Tayana-wog
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 28,851
- 37,565
Hii comment safi sana!Ubaya wa ukada ni unaona udikteta asubuhi ila jioni unaona huohuo udikiteka kuwa umahiri.
Ubaya wake ni pale ndugu yako au maslahi yako yakiguswa na kwa unafiki wa umri unampinga.
Ila akikamatwa fulani,kupigwa n.k ambaye hali chakula nawe,basi mdomo hutoa sifa tu kwa dikteta.
Mzima? Uwa nashindwa kukuelewa.Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.
Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.
Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.
Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hiyo azma yake iwe muhali.
Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.
Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.
Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.
Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.
Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.
Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.
Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Mzima? Uwa nashindwa kukuelewa.
Julius Magembe aka Nyani Ngabu anataka ngosha mwenzake ashindwe
Heheheee Julius Magembe.
Halafu Faru Kabula wewe ni wa kitambo eeBwa ha ha ha
So huyo ndo nani?
Link Julius Uko wapi?Julius Magembe aka Nyani Ngabu anataka ngosha mwenzake ashindwe
Hatari sanaWatu wanafukua makaburi
Sio sahihi? Huko ni mbali sana
Mmoja alinusurika kupigwa risasi,vp bado dua yako inaendelea?Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon
Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
Hajanusirika kupigwa risasi bali alinyooshewa bastola. Kunusurika maana yake risasi imefyatuliwa ila ikakukosaMmoja alinusurika kupigwa risasi,vp bado dua yako inaendelea?
kushindwa kufanyika ndiyo kunusurika kwenyewe . Kwani bastola ni kitu ni kitu cha kawaida kuonyeshewa.Hajanusirika kupigwa risasi bali alinyooshewa bastola. Kunusurika maana yake risasi imefyatuliwa ila ikakukosa
Sawa Mkuukushindwa kufanyika ndiyo kunusurika kwenyewe . Kwani bastola ni kitu ni kitu cha kawaida kuonyeshewa.
Kubadilika ni kitu cha kawaida kwa binadamu. Wapo waliokuwa wanamsema vibaya Mh. Lowassa kwamba eti ni fisadi; sasa hivi wamebadilika na wanamsifia baada ya kumfahamu vizuri! Hadi wanatamani awe presida wao!Tatizo lako Nyani Ngabu ni kubadilika badilika kwako kama kinyonga.Leo umesema vyema kabisa kwamba huyu jamaa apingwe.Lakini muda si mrefu utakuja kumsifia tena!!