Nataka ninunue smartphone

Nataka ninunue smartphone

Kweli Samsung ni nzuri lakini kimbembe kwenye betry tu. Nunua tecno ni simu poa tena zipo new versions za kutosha za hadhi.
 
Samsung tatizo lao liko kwenye btriii, yaani betrii zao hazidumu kivile
Sijui uwezo wa betri mnalinganishaje, mimi ninaona Samsung kwa sasa wameboresha mfumo wa betri, cha msingi nunua original.

Kwa mfano, kama ni mtu wa kuchati kwa kadiri, yani unaingia na kutoka, unaweza kushinda kutwa nzima hujaichaji simu.Ninajua kuwa kuna simu zina uwezo zaidi ya huu, lakini kwa simu janja nyingi, kushinda kutwa nzima hujachaji ni uwezo mkubwa pia.
 
Kama una hela samsung ni nzuri kama huna hela na budget yako ni kama laki 2 au 3 tecno ni simu nzuri sana
 
Au nunua Samsung S9 + kwa 1,950,000/= au Samsung Note 8 Duos kwa 1,580,000/=
Ni simu nzuri mno ni kama Laptop kila kitu hadi ATM
 
Hivi kati ya tecno na Samsung ipi nzuri!!?
Samsung ni bora kwa kiasi fulani,ila ni ghali.Kama una hela zisizo na kazi,hasa ukizingatia kwamba vyuma vimekaza,nunua Samsung.Ila kama ni mtu unaejali pesa,nunua Techno.Ni nzuri tu,mimi ninayo Techno W4 sasa mwaka karibu wa nne huu, inadunda tu.
 
Back
Top Bottom