Natamani Angekuwa ni Binti Yangu

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Binti Kinara 'form 4' afichua siri
attachment.php

JUHUDI, ufundishaji wa walimu, na malezi bora ya wazazi ndiyo siri kubwa ya mafanikio ya mwanafunzi bora wa kidato cha nne kwa mwaka 2009 nchini Tanzania.

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limemtangaza, Imaculate Mosha(16) kuwa ni kinara wa matokeo hayo, amewabwaga watahiniwa wenzake 315,151 waliofanya mtihani huo.

Msichana huyo amesema, hakuna kitu cha ziada kilichompa matokeo hayo zaidi ya hivyo.

"Ni furaha kubwa sana kwangu, namshukuru Mungu, wazazi na walimu kwa hili kwani bila wao na jitihada zangu binafsi hakika nisingefikia hapa nilipofikia," alisema Mosha mjini Bagamoyo muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo hayo.

Mosha alipokea matokeo hayo muda mfupi baada ya kutoka katika chumba cha mtihani katika Shule ya Sekondari St. Marian iliyopo Bagamoyo alipokuwa akifanya usaili pamoja na wanafunzi wengine wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu.

Mosha ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa Resto Mosha wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro na mama Agatha Mosha Mhasibu wa NSSF mkoni humo.

Mwanafunzi huyo kinara kutoka shule ya sekondari St Marian alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi 84 waliofanya mtihani huo mwaka 2009 shuleni hapo.

Akielezea historia yake ya mwenendo wa masomo yake darasani Mosha, alisema, nyota yake kishule ilinaza kung'ara tangu akiwa kidato cha kwanza shuleni hapo muhula wa pili aliposhika nafasi ya kwanza darasani.

"Nilianza kidato cha kwanza na katika mitihani ya muhula wa kwanza nilikuwa mtu wa nne darasani, niliongeza bidii na mwisho wa mwaka nilikuwa wa kwanza hadi namaliza kidato cha nne darasani sikuwahi kuachia hiyo namba," alisema Mosha.

Amesema, katika mitihani ya mchujo wa kidato cha pili yeye alishika nafasi ya 7 Kanda ya Mashariki jambo ambalo pia lilimsukuma kufanya vizuri zaidi.

Mosha aliyezaliwa katika Hospitali ya taifa Muhumbili, Mei 6 mwaka 1993 alianza elimu yake ya awali (chekechea) katika shule ya St. Ann mjini Morogoro na baadae kuanzia hapo darasa la kwanza hadi la tatu alipohama.

Darasa la nne alihamia katika shule ya Msingi Mukidoma iliyopo mkoani Arusha alipo malizia darasa la 7 mwaka 2005 na baadaye kalijiunga na sekondari ya St. Marian mjini Bagamoyo.

Mosha anasema, anamuombva Mungu amsaidie katika masomo yake ili ndoto yake ya kuwa mhandisi wa mitambo(Mechanics Engineer) itimie.

"Napenda sana hapo baadae niwe Injinia, hivyo nitaongeza bidii na kumuomba Mungu sana anitimizie hiyo ndoto yangu," alisema Mosha.

Akizungumzia maisha binafsi anasema miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni vile ambavyo watu wanaweza kumhukumu mtu kutokana na mwonekano wake wa nje.

"Sipendi sana watu ambao wana 'judge the book by its cover' bila ya kujua undani halisi wa mtu mwenye kama anaendana kweli na muonekano huo.

Akiwa ni msichana mwenye kupenda sana kula wali nyama kuliko vyakula vyoyote, pia hupendelea kuvaa suruali na ndiyo vazi ambalo hulipenda na kinywaji chake kikubwa ni soda iitwayo Fanta.

Pia anapenda kuwausia wanafunzi wenzake hasa wasichana kutojihusiha na vitendo visivyo faa katika kipindi cha shule kwani anaamini kuwa ndiyo msingi mbaya wa maendeleo yao shuleni.

"Mimi naamini kila kitu kina wakati wake, ukifika nitafanya hivyo ila kwa sasa sijawahi kujiingiza katika vitendo vya anasa na nawahusia wanafunzi wenzangu kuwa waachane na vitendo hivyo," aliongeza Mosha.

Source: Habari Leo ---http://www.habarileo.co.tz

NB
Nimefurahishwa sana na huyu binti, amesifia wazazi wake walivyomlea. Baba Prof na mama Mhasibu, nimejifunza kitu lazima wanandoa waangalie background ya mwenza wake ili matunda ya ndoa yawe yana neema. Hongera sana Immaculata nakutakia mafanikio na ndoto yako ya kuwa Engineer kama kaka yako ifanikiwe. Ubarikiwe sana
 
Mtoto wa namna hii niko tayari kujinyima kila kitu nimtimizie ndoto yake.....! hongereni wazazi pia
 
Hongera sana Imakulata,hahaha Genes jamani hamna kuolewa na kilaza wala kuoa kilaza.mimi mwanangu huwa anasema lazima awe injinia wa AIRBUS hahaha.
 
Alafu naambiwa mabinti wenye sura za mbuzi ndo huwa wanafauru sana au ndo vichwa darasani.
 
Hongera sana Imakulata,hahaha Genes jamani hamna kuolewa na kilaza wala kuoa kilaza.mimi mwanangu huwa anasema lazima awe injinia wa AIRBUS hahaha.

Hehehehe Pole mama 5J's nimeona kule shule yenu imedondokea pua hakuna kitu kabisa.
 
Hongera sana Imakulata,hahaha Genes jamani hamna kuolewa na kilaza wala kuoa kilaza.mimi mwanangu huwa anasema lazima awe injinia wa AIRBUS hahaha.

I love this comment...umenianzishia Jumatatu vizuri! Mimi kigezo ni GPA kama demu hana zaidi ya 4 na kwenda juu wala siwezi mdate, asije nipakazia mimba tukazaa kilaza. Mzenj wangu anafirst class teh teh teh eteh
 
Mosha anasema, anamuombva Mungu amsaidie katika masomo yake ili ndoto yake ya kuwa mhandisi wa mitambo(Mechanics Engineer) itimie.
Nakuombea kila la kheri ili ndoto yako itimie. Fani unayoi dream ni fani nzuri na inawezekana. Siku hizi ni kina dada wachache sana wametokea kuipenda fani hiyo maana inahitaji msuli wa kutosha ili kufanikiwa kumaliza masomo yake. Isipokuwa ni fani nzuri, huta regreat! Tunahitaji wahandisi wa kike maana nasikia hawazi 10% ya wahandisi waliopo Tanzania.
 
Hehehehe Pole mama 5J's nimeona kule shule yenu imedondokea pua hakuna kitu kabisa.
hahaha Fidel matokeo ni mabaya sana yaani hata nashindwa kuelewa kosa ni walimu au wanafunzi?kunahitajika changes za kifikira inabidi nipange safari ya kutia timu huko ili nielewe tatizo ni nini?
 
hahaha Fidel matokeo ni mabaya sana yaani hata nashindwa kuelewa kosa ni walimu au wanafunzi?kunahitajika changes za kifikira inabidi nipange safari ya kutia timu huko ili nielewe tatizo ni nini?

Hahahah genes za wazazi za hao watoto huenda pia zilichangia!
 
Unaowa ama kuolewa na ukoo hauna graduate hata mmoja....unategemea nini kwa watoto wako? Ukoo una form form failure mmoja.....!LOL
 
I love this comment...umenianzishia Jumatatu vizuri! Mimi kigezo ni GPA kama demu hana zaidi ya 4 na kwenda juu wala siwezi mdate, asije nipakazia mimba tukazaa kilaza. Mzenj wangu anafirst class teh teh teh eteh
hahahaha Masanilo si haba hapo mtoto asipoaffectiwa na mazingira lazima awe kipanga.
hahaha kigezo chako cha GPA kimeniacha hoi.
 
hahahaha Masanilo si haba hapo mtoto asipoaffectiwa na mazingira lazima awe kipanga.
hahaha kigezo chako cha GPA kimeniacha hoi.

Baba Kipanga Mama Kipanga hata mazingira yatakuwa ya Ukipanga......
 
Huyu binti yupo katika mafimilia bora anastahili kuperform wonders
 
Mtoto wa namna hii niko tayari kujinyima kila kitu nimtimizie ndoto yake.....! hongereni wazazi pia

masanilo asante kwa hili neno la busara!!

Alafu naambiwa mabinti wenye sura za mbuzi ndo huwa wanafauru sana au ndo vichwa darasani.

nani kakudnganya wewe, hamna cha sura ya mbuzi wala sura ya malaika hapa. anyone ca have a smart brain despite of hw they look like tafuta factor nyingine relevant
 
Back
Top Bottom