Nataka niokoke wapendwa

Bosi swala si kuokoka.
Amini kwanza then surrender kwa Yesu ukianza kutafuta mchungaji huyu na yule utapotea.
Maana unajuaje imani zao na makanisa yao kama ni ya kweli. Esp kama wakifanikiwa kupoison your mindi?
Sana sana utaishia kupekeka kila unachopata kwa huyo mchungaji. Then uishie kuchukia kuokoka au hata umchukie Mungu kabisa..
Mimi si mzuri kwenye ku crame mistari ila najua kuna moja ya nyaraka za paul ambazo aliwakemea alio waandikia kwa kujitenga. wengine wakijiita wa yesu wengine sijui wa nani kila mmoja akijitambulisha kwa yule aliye mhubiria habari kwanza.
Na wengine wakijiona superior kwa wenzao.
 
Woote ni wa yesu. So usimtafute mchungaji .Mtafute Yesu,
Ndiye mwalimu, mchungaji, njia na kweli.
Mwamini yeye. Jisalimishe kwake.
Ila angalizo kuokoka sio tiketi ya mafikio yako ya Mahangaiko ya kidunia. Anaye kuhubiria kwa mtazamo huo wa kidunia anakudanganya.
So its up to you ukitaka kuungana na waliodanganywa au unataka wokovu wa kweli.
 
Kuokoko kukoje ivi mungu hawezi kukuona mpaka uende kuokoka??? Duu sijajua uelewa wako ukoje Mimi nakushauri amini kama wanavoamini ndege ya kuwa hakuna spasayekufuatwa/kuabudiwa isipokuwa mungu mmoja aliyetuumba maana makanisa yapo mengi utaenda wapi ndugu yangu maana Kuna kanisa lingine linasema mungu aliyeumba mbingu na nchi ni YESU NILILIA SANA SASA NDUGU YANGU SIJUI UTAENDA KANISA GANI HAKUNA MTU HATA MMOJA ANAYEWEZA KUKUOKOA ISIPOKUWA NI KUAMINI KATIKA NAFSI YAKO TU NA KUTENDA YALE TU YALIYO MEMA MUNGU ATAKUJAZI
 
Mkuu unataka kuokoka kwa lengo gani?

Maana kama Kwenda Mbinguni unatakiwa uwe Mtakatifu tambua hilo.. Watakatifu hawafanyi dhambi ndio wameandikwa kwa idadi watakao ingia Mbinguni Mataifa kumi na mbili ya Waisrael kila kabila Watakatifu kumi na mbili Elfu jumla kwa wote ni 144,000.

Imeandikwa hiyo kwenye Biblia.... Biblia isome wewe mwenyewe uelewe nini kimeandikwa na nini unatakiwa kufanya uwe Mtakatifu... Hilo ni Agano Mungu ameahidi... Achana na wazushi hao wapiga deal Biblia ndio Jibu. ukikubali kusomewa utafichwa mengi sana isome mwenyewe...
 
Sina furaha sina amani kwa maisha nayoishi nataka nimrudie Yesu anisamehe dhambi nahisi ndo zinanikwamisha. Mda mwingine huwa nasali mwenyewe lakini naona kama Roho Mtakatifu yupo mbali na mimi, sala zangu hazileti matunda kwa sasa nataka niokoke nisimame sawa sawa shetani ananitesa.

Nahitaji nguvu ya wengi

Nipo Iringa namuhitaji mchungaji Boaz Solo mwenye radio ya Overcomes Fm.
Umeamua kumtangaza mchungaji wako Boaz kupitia @JF
 
Hayo ni maamuzi mazuri na yenye hekima. Kumrudia Mungu ni jambo nzuri sana. Mungu akubariki kwa uamuzi huu. Nenda kwa askofu Mkane pale TAG - MLANDEGE utaongozwa vizuri.
 
Sema, Bwana Yesu, Naja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi, nimekutanda dhambi wewe peke yako, naomba unisamehe, takasa dhambi zangu zote kwa damu yako iliyomwagika pale msalabani, natamani kuanza maisha ya wokovu sasa, ingia ndani ya moyo wangu, nifanye kuwa kiumbe kipya, nakuamini Yesu, ya kuwa ulikufa na siku ya tatu ukafufuka, uko mbinguni unakaa mkono wa kuume wa Mungu Baba, naokoka sasa, eee Yesu nisaidie. Amina.

Sali sara hii kwa kumaanisha na utaona mabadiliko katika roho na maisha yako.

Kesho au siku yeyote mtafte mtu aliyeokoka au kanisa lolote la walokole uende ujitambulishe na ujiunge nao.

Mungu akubariki sana.

Na wengine wenye shida kama ya huyu ndugu, fuatisha hayo maneno kwa sauti ukiwa peke yako au sehemu yeyote na Mungu atakuokoa.
 
Hao wachungaji wenu akina Boaz Solo si ndo wale wanaowakwea mgongoni kuanzia mwanzo wa misa mpaka mwisho hawataki kukanyaga chini.
 
MPE yesu maisha yako yote,kumbuka wokovu ni kutangaza vita na shetani lakini Mungu atakushindia
Achana na Mchungaji Boazi tafuta kanisa lolote LA walokole wakuongoze sala ya toba
Acha kuongopea watu aliyejwambia kwa walokole ndo Kuna mungu Nani je yesu alikuwa mlokole?? Yesu aliongoza sala ya toba usijifanye unamjua mungu kumbe zero. Mungu unamjua tangu uzaliwe ila tumekengeuka kinachotakiwa kuwa kama Mimi amini MUNGU MMOJA TU ALIYEKUUMBA KAMA NI SADAKA WAPE WAJANE NA YATIMA FULL STOP
 
MAN kimsboy HIVI HILO JUKWAAA LA DINI NI SIFA GANI MTU UWE NAZO NDO UWEZE KUSOMA THREAD ZAKE.MANA TANGU 2011 IF I NOT MISTAKEN NIJIUNGE JAMII FORUM NIPO TANGA ADVANCE SHULE.HADI LEO SIJAWAHI ACCESS.nishaomba sana kwa @moderators holaaaa.JAMAN nawaombaaaa NIUNGANISHENI
hata mm natamani sana mkuu naskia ni.mpaka uwasiliane na mods
 
Naona umeamua kuwa mjumbe wa ibilisi kumpotosha mwenzio! Kuna makanisa mengi sana yana mtumikia Mungu. Marafiki hawawezi kuwa na msaada muache aokoke wewe endelea kuzinzika tu.
Niendelee kuzinzika? haya ndio mawazo ya mlokole typical, kujidhania wao ni watakatifu kuliko wenzao kisa wametofautiana imani...huu ni ugonjwa mbaya sana
 
Niendelee kuzinzika? haya ndio mawazo ya mlokole typical, kujidhania wao ni watakatifu kuliko wenzao kisa wametofautiana imani...huu ni ugonjwa mbaya sana
Mtu hunena yajazae moyo wake, unamzuaje asiokoke kisa et wachungaji wata take advantage ya matatizo yake? Wewe unawajua wachungaji wote? Ndiyo wewe ni wakala wa ibilisi kama walivyo wachawi, wanga na waganga wa kienyeji, sema wewe ni indirect devil's agent ndiyo maana umesimama upande wake.
Pia unazinzika kataa!
 
Mtu hunena yajazae moyo wake, unamzuaje asiokoke kisa et wachungaji wata take advantage ya matatizo yake? Wewe unawajua wachungaji wote? Ndiyo wewe ni wakala wa ibilisi kama walivyo wachawi, wanga na waganga wa kienyeji, sema wewe ni indirect devil's agent ndiyo maana umesimama upande wake.
Pia unazinzika kataa!
Kwa hiyo unapinga kuwa hakuna wachungaji matapeli? kumwambia mtu kuna wachungaji matapeli nimeshakua 'muovu' tayari.....
 
Kwa hiyo unapinga kuwa hakuna wachungaji matapeli? kumwambia mtu kuna wachungaji matapeli nimeshakua 'muovu' tayari.....
Kitendo cha kumwambia mtu asiokoke hakiwezi kufanywa na mtu mwenye Mungu, ..wewe umesema wachungaji wata take advantage means wote,hapo ndipo ulipo haribu, kuna wachungaji wa kweli tena wengi kuliko wa uongo na uwepo wawachungaji wa uongo siyo sababu ya kumzuia mtu kuokoka wakati mwingine usijitie kiherehere kuchangia kitu usicho kijua.
 
Back
Top Bottom