Suala sio kuombeana au kutakiana mabaya. Sio vizuri na sio maadili au misingi ya Taifa letu. Tabia na Utamaduni wa chuki uliotanda katika jamii ya nchi za Maziwa Makuu tusiruhusu kuingia Tanzania.
Rais wetu, Kiongozi wetu ana haki na heshima zetu zote. Pia sisi ni jukumu letu kulinda hadhi na utu wa Kiongozi wetu.
La muhimu, tuchukue fursa hii ya mitandao kuelimishana.
Bila shaka, Rais wetu sio mbomoaji, nia yake ni nzuri na anameonekana ana hamu kubwa la kulijenga Taifa letu. Tutakuwa nae kutimiza nia yake nzuri ya kuliendeleza Taifa letu.
Tuwacheni chuki binafsi.
Mhe. Tundulisu alizungumza vizuri kwenye hoja yake moja Bungeni, kuwa watendaji kazi wa Serikali wanafanya kazi zao kwa kuogopa na pia wengi wanafanya kwa kutaka sifa. Hapo ndipo wanapolipaka tope Awamu ya 5.
Sisi pia tunaotoa maoni, maoni yetu yawe na busara ili iwe source ya elimu kwa Serikali au jamii. Na pia sio maoni yetu tuu, tuonyeshe kwa vitendo. Vitendo vizuri.
Ni kweli kama binaadamu yeyote Rais wetu hajui mengi, tunamsihi na tunamuomba atoe mwanya wa kushaurika na wananchi, haitaidhuru au kulipunguzia Taifa au Serikali yetu lolote.
Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Bwana Thabo Mbeki (Mpigieni makofi na mshangilieni) tunamkumbuka kwa mfumo wake mzuri wa Utawala: "Watu Mbele" au Wananchi Kwanza, na nadhani mpaka sasa Watanzania ndio wana kiu hicho.
Leo kwenye mitandao hii, tusimpinge mtu binafsi, tupinge sera dhaifu zinazotawala, na sio kwa ajili ya manufaa yetu binafsi tuu, bali ni kwa ajili ya kizazi kinachokuja.
Mengi hapa sio mawazo yetu Binafsi au kwa ajili ya Matamanio yetu Binafsi. Tunaunga mkono au Tunapinga chini ya Kivuli cha Wale Waliotangulia, Misingi na Maadili mazuri ilyowekwa na wale Waliotangulia kama akina Patrice Lumumba, Mwalim Nyerere na Nelson Mandela, juhudi zao zimeleta mafanikio makubwa kwenye bara hili.
Wengi hatuna nia mbaya wala hatutakiani ubaya. Its a way to stimulate and expand our views and our intelligence, and this has been a unique theory that has been used in any political organization or many educational institutions. This is what brought and added civilization to the human history.
We will debate, we might agree or disagree, but at the end of the day lets eat and drink together. Our Unity is essential.
JF, you deserve our Thanks!
Our prayers are with Comrade Max Melo, his family, and his folks, all the honest protesters and activists on JF. We extend our Thanks to our fellow citizens and all the children of this blessed Continent.
Long Live the Spirit of Bantu Stive Biko "I Write What I Like".