PapoKwaPapo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2008
- 380
- 45
nimeona jinsi wabunge walivyokuwa wanapata shida kujieleza walipokuwa wanagomembea uwakilishi wa SADEC nimecheka kupita kiasi kwa watu walikuwa wanatumia nguvu kupita kiasi ili waweze jielezea..........
Walishindwa kabisa kusema nini watakachokifanyia tz huko sadec zaidi watu wanataja tuu vyeti vyao feki.....embu jaribu kuicheki kwenye youtube hii hapa, Wagombea wa uwakilishi SADC
siyo SADEC ni SADC.:A S angry:
IKO wapi hiyo clip ya you tube
mkuu kama unakumbuka kwenye mdahalo wa dr wa ukweli alisema namnukuu " hata mimi nimeathirika kule kwangu karatu, kuna hoteli 20 za kitalii na hata mbeba mizigo ni kutoka nje ya nchi, na wanayo sababu kwani wanasema wageni wangu ni kutoka nje ya nchi na anapotembea anataka aulize swali hili na hili" mwisho wa kunukuu so kingereza kina umuhimu wake hususani dunia hii tunaishi sas ivi............Sijui ni ushamba , sijui ni ulimbukeni , sijui ndiyo ukoloni bado upo mpaka vichwani kwetu!. Mimi nashangaa sana mtu anapofikiri kujua kiingereza sijui ndiyo elimu ? . Hii kasumba inatusumbua sana, kama kiswahili tu watu kinawagonga unategemea mtu atakuwa na miujiza kuongea lugha ambayo siyo yake na haitumii mara kwa mara?. Mimi nafikiri kasumba hii inatutafuna na ndiyo inatufanya tusiendelee, hata wataalamu wetu huenda tunawalalamikia kuwa wamesaini mikataba mibaya, si wanajifanya wanajua kiingereza kumbe hawahjui wanaishia kusaini tu. Ukweli ni kwamba ni matatizo wa kuwatawaliwa na wakoloni, kwani hao wabunge walioongea kiingereza leo wanazidiwa kiingereza na Fabio Capelo -kocha wa Uingereza ? mbona waingereza tena ndiyo wenye lugha hawasemi hivyo na wala hata yeye haoni aibu. Mimi sijawahi sikia Marcio Maximo akichekwa kwa kiingereza chake kibaya, tena ni kibaya kuliko watanzania wengi wanavyooongea.
Tuache kiingereza kiwe lugha kama lugha zingine Kifaransa, kireno, kimatumbi n.k , hiyo sifa ya kiingereza kama ina maana hivyo je ni miongoni mwa sifa za kuwa Mbunge? kama siyo sifa kwanini sasa. Hiyo ni kutishana tu kunakotumiwa na wajanja wachache tena wasio na uwezo.
Nimesema kwamba kiswahili chenyewe ni shida kwa watu wengi mbona hatuchekani, mbona mzee wa kiraracha hawezi kutamka Nchi anasema NJI mbona hakuna anayemcheka au kwa sababu ni kiswahili?
Kuongea kiingereza si ujanja, kikubwa ni IQ yako inavyofanya kazi, kama mtu hawezi kuongea kiingereza anaongea kiswahili translator atafanyakazi ya kutafasiri. kuna watu bongo wanaongea kiingereza kizuri lakini kichwani hamna kitu. Binafsi naona wanaosisitiza kiingereza wanakasumba ya kikoloni. unatakiwa kujua kiasi na kujiamini, so hata hao uliowaona wanatumia nguvu kujieleza kwangu natafsiri kuwa walikuwa hawajiamini tu-"lack of confidence" tu
Kuongea kiingereza si ujanja, kikubwa ni IQ yako inavyofanya kazi, kama mtu hawezi kuongea kiingereza anaongea kiswahili translator atafanyakazi ya kutafasiri. kuna watu bongo wanaongea kiingereza kizuri lakini kichwani hamna kitu. Binafsi naona wanaosisitiza kiingereza wanakasumba ya kikoloni. unatakiwa kujua kiasi na kujiamini, so hata hao uliowaona wanatumia nguvu kujieleza kwangu natafsiri kuwa walikuwa hawajiamini tu-"lack of confidence" tu