Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
I suspect NN is a magnet designated through this thread to attract all wenye nia mbaya na rais to utter their boiling grudges here. Then, it will be easy for "right machinery" to fetch them out!!
Be Careful with what you are posting here.
 
[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] wanaotaka kuombewa waje inbox niwapime akili kwanza maana maana nataka kuanza maombi huu mwaka.
 
Lini tumewahi kuwa na maisha mazuri yenye nafuu?

endeleeni kumsifia tu!
 
Tumerudi nyuma miaka 55 kabla ya uhuru! Yes, kuna tofauti gani kati ya aliyofanya mkoloni mzungu na haya anayofanya mkoloni mwenzetu mweusi? By the way kuna mawili...hana washauri kabisa, anao ila yeye ndiye anayetoa ushauri badala ya kushauriwa!
 
I suspect NN is a magnet designated through this thread to attract all wenye nia mbaya na rais to utter their boiling grudges here. Then, it will be easy for "right machinery" to fetch them out!!
Be Careful with what you are posting here.
Ha ha ha nimeishia kucheka tu.
 
I suspect NN is a magnet designated through this thread to attract all wenye nia mbaya na rais to utter their boiling grudges here. Then, it will be easy for "right machinery" to fetch them out!!
Be Careful with what you are posting here.
Ukiyavulia maji nguo huna budi kuyaoga.
 
Bunge limezibwa mdomo, vyombo vya habari vimewekewa speed gavana na JF mnataka kuiziba mdomo? Hili haliwezekani.

Labda tukumbushane tu inawezekana wengi wameijuwa JF sasa hivi, kama Rais wetu amepania kwa dhati kupambana na ufisadi na mchwa wote wanaolihujumu Taifa basi JF ndio tool number one ya kuitumia bila gharama yoyote.

Watu wa vyombo vya dola mkumbuke kashfa ya Richmond kwa mara ya kwanza ilibuuliwa hapa JF, hata ujiko alioupata Dr Slaa bungeni 90% ya data zake alikuwa anazipata hapa.

Marehemu Samuel Sitta alimponda Dr Slaa ati ana ushahidi wa kuokoteza vichochoroni lakini ukweli ushahidi ule ulikuwa thabiti na hatimaye ukweli ulijulikana.

Majangili wote wakubwa orodha yao iko hapa JF, nilitalajia vyombo vya dola viverify information zilizopo hapa.

Orodha wa wauza unga wakubwa wote iko hapa JF, nilitajia Anti drugs wapate pa Kuanzia through hizi information.

Isitoshe Max kwa nia njema ameweka thread maalum ya kuishauri serikali na kufichuwa uovu mbalimbali yote hii ni kazi bure?

Hivi mtu kama Max anayestahili tuzo kwa kazi aliyoifanya kwa Taifa badala yake tuzo yake ndio iuwekwa ndani?

Huu uzalendo mnatuhubiria tuwe nao nitakuwa vipi mzalendo, kama mzalendo wa kweli kama Max anatendewa haya?

Mwigulu brother cheo ni dhamana, kumbuka hayo mabasi ya kubeba maabusu aliyaleta Laurence Masha finally na yeye akayapanda na alilala segerea.

Cheo cha uwaziri ni dhamana lakini ukirudi nyuma wewe ni mwanachama mwenzetu hapa na wanaomshikiria Max wapo chini yako hivi mheshimiwa huyu Max ameuwa mpaka ushindwe hata kuwaambia vijana wako wampe dhamana atakuja kuripoti polisi? Hivi tukufikiriaje?

Funguwa ile thread ya utetezi wako kuhusu wewe kufoji na kutumia jina la mtu jinsi tulivyokutetea huku tukiujuwa ukweli lakini tulisimama kukutetea kwa sababu tunaujuwa mfumo wa nchi yetu ulikuwaje enzi za mwalimu.

Leo hii wewe huyuhuyu muheshimiwa sana unashindwa kumtetea Max? Ni thread ngapi hapa JF huwa zinapigwa kufuri kama haziendani na maaudhui mpaka vijana wenye mihemko wa Chadema wanasema JF imenunuliwa na ccm?

Kwakweli hii ni chuki ya bure mnaijenga, Max ana wafuasi wengi kuliko mnavyoweza kufikiri labda naona mmeamuwa kulipaisha jina lake hata wasoma udaku sasa wamjuwe maana Max always anaaply low profile.
 

Nyani ngabu kwa mara ya kwanza, kwa jinsi ninavyokusoma na kukuelewa, aidha umeandika kwa hasira au ni bandiko la kuchokonoa mawazo ya wanaJF!

1) Unataka Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Kumbuka yeye ni Rais na nyuma yake anao milioni kadhaa ya wananchi waliomweka madarakani kwa kura zao. Kwa msingi huo, wewe na wenye mawazo kama wewe, mtashindwa na kulegea. Katiba ya JMT (1977) inampa madaraka makubwa kama unavyofahamu. Pamoja na hilo anawajibika kulinda haki na uhuru wa kila mwananchi, hata na wanaomwombea kushindwa na kulegea kama wewe.

2) Hakuna aliye juu ya sheria, hivyo mtu yeyote akivunja sheria, atafikishwa kwenye vyombo husika. Kama ulivyoandika "Haogopwi mtu zama hizi". Hata wewe Nyani Ngabu maandiko yako haya yakionekana yanaashiria kuvunja sheria ya mtandao, hutoogopwa. Hizi ni zama za utawala wa sheria.

3) Ukichemka nami nitakukusoa kama ninavyokukosoa kwa hoja zangu hizi. Ukichapia kiingereza nitakucheka, ila naamini utachapia tu kwa kuwa lugha ya kiingereza umeisomea darasani na kufundishwa na mwalimu ambaye pia siyo lugha yake ya asili.

4) Kwa hiyo nami nataka ushindwe na ushindwe kabisa kwa kudhani ndoto zako zinaweza kuwa kweli na maombi yako hayo kuhusu Yeye, yakurudie. Mwungwana humwombea binadamu mwenzake heri!

Mimi mdau hayo ndiyo yangu ninayosema.
 
nyani ngabu ushindwe na ulegee. napenda uhuru wa habari ila sio wa kuwalinda wenye lengo la kuendeleza dhuluma kwenye jamii kufanikisha malengo yao. kwa kuonyesha chuki kwa jpm nahisi una maslahi na watumbuliwa wa ufisadi rushwa uzembe na ubadhilifu au mrija wa dili umekatwa.
 
Halikuwepo nyerere sembuse yeye hivi mungu wa dar simsikii et tumwombee wakati kateuwa mungu ambae anasema akisimama yeye hakuna wa kupishana nae
 
Mkuu umeshachukua passport ya blue na kuachana na ile yenye rangi ya ccm(kijani)? Si unajua mtukufu hajaribiwi.
 
wewe hujui anadhulumu haki za wafanyakazi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…