Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Hivi yule aliyesema serikali haina ugomvi na Dangote na anatala gesi ya bure kisha kesho yake akasema kweli serikali intatizo na Dangote na jana alidanganya ila ukweli ndio huu. Ni nani muongo hapa????
 
Bunge limezibwa mdomo, vyombo vya habari vimewekewa speed gavana na JF mnataka kuiziba mdomo? Hili haliwezekani.

Labda tukumbushane tu inawezekana wengi wameijuwa JF sasa hivi, kama Rais wetu amepania kwa dhati kupambana na ufisadi na mchwa wote wanaolihujumu Taifa basi JF ndio tool number one ya kuitumia bila gharama yoyote.

Watu wa vyombo vya dola mkumbuke kashfa ya Richmond kwa mara ya kwanza ilibuuliwa hapa JF, hata ujiko alioupata Dr Slaa bungeni 90% ya data zake alikuwa anazipata hapa.

Marehemu Samuel Sitta alimponda Dr Slaa ati ana ushahidi wa kuokoteza vichochoroni lakini ukweli ushahidi ule ulikuwa thabiti na hatimaye ukweli ulijulikana.

Majangili wote wakubwa orodha yao iko hapa JF, nilitalajia vyombo vya dola viverify information zilizopo hapa.

Orodha wa wauza unga wakubwa wote iko hapa JF, nilitajia Anti drugs wapate pa Kuanzia through hizi information.

Isitoshe Max kwa nia njema ameweka thread maalum ya kuishauri serikali na kufichuwa uovu mbalimbali yote hii ni kazi bure?

Hivi mtu kama Max anayestahili tuzo kwa kazi aliyoifanya kwa Taifa badala yake tuzo yake ndio iuwekwa ndani?

Huu uzalendo mnatuhubiria tuwe nao nitakuwa vipi mzalendo, kama mzalendo wa kweli kama Max anatendewa haya?

Mwigulu brother cheo ni dhamana, kumbuka hayo mabasi ya kubeba maabusu aliyaleta Laurence Masha finally na yeye akayapanda na alilala segerea.

Cheo cha uwaziri ni dhamana lakini ukirudi nyuma wewe ni mwanachama mwenzetu hapa na wanaomshikiria Max wapo chini yako hivi mheshimiwa huyu Max ameuwa mpaka ushindwe hata kuwaambia vijana wako wampe dhamana atakuja kuripoti polisi? Hivi tukufikiriaje?

Funguwa ile thread ya utetezi wako kuhusu wewe kufoji na kutumia jina la mtu jinsi tulivyokutetea huku tukiujuwa ukweli lakini tulisimama kukutetea kwa sababu tunaujuwa mfumo wa nchi yetu ulikuwaje enzi za mwalimu.

Leo hii wewe huyuhuyu muheshimiwa sana unashindwa kumtetea Max? Ni thread ngapi hapa JF huwa zinapigwa kufuri kama haziendani na maaudhui mpaka vijana wenye mihemko wa Chadema wanasema JF imenunuliwa na ccm?

Kwakweli hii ni chuki ya bure mnaijenga, Max ana wafuasi wengi kuliko mnavyoweza kufikiri labda naona mmeamuwa kulipaisha jina lake hata wasoma udaku sasa wamjuwe maana Max always anaaply low profile.
Wape za mbavu hao Mkuu!

Hata mimi niliipata ishu ya mheshimiwa kujiuzia nyumba za serikali mahali hapa.
 
Maneno yako na yakapate kibali, kwa Mungu ili yatimie 2020, Ee Mungu baba tunakuomba ukatuinulie Edward Lowasa awe rais wetu wa Tanzania, tunaomba na kushukuru kwa Jina la Yesu...wote tuseme amen
Amen!
 
Mimi naombea dua za LEMA zitimie huu yake leo kesho!!
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hiyo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Kila mtu ni kichaa ukitaka kujua ukichaa wa mtu suburi akikasirika yeye anajivunia nguvu ya dola (peoples power) ndiyo mpango mzima
 
Hata kulike point nzuri tumekuwa waoga maana unaweza ukalike nyundo ya mdau kumbe jamaa ndio wanaispot hiyo hiyo nyundo wakijafanikiwa (just incase) kupata access ya jf watabeba mtoa hoja na waliolike.
Mbona tunalo

Ahahahahaaaaa daaah hii ni kali aisee.
 
JF needs to go hollow mode....tuone watakamata nani. Na ndio wapigwe za uso mpaka waombe pooo! nimeumia sana jinsi wanavyo m-treat Max
Adhabu ya dhambi ni mauti. Mungu wajua nini cha kuwafanya watesi/magoliath hawa.
 
Umemtandika za uso msukuma mwenzio bila huruma

Ila hii ndio lugha anayoielewa

#freemaxencemelo#

#justiceforlema#

#bringbackbensaanane#
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hiyo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Utashindwa wewe..
 
Wana mabadilko mnataka rais ashindwe halafu mnajiita wazalendo HAHA HAHHAHA kweli mamvii kawaroga
 
Ndo maana UKUTA ulikuwa na maana sana, baadhi ya watu walipoguswa na mkono wa chuma wa awamu ya 5 kwamba eti ni mafisadi tulikaa kimya maana sisi hatukuwa mafisadi, wakafunga ajira zote, tulikaa kimya maana sisi tuna ajira, sasa wanaminya Uhuru wa habari na mitandao ya kupata habari ndo tunajikuta hakuna mtu wa kutusemea tena zaid ya kuvumilia haya maumivu. Hebu tujikumbushe kwa pastor Martin Niemoller.
Martin Niemöller (1892–1984) was a prominent
Protestant pastor who emerged as an outspoken public foe of Adolf Hitler and spent the last seven years of Nazi rule in concentration camps.

Niemöller is perhaps best remembered for the quotation:

First they came for the Socialists, and I did not speak out—
Because I was not a Socialist.

Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out—
Because I was not a Trade Unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—
Because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.

The quotation stems from Niemöller's lectures during the early postwar period. Different versions of the quotation exist. These can be attributed to the fact that Niemöller spoke extemporaneously and in a number of settings. Much controversy surrounds the content of the poem as it has been printed in varying forms, referring to diverse groups such as Catholics, Jehovah's Witnesses, Jews, Trade Unionists, or Communists depending upon the version. Nonetheless his point was that Germans—in particular, he believed, the leaders of the Protestant churches—had been complicit through their silence in the Nazi imprisonment, persecution, and murder of millions of people.

Only in 1963, in a West German television interview, did Niemöller acknowledge and make a statement of regret about his own antisemitism (see Gerlach, 2000, p. 47). Nonetheless, Martin Niemöller was one of the earliest Germans to talk publicly about broader complicity in the Holocaust and guilt for what had happened to the Jews. In his book Über die deutsche Schuld, Not und Hoffnung (published in English as Of Guilt and Hope)—which appeared in January 1946—Niemöller wrote: "Thus, whenever I chance to meet a Jew known to me before, then, as a Christian, I cannot but tell him: 'Dear Friend, I stand in front of you, but we can not get together, for there is guilt between us. I have sinned and my people has sinned against thy people.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom