Kuokoka ndo kukoje? We umeshaweka nia ya kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu hapo, sa wokovu wa Kweli ndo huu.... Fata kanuni kuu, mtendee jirani wako kama upendavyo wewe kutendewa, tena kwa UPENDO. Ktk hili, jifunze KWELI KUU ktk yote ili usije ukaangamia kwa kukosa maarifa. Tafuta kweli juu ya maisha, Yesu, Mungu, biashara, dini, chakula nk. Tafuta kweli juu ya jambo lolote lile.
Mfano, Kweli juu ya jirani wako ni yeyote /chochote chenye kuathirika na matendo yako. Ukiwa ni dereva barabarani mbwa akatishae, ng'ombe watu, nk ni majirani zako na wote unatakiwa uwatendee kama upendavyo wewe kutendewa nao kama mngebadilishana viatu vyenu.
Housegirl wako, mlinzi wako, kijakazi shambani wote watendee vile uonavyo ungepaswa wewe kutendewa, walipe kile ambacho ungependa wewe kulipwa, hata kama mwenyewe ametaja kiwango cha chini we mlipe vilevile kadri ya kile ukipendacho wewe.
Ukifanya hayo, ukaishi hivyo, hata kwa huyo mchungaji usijisumbue nae, pepo yako nyeupe kabisa.