Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Kuminya vyombo vya habari ni kuiteketeza demokrasia yetu tuache huru tujadiliane kutuzuia ni kutufanya tuishi ndani ya box.Tunakataa hali hii kwa nguvu zote na tunasema ##free Max###
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Nini maana ya uchochezi?
 
Nataka rais Magufuli ashindwe
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
Ameshindwa tayari kilichobaki ni kupigia majibu mistari
Link Swali la Ugomvi: Ni Kina Nani Wasiotaka Magufuli Afanikiwe na Kwanini?

Link2. Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
Napiga goti usiku kucha nikiomba hayo maono yako yawe ya kweli ya Lema naona kama yanakawia vilee!
 
Nini maana ya uchochezi?
Ni kusema au kumwambia mfalme anaetembea na joho linalompendeza na sililoonekana kwa kutumia lugha ya mtoto mdogo na ya mshangao , "mama, mama, mfalme hajavaa nguo".

Maana ingine ya uchochezi ni kuita domo-krasia kwa jina lake, domo-krasia.

Pia unapolalamika kwamba umepigika kimaisha baada ya wataalamu wa uchumi wa mwendokasi wanapozuia wapiga dili (walalahoi) wasipate uwezo wa kupeleka mkono kinywani.

Unaitwa uchochezi pia unaposema huna tena uwezo wa kujitetemesha/kukaza mkanda ili Kaizari apate vitu vyake (akusanye kodi yake).
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
Umewasahau wengine. Dr. Mwakyembe anaongoza wizara ipi?
Mwanasheria mkuu wa siri-kali anafanya kazi ipi?
Napiga goti usiku kucha nikiomba hayo maono yako yawe ya kweli ya Lema naona kama yanakawia vilee!


Link Rais Magufuli asaini Sheria ya Habari
 
Huyu rais nilidhani angekuwa wa maana kumbe bora mpenda safari Kikwete. Huu udikteta angeupeleka kwenye mambo ya msingi angefanya la maana sana. Seems hana shughuli anazi create kama Mjinga mjinga yule taahira Paul Makonda

Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema
Mkuu mimi nimeshakupa LIKE, naomba nikuamkie 'Shkamoo'.

Umeukonga moyo wangu.
 
JF ni Jukwaa linalofuatiliwa sana na viongozi.
Inasemekana baada ya viongozi kutoa matamko yao, huja huku haraka kuangalia maoni ya vijana.
Wanakuja huku kwa kuwa waliopo huku wanajielewa.

Vita dhidi ya JF ni vita dhidi ya wanao jielewaa.

Ila wakumbuke kuwa JF haijawahi kushindwa na haitoshindwaa!!
[HASHTAG]#GREATJF[/HASHTAG]
Mmmm...mkurugenzi yuko lock up....mwisho wa siku details za wachangiaji zitakuwa hadhalani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom