Unaona unavyojikanyaga, unasema mitandao haina faida halafu hapa unatumia mtandao kuomba ushauri.
Mitandao inafaida yake kama utaitumia kwa manufaa, lakini kama utaitumia vibaya, kama kufuatilia udaku na mambo mengine yasiyo na maana hutofaidika hata utumie miaka mia.
Na kingine ni kuitumia kistaarabu sio muda wote unashinda mtandaoni, hayo ndio matumizi mabaya.