nilikuwa nauwezo wa kumsaidia?, Je nilikosea kutompa nafasi Jasmin ndani ya moyo wangu au labda nimekosea wapi. Huwa sielewi kama nilikuwa sahihi au la. Kun amuda najutia ila kuna mda nafarijika kuona Jasmin 'niliyemuokoa' yupo na furaha na anaendelea vizuri kiuchumi na kuleta tabasamu kwa ndugu zake...

Pamoja na yote, tatizo kubwa ni 'jamii' nikimaanisha ndugu wa jasmin na marafiki zake ambao walikuwa wananijua na kujua uhusiano wetu hadi leo wananiona mwanaume katili sana kwa kumfanyia vile ndugu na rafiki yao. Bahati mbaya hawajui chocote kilicho nyuma ya pazia japo huwa natamani wangejua japo robo tu maamuzi yangu na hii story pengine wangenipunguzia hukumu katika mioyo yao. Na bahati mbaya hawatakuja kuujua ukweli wangu wote. Kuna muda nahisi pengine vinyongo vyao ndio vinanihukumu katika mahusiano mbalimbali. Lakini sina jinsi naishia kutamani wangejua. Pengine kama wapo hapa JF wanaweza unganisha dots na kunipunguzia adhabu kwa sababu naamini I played a fair game. Sikuwa tayari kumpoteza mpenzi wangu kisa Jasmini.

Kwako mwana JF, heshimu hisia za mwenza wako awe ni ME au KE. Kuna siku utatamani urudishe masaa nyuma ili u-win trust yake lakin itakuwa sio rahisi. Hamna kitu kibaya kama kumwaga machozi au kumpa maumivu mtu anaekupenda kwa dhati. Hiki nimejifunza na huenda kwa vyovyote vile my future wife afaidika kutokana na funzo nililopata kwenye mahusiano yangu ya awali. Ila nitampata lini huyo future wife?, yuko wapi?, atanipenda kwa dhati?..Mmi sijui. Na je ni lini Jamii itanisamehe na kunipunguzia vinyongo na lawama ambazo nimechoka kuzisikia kwa kitu ambacho nilifanya kwa faida ya Jasmin?..Mimi sijui nachojua nikuwa nilimpoteza mpenzi wangu na kwasasa napambana na hali yangu iliyojaaa upweke. Upweke wangu ni kukosa kupata mwanamke sahihi wa kujenga nae maisha..I wish and I hope nitampata as long as nishajutia kosa langu, wahanga wamenisamehe..Kuweni makini na hisia za wenzi wenu pamoja na maamuzi yenu katika mahusiano.

Poleni kwa story ndefu. God bless you all.

NB: This is a true story about me...Focus Hardwork Discpline...FOHADI.

Obligado.

Kwa hii story mimi ninaamini atarudi ondoa shaka

Unachotakiwa kukifanya hakikisha mawasiliano yenu ya awali yasikatike na hakikisha usizungumzie lolote kuhusu mapenzi, pia endapo itatokea jaribu kukusisitiza uko single na hauhitaji kuzungumzia neno mapenzi

Binadamu tumeumbiwa kusahihisha pale tulipokosea na kama wampenda kweli atarudi....

Chukua hiyo

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA TATU.

Tuendelee......

Simu ya mpenzi wangu ilinivuruga kabisa, furaha yote ya likizo iliyeyuka na nikajiona kama nisipochanga karata zangu vizuri naweza kuwapoteza wote wawili. Kumpoteza mpenzi wangu wa kwanza kilikuwa ni kitu ambacho nilikuwa sipo tayari kukiona kikitokea kutokana na heshima yangu kwake. Ila Kumpoteza Jasmin ilikuwa sawa lakini ndo kwanza ameanza kugain focus ya masomo na furaha imemrudia, je itakuaje sasa kama akijua mimi ni mbabaishaji mapema hivi. Japo Jasmin nilikuwa sina future nae ila isingekuwa rahisi kumpoteza mapema kabla sijagonga mhuri (kula tunda)..Najua hapa mabaharia watanisapoti hahahahahaha....Kwa akili ya haraka nilikuwa nishaamua kumuweka benchi mpenzi wangu wa zamani ili nizidi kuwa karibu na Jasmin lengo likiwa ni kumrudishia furaha yake ili amalize salama shule..Kwahiyo nilichofanya nilimkubalia mpenzi wangu pale pale kuwa tutaonana eneo la tuition maana kama ningemkatalia kwa simu angeshituka na angejihisi vibaya. Lengo langu ilikuwa ni kuja kumtafuta tena jumapili na kumpa excuse ya kutoonana.

Kuanzia jumamosi nilikuwa nawaza namna ya kumkwepa mpenzi wangu. Baada ya kuwaza sana nikafikia hitimisho la kumwambia mpenzi wangu kuwa sitakuwepo tena tuition pale maana kwa hizi wiki mbili inabidi niwe kwa uncle wangu mmoja maeneo ya kijichi nikisimamia ujenzi wa nyumba yake. Ulikuwa ni uongo ambao nilimwambia mpenzi wangu nayeye kwa moyo mmoja akawa amenikubalia na akasema atamiss kampani yangu pale tuition. Kuhusu mawasiliano nilimwambia asijisikie vibaya akiwa anapiga simu au msg hazijibiwi maana kazi ya site itakuwa na ubize mwingi na suluhisho pekee ni kuwasiliana nyakati za usiku. Hakuwa na shida nikawa nimesolve upande mmoja na nikamjulisha Jasmin kuwa inabidi tubadili tuitiion center, akaniuliza kwanini nikamwambia ile tuition center watu wamenizoea sana na wengine tunasoma nao shule sasa story zitakuwa nyingi pamoja na discussion kiasi kwamba tutakosa ata mda wa kufundisaha na kuwa pamoja.. Jasmin hakuwa na hiyana, alichotaka ni kampani yangu namimi sikutaka kumuangusha. Jumatatu ilipofika mimi na Jasmin tulikutana center nyingine ambako niliamini isingekuwa rahisi mpenzi wangu kuja.

Kiukweli nilifanya kumuumiza mpenzi wangu kwajili ya Jasmin, nikiwa na Jasmin simu yangu ilikuwa silent mda wote ila missed calls na msg kutoka kwa mpenzi wangu hazikukoma namimi sikumuangusha kila ilipofika jioni nilikuwa nazijibu na kusingizia uchovu wa shughuli za ujenzi. Likizo ile nilienjoy sana na Jasmin binti amabe kwao kidogo walikuwa safi kwahiyo ilikuwa ni kuenjoy na kufurahi maisha. Tulisoma, tulifurahi na likizo ikaisha na wala sikuwa na papala na tunda, likizo nzima sikugusia wala kuomba tunda ingawa naamini ningekula kiulaini tu. Baada ya kurudi shule penzi lilipamba moto, tayari Jasmin alikuwa ameamini mimi ni mwanaume sahihi kwake kwani hata nje ya shule sikuwa na makoloni. Kwahiyo ilikuwa ni furaha na mapambano ya masomo kitu amabcho hata mimi ndio kilikuwa lengo langu. Nikiri kabisa, pamoja na yote aliyonifanyia Jasmin mpaka muda huu, nilikuwa bado sijampenda na wala hakuuteka moyo wangu ili apate nnafasi ya kudumu. Moyo wangu ulimchagua Mpenzi wangu yule wa kwanza, japo hakuwa vizuri kifedha kama Jasmin lakini mapenzi ni upofu, alinipenda, nilimpenda na nilijiapiza kuendelea kumpenda.

Maandalizi yangu ya pre-necta yalipambwa na kadi moja yenye maneno matamu iliyofungwa kwenye bahasha ya kuvutia kutoka kwa Jasmin. Hakika alinipenda na nilizidi kupretend kwa kiwango cha SGR. Lait Kama angenikuta nikiwa single, ningezama mazima lakini sasa tayari nilikuwa occupied. Tulifanay pre-necta matokeo yakaja perfomance yake imeongezeka. Nilipata pongezi nyingi kutoka kwa rafik wa Jasmin ambao walinipongeza kwa kumpa furaha rafiki yao. Changamoto kubwa ilikuja wakati wa graduation, Mpenzi wangu alikuwa anaijua siku ya gradu na alikuwa tayari kutengeneza mazingira ya kuja kuhudhuria lakini mimi nilimkataza asije. Alilalamika sana kwanini asije wakati ni siku ambayo tuliwahi ipania siku za nyuma. Kosa kubwa la kiufundi nililolifanya ni kutofikiria vizuri jinsi ya kumshawishi asije hadi nikajikuta nimeropoka 'Sitafanya gradu'. Kweli aliamini kuwa sitafanya gradu na akawa ameelewa. Huku shule maandalizi ya gradu yaliendelea na wanafunzi wa combination tofauti walikuwa wakitengeneza tshirts zao za mahafari. Mimi na Jasmin tulichapisha tishirt zetu mbili unique, moja ya pink kwajili yake na nyingine nyeusi kwajili yangu. Siku ikawadia na hakika tulifurahi kupita maelezo. Pamoja na furaha yote ile, lakini bado moyoni niliumia kwa mpenzi wangu kutokuwepo pale. Ni siku aliyoisubiri kwa hamu lakini wema wangu kwa Jasmin ulikuwa ni mateso makubwa kwa Mpenzi wangu.

Nakumbuka kipindi hicho cha jakaya ndio kipindi ambacho facebook ilikuwa inatawala. Na kama ilivyo kawaida wakati wa gradu kuna kupiga picha za ukumbusho na ndugu jamaa na marafiki na huwezi wapangia matumizi ya zile picha. Picha zilipostiwa huko mitandaoni na ndiko hukohuko mpenzi wangu alipoona picha zangu nimeshiriki gradu. Hazikuwa picha mbaya labda nipo na Jasmin hapaana ila ubaya wke ilikuwa ni picha zinanionesha nipo kwenye gradu na wakati nilisema sifanyi. Taa nyekundu iliwaka katika kichwa cha mpenzi wangu na pengine nahisi alijaribu tena kufikiria upya sababu za mimi kutoonekana tuition centre kipindi kile. Conclusion yake alihisi kuwa kuna kitu namficha. Inawezekana nina mpenzi mpya au nimemchoka. Hakuwa na uhakika na sasa aliamua kufatilia kwa undani na ingekkuwa rahisi kugundua ukweli wote maana anawajua baadhi ya rafiki zangu au wengine angewapata facebook kupitia zile picha na tags. Wakati mimi sijui chochote kinachoendelea, kumbe mpenzi wangu ameingia field kufanya research kuhusu mimi ili kutest hypothesis au assumptions zake.

Huku shule tulianza mitihani na wiki ya kwanza ya mwezi wa 5 tukawa tumemaliza mitihani yetu. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwangu kwani nilikuwa nimeshiriki kwa kiwango kikubwa katika kuiokoa future ya Jasmin. Na hapa ndipo ilikuwa mwisho wa mkataba wangu wa kimapenzi na Jasmin. Sikusaini huu mkataba na mtu yeyote ila moyoni mwangu toka mwanzo nilijiapiza kuwa pretender na kweli nilifanikiwa hadi namaliza shule sikuwahi kufall in love na jasmin. Nilijua sasa naenda kuwa huru na mpenzi wangu baada ya 'kumtesa' kwa kipindi kirefu. Nilichokuwa nasubili ni kula tunda la Jasmin kwani nisingeweza kumuacha hivi hivi mabaharia wasingenielewa..Wakati nikiwa na furaha hivi sikujua kumbe tayari mpenzi wangu nimemuumiza kiasi kikubwa na ameingia kufanya utafiti............

NB:

Mpaka hapa naamini mmeshaielewa historia yangu na Jasmin, tulivyokutana hadi tunamaliza shule. Sehemu inayofata ni ya MWISHO na ndiyo sehemu iliyobeba maumivu makali sana na mambo ambayo mpaka mda huu huwa nayajutia. Ni sehemu ambayo tupo mtaani, Jasmin amezidisha upendo kwangu, mimi simtaki na upendo wangu na akili yangu yote iko kwa mpenzi wangu ambae nae sasa amegundua nina demu mpya. Kuna kipindi nilifikia hatua ya kuchagua either nimpoteze mpenzi wangu nibaki na Jasmin, au nibaki na mpenzi wangu nimpoteze Jasmin au niwakose wote...Ilifikia kipindi kumpoteza Jasmin ilikuwa sio rahisi tena maana tayari kuna mzingira yalikuwa yananifunga na kama chochote kibaya kingetokea kwa Jasmin familia yake ingenitafuta. Huku nako mpenzi wangu alikuwa bado denti wa kidato na tayari ameumia kwa kiasi kikubwa sana (aliumia sana baada ya kujua namcheat). Alianza kuyumba hadi braza ake akashitukia depression aliyokuwa anapitia mdogo wake akaanza kunitafuta..Sehemu ya mwisho ndio imebeba title ya hii thread. Sijui kama nilikuwa sahihi katika maamuzi yangu ila natamani 'Jamii' ingejua walau robo tu ya hii story niliyoiweka humu...Kama umesoma story yote kuanzia mwanzo na ukibahatika kumalizia sehemu ya mwisho naamini utakuwa umeelewa vizuri na pengine utanisaidia kujua kama nilikuwa sahihi au sikuwa sahihi na situation kama hiyo ingekukuta wewe ungefanyaje...Tukutane kesho panapo majaaliwa.....

We dogo hovyo sana, unatumia muda mwingi kusimulia part ya mwisho
 
Katka hii story yako kunamambo nmejiuliza ila nmeshindwa pata majibu, nlichoona n kwamba Jamaa ulimtamani Jamal na si kutaka kumsaidia kama ulivyodai. Kwa sababu
ikiwa hukuwai fahamiana na jamila mpaka kwa x1 mlipoonana tuition akiwa na rafiki yako then mkaonana shule ambapo haikuchua time ndefu mpaka mtoto kukueleza hisia zake
Swali ni je ulijua VP kwamba anateseka na mahusiano mpaka kufika hatua ya kumkubalia
 
SEHEMU YA MWISHO.

Mawasiliano yangu na mpenzi wangu aliye shule hayakuwa ya mara kwa mara kwani yeye ndie alikuwa akinitafuta pindi anapokuwa amepata upenyo wa kutumia simu huko shuleni. Hivyo hata kipindi ambacho alianza kukata mawasiliano namimi sikuweza kugundua mapema kwani kila nilivyoona hanitafuti nilijua tu ni ubize wa huko shuleni kwao na pengine angenitafuta. Sikuwa na mawazo yooyote kama tayari ameanza kubadilika. Huku mjini maisha ya mtaani sasa baada ya kumaliza shule Jasmin alirusi kwao kinondoni namimi nikabaki nyumbani. Mawasiliano yalikuwa ya kila siku na mwisho wa siku tulipanga miadi na nikaweza kula tunda kiulainii. Ulaji wa tunda ilikuwa ni kama malipo yangu kwa kazi kubwa niliyokuwa nimeifanya. Narudia kusema tena kuwa mpaka mda huo nilikuwa sija fall in love na Jasmin. Alikuwa binti mrembo wa kiasi chake, mpole, mwenye upendo wa dhati kwangu lakini bado nilitamani mda wowote aniache niendelee na maisha yangu. Nilitamani sana mabaharia wampitie ili anisahau lakini haikuwa hivyo. Tuliendelea kuwasiliana na kuongea mambo mengi sana kkuhusu kesho yetu. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwanini sasa nilikuwa nataka kumuacha binti wa watu, jibu ni kuwa, tayari nilikuwa na mtu wangu ninaempenda kwa dhati. Ningeendelea kuwa na Jasmin ila niliogopa kuwa kadri nilivyozidi kuwa nae ndivyo nilivyozidi kumuanisha na kumzamisha kabisa. Sasa kwanini niendelee kuwa nae wakati sina malengo nae?. Sikutaka kumpotezea mda wake na nilitaka kama kuumia aumie leo mapema atazoea kuliko kuja kuumia keshokutwa. Sikupenda awachukie wanaume kwa kiasi hicho ukizingatia kuwa alishawahi niambia kuwa yule jamaa aliyemtesa enzi zile shule ndie aliyekuwa first lover wake na ndie aliyeivunja bikara yake. Sasa jaribu kufikiria, bwana wake wa kwanza tu kwenye mapenzi kamtesa vile, namimi wa pili nimepanga kumtema. Kiukweli nilimhurumia na nilipanga kumtema taratibu mwendo wa kung'ata na kupuliza.

Jasmin kwao alikuwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa na alikuwa na urafiki wa karibu sana na dada yake aliyezaliwa kabla yake. Hakumficha kitu na tayari alikuwa amemueleza kuhusu mimi kama kijana mwenye busara na ndie mtu wake. Dada mtu alifahamu kuhusu mimi ila hatukuwahi kuonana zaidi ya kuongea kwa simu. Sasa tayari nilikuwa najuliakana ukweni. Baada ya kufikiria sana na kugundua kuwa sipaswi kumuacha ghafla huyu binti, nilianza kumuacha taratibu. Simpigii simu, simtafuti na akinitafuta sipokei simu na msg sijibu kwa wakati, hata nikijibu inakuwa kwa ufupi. Kwakuwa sikuwa nimemzoesha vile ilikuwa rahisi kwake kugundua kuwa Fohadi amebadilika. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndio nilizidisha kipimo cha kubadilika. Jasmin sasa akawa ni mtu wa kulalamika na kulialia kila siku, sikujali na nilishaamua kumove on. Mpaka muda huo tayari nilikuwa chuo mwaka wa kwanza na Jasmin nae alikuwa chuo. Vyuo viwili tofauti ndani ya mji mmoja..aiseeee, Jasmin alikuwa hakwepeki. Alikuwa anatamani aje chuoni kwetu siku yoyote kunitembelea lakini nilimwambia asije hadi pale nitakapomuita mimi, na kama angekuja bila taarifa labda kupitia marafiki zangu wa shuleni niliokuwa nao pale chuo nilimwambia wakimleta hostel kwangu mimi nitamuacha nao maana amekuja bila taarifa. Jasmin alikuwa ni mtu wa kulia, kuugua na kuhangaika kila siku. Ikafikia kipindi nikazoea kilio chake na nikawa mtu wa kutojali. Kwakwua dada yake alikuwa anajua kila kitu, alikuwa akinipigia mara kwa mara kuniomba nisimfanyie vile mdogo wake kwani hadi mama yao mzazi japo walimficha kuhusu sababu ya matatizo ya Jasmin alikuwa anaumia kuona Kitinda mimba wake hana furaha.

Pamoja na mateso yote Jasmin hakuchoka kunambia vile ananipenda na atapambania penzi letu. Aliwalaumu sana wadada wa chuo ambao pengine alihisi wamenibadilisha. Alinikumbusha mambo mengi mema mazuri tuliyofanyiana na kuniomba nisimtese kama bwana wake wa zamani. Sikumuelewa na wala sikujal, niliendelea kufanya yangu bila kujali maumivu yale. Mpaka muda huu Jasmin hakujua kama kipindi nakutana nae nilikuwa na mtu wangu moyoni. Kuna kipindi alikuwa anapiga simu kuhitaji penzi ila nilimzingua na nilimwambia niko busy na masomo. Kiukweli nilimfanyia mambo ya ovyo sana. Nakumbuka siku moja wakati wa mkesha wa mwaka mpya, jasmin ni wale watu wa kaskazini ambao wana desturi ya kurudi mkoani kwao kwajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Jasmin aliniomba niende kwa dada yake maana amebaki peke yake ndugu zake wote katika familia wameenda mkoani kwajili ya sikukuu, Jasmin alibaki kwajili ya ratiba ya chuoni kwao. Nilikubali na nikaenda kule kwa dada yake ambako alibaki kulinda nyumba ya dada yake. Hii ni moja ya siku niliyofanya kitu cha kipuuzi, kulala kwenye kitanda cha dada yake na je ingekuwaje kama dada mtu au ndugu yao mwingine angekuja akanikuta mule ndani, hahahaah nilifanya uboya sana, tuachane na hii story. Sasa nilivyoenda kweli nilimkuta Jasmin ameandaa chakula, tulikula na tukalala. Sasa wakati nimelala, simu yangu haikuwa na password kwahiyo Jasmin aliichukua na kukagua kila kitu na kukuta chats za madem kibao akiwemo yule demu wangu aliye shuleni. Hii siku huwa siisahau hadi leo maana kwa jinsi chatts zilivyokuwa na kwa jinsi alivyokuwa anaumia Jasmin na ule muda nimelala sina habari, angeweza hata kunichoma kisu kwa hasira. Lakini niliamka salama siku hiyo ya mwaka mpya na wala hakuonesha hali ya utofauti. Hakuniulizachochote hadi wakati ananisindikiza kituoni ndio akaniuliza yue ni nani na yule ni nani. Japokuwa nilipanga kumuacha Jasmin ila kitendo cha kumuona live katika hali ile kilinifanya niumie sana. Nilimpa uongo mwingi na akanipa hukumu ya kufuta zile namba zao mbele yake. Nilifuta na kitu ambacho sikujua ni kuwa kumbe zile namba zlizikopi sehemu na akabaki nazo. Nilifuta namba zote kabisa ikiwemo ya mpenzi wangu wa shule. Baadae nilivyoacahana nae pale kituoni niliisave upya namba ya mpenzi wangu wa shuleni maana nilikuwa nimeikariri. Sijui hata kama alikula vizuri sikukuuu kwakweli.

Badae Jasmin alianza kuwatafuta wale wadada (walikuwa 3, mpenzi wangu na videmu vingine viwili). Binafsi, mademu huwa siwambii jina langu la ukweli. Huyu atajua naitwa James, huyu atajua naitwa Jamal n.k. Mtu pekee aliyekuwa anajua jina langu ni mpenzi wangu Orginal. Baaada ya kuwatafuta wale wadada, wawili walisema hawamjui Fohadi kasoro yule mmoja ndie alisema ananijua Fohadi na yeye ni mpenzi wa Fohadi. Sasa hapo wakawa wamekutana Jasmin na mpenzi wangu. Alichofanya Jasmin ni kumwambia mpenzi wangu aniache, japokuwa mpenzi wangu ndiye alikuwa wa kwanza kuwa namimi hapo tumefikisha miaka 3 tayari ila Jasmin alimwambia aniache tu na alikuwa tayari kumpa zawadi yoyote ili aniache. Badae nimerudi getto chuo nimechoka, mara naona simu inaita na namba ya mpenz wangu ndio ipo kwenye screen. Kumbuka nilikuwa sijawasiliana nae muda mrefu maaana sikujua kama amenichunia so nilijiona bado niko salama kwake, kumbe maskini ya mtoto wa watu alikuwa anafanya utafiti juu yangu na sasa utafiti umejifanya wenyewe. Mpenzi wangu alilalamika sana, kwanini namfanyia vile kumbe ndio maana kwenye graduation nilimkwepa na kule tuition center nilimuongopea niko site kumbe nipo na Jasmin. Alilia sana sana na nilipomuuliza amejuaje akanambia Jasmin amemtafuta. Aiseee, mapenzi mabaya, Nilimpigia simu Jasmin na nikamlaumu sana sa kwa kumtafuta mpenzi wangu. Niliongea mambo mabaya kwa Jasmin kiasi kwamba akawa analia zaidi. Sikujali na sikukuu yangu ya Mwaka mpya ikawa imeingia misukosuko. Ninachoshukuru kuhusu Jasmin hadi leo ni kuwa hakuwa mtu wa kuchukua maamuzi magumu pengine angeweza ata kujifanyia kitu kibaya na nikaingia matatizoni. Sasa hapo sehemu zote mbili zikawa zinawaka moto.

Baada ya hapo nilipoteza mawasiliano na Mpenzi wangu ila bado Jasmin alizidi kunitafuta huku analia. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini niliwahi kumpa furaha tena. Dada yake aliporudi kutoka mkoani alikuta hali tofauti kwa mdogo wake na hapo nae uchungu ukamwingia akaanza kunitafuta ananitukana na kunigombeza kwa kumtenda mdogo wake na akasema chochote kibaya kikitokea kwa mdogo wake mimi nitakuwa mhusika wa kwanza. Nilihisi dalili za kupigwa kipapai siku za usoni hahahahaha. Nilidata kiukweli. Nilivyofanya sasa kwakuwa nilijua Jasmin angepata faraja kwa neno moja kutoka kwangu, nilimtext nikamwandikia I love you. Baada ya ile msg niliona calls kibao za Jasmin niliongea nae akasmile na pale nikajua nimemuokoa na huenda hali yake ikawa poa japo alikuwa amedhoofu sana. Wakuu niliogopa kupigwa kipapai. Sasa mtihani ukawa kujua mpenzi wangu anendeleaje, siwezi kumpigia simu kujua anendeleaje maana ni dent na anaishi na wazazi, sikuwa tayari kwa mikwaju 30. Sasa nikawa naishi kwa hofu sijui nini kinaendelea kwa mpenzi wangu na hakunitafuta tena. Basi nikawa mtu wa kuishi bila kujiamini, kila nikikutana na watu siwajui nahisi labda ni ndugu wa mpenzi wangu wananitafuta wanidake pengine kuna chochote kibaya kimetokea hahahahaha. Nilikuwa mtu wa mawazo kila mara. Sasa Jasmin hakutaka kudeal namimi tena, alichofannya ni kudeal na mpenzi wangu, kuongea nae, kumtafuta kwa simu ili kumuomba aachane namimi. Jasmin ni wale wadada wenye huruma sana..a wife material in deed. waliendelea kuwasiliana bila mimi kujua na uzuri ni kuwa kati yao hakukuwa na mkorofi wa kumtukana mwenzie. So waliendelea kuyamaliza kidplomasia.

Kuna kitu kimoja kilitokea hadi nikahisi naota. Kumbe katika harakati za masomo ya Olevel miaka ya nyuma sana, Jasmin aliwahi kufahamiana na kaka wa mpenzi wangu kupitia tuition center moja maarufu pale mwenge. Enzi hizo jasmin anasoma O level Moshi na Huyu jamaa alikuwa anasoma bagamoyo sasa walifahamiana wakawa marafiki wakati wa likizo tuition pale. Kipindi hicho wanafahamiana mimi na mpenzi wangu hatukuwahi hata kujuana. It was a long time before. Sasa, siku moja katika pitapita zake maeneo ya mjini ata sijui ni wapi, jasmin alikutana na kaka wa mpenzi wangu na walikuwa hawajaonana mda mrefu. Sasa katika story zao yule jamaa alimuuliza Jasmin vip mbona amedhoofu kiasi kile na hana furaha, Jasmin wa watu akaficha ficha mwisho akafunguka ni mapenzi tu. Mapenzi? yule jamaa akawa anamhusia aachane na huyo anaemtesa na Jasmin akasema hawezi kumuacha kwani ni mtu anaempenda kwa dhati. Sasa Jamaa akatamani kumjua huyo mtu anaependwa kiasi hicho, kuoneshwa picha akakutana na sura yangu akashituka akasema yaani unahangaika kisa hiki kijamaa?..Jasmin akasema namjua na huyu kijana mhuni mhuni tu na pia anamtesa mdogo wangu. Mdogo wako yupi?, jasmin akauliza jamaa akataja jina la mpenzi wangu na ndo hapo Jasmin akathibisha kuwa yule jamaa ni kaka wa mpenzi wangu. Binafsi, nilikuwa namfahamu kwa sura kaka wa mpenzi wangu nayeye alikuwa ananijua kwa sura. Kuna kipindi fulani mpenzi wangu aliniombaga nimsindikize kwa ndugu yake mmoja hivi, kweli tulienda kama marafiki wa shule na wala haikuwa tatizo kwa yule ndugu pale. Wakati nimekaa pale mara gafla na huyu kaka yake mpenzi wangu akaja. Alinikuta pale tukasalimiana ila hatukupiga story zozote japo tulikaa pamoja pale zaidi ya masaa 4. Wakati naondoka pale mpenzi wangu alinisindikiza, nikamuacha pale yule kaka mtu. Sijui alihisi nini kati yangu na mdogo wake ila nahisi alihisi kitu japo hakuwahi kufatilia na hata nilivyomuuliza mpenzi wangu alisema kaka yake hakumuulizaga chochote kuhusu mimi. So tunafahamiana japo hakuwahi kunijua jina ila mimi nilikuwa namfahamu jina. Hapa ndipo utata lizidi kuongezeka.

Sasa baada ya pale Jasmin alikuw na furaha sana, alijua njia rahisi ya kunitenganisha mimi na mpenzi wangu ni kupitia kaka yake. Mimi sjui hili wala lile kumbe kaka mtu alirudi nyumbani (ilikuwa bado ni wakati wa likizo ya mpenzi wangu), akampiga mdogo wake na kumuomba aachane namimi mhuni, malaya ninaemtesa pia Jasmin kabla hajawambia wazazi na akahidi kunitafuta ila 'anioneshe'. Wakati huo mimi sijui hili wala lile, kumbe natafutwa na Jasmin anafahamiana na kaka wa mpenzi wangu. Gafla nikapigiwa simu na mpenzi wangu akanisimulia kila kitu na kuzidi kuumia kwa yote yanayotokea. Nilimuomba msamaha lakini wapiiii, alikuwa ameumia sana na hakutaka tena kunielewa kwa chochote na alikuwa ameamua kunipotezea. Kwahiyo simu yake ilikuwa ni kuniambia kuwa ananiacha nibaki na Jasmin na nisimtafute tena maana mimi mhuni, malaya nina maduu wenglikizo inakaribia kuisha, simu ikakatwa na hapo . Hakuna siku niliyoumia na kupagawa kama hiyo (mapenzi yanauma sana aisee), nikachukua simu nikamtafuta Jasmin nikamuuliza kila kitu na nikamwambia kilichotokea kati yangu na mpenzi wangu na ndipo kwa hasira nikamwambia ukweli kuwa sikuwa nampenda na nilikubali kuwa nae ili tu amalize vizuri shule tu ajiunge chuo. Ulikuwa ni ukweli mchungu kwa Jasmin, nilidhani natibu kumbe naharibu. neno sikupendi lilikuwa ni zito sana kwa jasmin kulisikia kutoka kwangu. Sikujali kilio chake nikamwambia, nimempoteza mpenzi wangu kwajili yake sasa nayeye inabidi aendelee kufanya yake aachane namimi then nikakata simu. Ndani ya siku moja wote watatu tukawa tumeumia. Niliumia sana sana sana, Jasmin alipiga simu mara kibao sikupokea na msg sikujibu, hadi badae ilikuja namba ngeni kupokea kumbe ni dada yake akanitukana sana, akanimind sana na akaniambia kuwa niachane na mdogo wake maana mimi sina shukurani, sipendeki na sina roho ya ubinadamu. Akanionya nisithubutu tena kumtafuta mdogo wake na niendelee na maisha yangu. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisaaa.

Katika kuhangaika kumtafuta mpenzi wangu, siku moja simu yake nilipiga ikaita, ikapokelewa na sauti ya kiume. Nilishituka badae nikajua ni kaka yake. Bahati nzuri mpenzi wangu alikuwa amefuta namba yangu kwahiyo yule jamaa hakushituka chochote namimi nikazuga nilivyojua nikakata simu. Sikujaribu kuipiga tena ile simu na hapo connection yangu na mpenzi wangu ikawa imekatika. Mapenzi upofu, Jasmin aliendelea kunitafuta na kunitaka nimsamehe kwa makosa aliyonifanyia (Maskini, ilibidi aombe msamaha wakati mimi ndio mkosaji). Aliendelea kunitafuta akilia na muda huu hakuwa akimshirikisha dada yake tena maana nahisi angepigwa maana alishaonywa. Hivyo hakuwa na uwezo tena wa kulia au kuugua mbele ya ndugu zake maana wameshamuonya kuhusu mimi. Kwahiyo, alikuwa akilia na kujinyamazisha mwenyewe. Mimi huku ndo sijui ata mpenzi wangu nitampata vipi na yupo shule. Miezi ilienda ndipo siku 1 nikapokea msg kutoka kwa Jasmin, Ilikuwa ni mwezi wa 10 nipo likizo ndefu ya chuo. Aliniandikia maneno mengi ya kuumiza ila dhumuni kubwa lilikuwa ni kuniambia kuwa AMECHOKA na AMEKUBALI kuniacha niishi maisha yangu. Mwishoni pia aliandika neno moja lililonopa faraja kuwa "Fohadi, nakushukuru sana kwa kunivusha kipindi cha masomo, nimekusamehe kila kitu". Huo ndio ulikuwa mwisho wangu na Jasmin, Binti aliyenipenda kupita kiasi hatimae alikuwa ameamua kukaa pembeni kuepusha msongamano. Kama maumivu ameyapata ya kutosha na sasa alitaka kupona na kuendelea na maisha yake. Sikuijibu ile msg ila moyoni nilifurahi angalau msamaha wake utaniepusha na malipo ya hapa duniani. Na kubwa zaidi naachana ane akiwa mzima wa afya kasoro mwili tu ambao utarudi.

Baada ya wiki tatu nilimpigia simu Jasmin na kumwambia kuhusu kuupata ujumbe wake. Hapa sasa bila hasira na shida yoyote niliamua kumuelezea kila kitu kuhusu nilikotoka na mpenzi wangu na kwanini nilikubali kuwa nae kimahusiano pale sekondari. Nilimuomba msamaha kwa unyama niliomfanyia na nikamtakia kila la heri kwenye safari ya maisha yake. Alilia sana na kunishukuru kwa kumfanya kupata cheti cha elimu ya sekondari na kuingia chuo. Alinisamehe kwa moyo mmoja na akasikitika sana kuwa laiti angejua kuwa nilikuwa kwenye uhusiano toka siku ya kwanza asinge lazimisha kuni approach maana hapendi kuingilia mahusiano ya watu. Alinitakiwa maisha mema na mpenzi wangu lakini nikamwambia kuwa sipo nae tena maana kaka yake baada ya kujua kila kitu amesababisha tukaachana. Jasmin alijutia sana na akaniomba radhi lakini nilikataa msamahan wake kwani mimi ndio nilipaswa kumuomba radhi. Tuliachana kwa amani tukawa marafiki. Huku kwa mpenzi wangu alikuwa tayari amemaliza elimu ya sekondari na sasa alikuwa anajiandaa kwenda chuo kimoja pale jijini dodoma. Mimi nikiwa naenda kuingia waka wa pili yeye alikuwa anenda kuanza first year.

Siku moja nilipokea simu kutoka kwa mpenzi wangu, baada ya mda mrefu sasa alinipigia simu kunisalimia. Tuliongea mengi sana na akasema alinichukia sana kwa kunitenda na leo amenipigia simu baada ya Jasmin kumtafuta na kuniombea msamaha. Yaani jasmin alimtafuta mpenzi wangu na kuniombea msamaha na kumwambia kuwa ametuacha tuwe wote. Alimsimulia kila kitu mpenzi wangu kuhusu sababu iliyonifanya nikamsaliti na kuwa nae. Mpenzi wangu alielewa ndipo akakubali kunitafuta japo anisalimie. Sasa Jasmin na mpenzi wangu wakawa marafiki na wakawa wanashauriana mambo mengi sana. Nilifurahi kwa swala hilo. Bahati mbaya kwangu ni kuwa mpenzi wangu tayari alikuwa ameamua kuendelea namaisha yake na tayari alikuwa na mtu wake mpya. Nilipambana sana kumrudisha katika himaya lakini wapiiiii. It was too late na tayari nilikuwa nimempoteza mpenzi wangu. Kati ya jasmin na mpenzi wangu sielewi nani alinipenda zaidi maana walichotofautiana tu ni material things, Jasmin alikuwa na uwezo mkubwa kifedha. Ila wote walinipenda kwa dhati sana sana sana sana japo moyoni hadi leo nampenda sana mpenzi wangu kuliko Jasmin. Katika historia yangu ya mahusiano sijwahi kupata mwanamke aliyenipenda kwa dhati kama wale. Nilibahatika kupata upendo wa dhati, nasema tena wa dhati ila niliupoteza. Niliumia sana kuhusu mpenzi wangu lakini hakuna kitu ningeweza kufanya kubadili uhalisia. Nilitumia nguvu kubwa sana kurudisha pendo la mpenzi wangu lakini haikuwezekana. Baada ya kuona ngumu ikabidi nirudi kwa Jasmin kwani niliamini ananipenda na angeweza kunipa nafasi kwakuwa sasa nilikuwa huru na single boy. Sikuwa na bahati Jasmin tayari alikuwa ameamua kunisahau japo alinipenda lakini hakutaka kuingia kwenye migogoro na ndugu zake kwa kunirudia. Niliwakosa wote na nimeamini mwanamke akikupenda kwa dhati yupo tayari kuvumilia kila kitu, ila akisema NO aiseeeee ni NO kweli kweli...Huwa hawarudishi moyo nyuma wale aiseeee. Walinipenda kwa dhati japokuwa sikuwa na kitu. Wema wangu kwa Jasmin uliniponza nikapoteza penzi la mpenzi wangu. Ninachoshukuru sasa kila mtu alinisamehe na kunielewa na kunitakia kila laheri. SIpendi kuacha vinyongo kwa mwanamke. Sasa hivi hatuwasiliani sana ila kila mtu yuko na serious relationship yake kasoro mimi hapa ambae nahangaika kumpata wa kujenga nae maisha.

HITIMISHO:

Historia yangu imejaa mambo mengi sana lakini mwishoni nilikosa wote. Wanawake wenye upendo ww kweli wapo, ukimpata akupendae mthamini na mtunze maana siku ukimpoteza ndio utajua umuhimu wake. Mpaka sasa hivi sina serious relatinship na nimekuwa nakutana na vimbwenga vya kila aina kwenye mahusiano. Nahisi karma inanitafuna. Na siku zote nikipataga nafasi ya kuongea nao huwa nawakumbusha kuhusu kunisamehe kwa dhati ili watoe vinyongo vyao vyote. Na wote wamesema wamenisamehe japo niliwaumiza na sasa wana furaha.

Mpaka sasa sijui kama nilikuwa sahihi au kuna sehemu nilifanya uamuzi wa makosa katika story yangu. Pengine mwana JF unaweza kuniambia ni wapi ambapo nilifeli. Chanzo cha yote haya ni Jasmin, lakini je, Nilikosea kuwa nae katika mahusiano?, je ningemuacha apotee kiafya na kielimu wakati nilikuwa nauwezo wa kumsaidia?, Je nilikosea kutompa nafasi Jasmin ndani ya moyo wangu au labda nimekosea wapi. Huwa sielewi kama nilikuwa sahihi au la. Kun amuda najutia ila kuna mda nafarijika kuona Jasmin 'niliyemuokoa' yupo na furaha na anaendelea vizuri kiuchumi na kuleta tabasamu kwa ndugu zake...

Pamoja na yote, tatizo kubwa ni 'jamii' nikimaanisha ndugu wa jasmin na marafiki zake ambao walikuwa wananijua na kujua uhusiano wetu hadi leo wananiona mwanaume katili sana kwa kumfanyia vile ndugu na rafiki yao. Bahati mbaya hawajui chocote kilicho nyuma ya pazia japo huwa natamani wangejua japo robo tu maamuzi yangu na hii story pengine wangenipunguzia hukumu katika mioyo yao. Na bahati mbaya hawatakuja kuujua ukweli wangu wote. Kuna muda nahisi pengine vinyongo vyao ndio vinanihukumu katika mahusiano mbalimbali. Lakini sina jinsi naishia kutamani wangejua. Pengine kama wapo hapa JF wanaweza unganisha dots na kunipunguzia adhabu kwa sababu naamini I played a fair game. Sikuwa tayari kumpoteza mpenzi wangu kisa Jasmini.

Kwako mwana JF, heshimu hisia za mwenza wako awe ni ME au KE. Kuna siku utatamani urudishe masaa nyuma ili u-win trust yake lakin itakuwa sio rahisi. Hamna kitu kibaya kama kumwaga machozi au kumpa maumivu mtu anaekupenda kwa dhati. Hiki nimejifunza na huenda kwa vyovyote vile my future wife afaidika kutokana na funzo nililopata kwenye mahusiano yangu ya awali. Ila nitampata lini huyo future wife?, yuko wapi?, atanipenda kwa dhati?..Mmi sijui. Na je ni lini Jamii itanisamehe na kunipunguzia vinyongo na lawama ambazo nimechoka kuzisikia kwa kitu ambacho nilifanya kwa faida ya Jasmin?..Mimi sijui nachojua nikuwa nilimpoteza mpenzi wangu na kwasasa napambana na hali yangu iliyojaaa upweke. Upweke wangu ni kukosa kupata mwanamke sahihi wa kujenga nae maisha..I wish and I hope nitampata as long as nishajutia kosa langu, wahanga wamenisamehe..Kuweni makini na hisia za wenzi wenu pamoja na maamuzi yenu katika mahusiano.

Poleni kwa story ndefu. God bless you all.

NB: This is a true story about me...Focus Hardwork Discpline...FOHADI.

Obligado.

Kwanza nikwambie kitu kimoja tu hapo unaongelea habari za "mwanamke" anayekupenda sijui nini blah blah wakat Ulikua na visichana hivyo

Hayo mapenzi yenu yana/yalikua na utoto mwingine sana

Nikwambie ukweli tu bado hujawajua wanawake ila ndo unaelekea kujifunza vizuri kuhusu wanawake na jinsi ya kuishi nao. Yule umpendae na michepuko yote na uwafurahishe wote(Umesema Ulikua na mpenz na Jasmin na videmu) so unaelewa kumbe kuwa wanaume tuna makoloni mengi

Mwishiy kabisa ishi maisha yako,hakuna laana ya ndugu wala hukumu sijui vinyongo vya rafiki. Enjoy maisha, uliyeandikiwa kumuoa atakuja tu na michepuko utajipatia tu

Bazazi mkongwe nakushauri
 
Mapenzi yanaumiza sana mwamba ,hasa sie madomo zege na wenye aibu.Nilishawahi kupenda , kishule shule,unamchana makavu wala haelewi.Afu ndo moyo umemkubali hatar ,nilihangaika mpaka anenda chuo mambo ni 0-0.Apo ndo nikaanza kuzingatia nyasi kwa sana na viroba ndo ikawa faraja yangu.Mpaka Leo miaka imepita dogo namuelew ,ila ndo ivo acha nipambane na upande mwingine wa maisha tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom