Nataka nikae mbali na Social Media kuepuka siasa,nataka nianze utaratibu wa kusoma vitabu

askofu rashid

Member
Oct 26, 2020
25
43
Asee nimekua rafiki sana wa mitandao ya kijamii tangu mwaka 2009 lakini naona hakuna kitu nimegain zaidi ya concentration yangu kuwa katika vitu visivyokuwa na maana. Kama niliweza kushinda jaribu la kupiga punyeto na kuangalia porn nadhani nitashinda.

Nilichogundua mambo mengi tuyaonayo mitandaoni ni tofauti sana na uhalisia wa maisha yetu halisi, Ndo maana kuna watu ambao hawapo katika trend ya mitandao kuna baadhi ya mambo ukiwauliza au ukiwaeleza hamuelewani.

Pia nataka nijiepushe na mambo ya siasa dah yanaudhi sana ndo maaana nataka niache upepo wa mitandao ya kijamii tayari nishaanza kufanya mazoezi jioni baada ya shughuli zangu mi napiga mpira balaa.

Nataka nihamie pia katika upande wa vitabu naombeni mnishauri vitabu vya kusoma au wapi naweza kua napata vitabu vya kusoma ila sio online nataka hard copy,mi ni mpenzi wa kujifunza mambo mengi so nadhani inspiration history, documentary na mapenzi vitanifaaa sana.

Karibuni kwa ushauri wapi naweza kupata vitabu na vitabu gani vizuri nianze navyo.
 
Umeshatubu hii dhambi kwa wananchi?
709081.jpg
12460.jpg
098765.jpg
 
Jina lako na picha yako tu sheikh wangu mie hoi kwa kicheko 😂🤣😂😂🤣😂😁😀😃
 
Unaona unavyojikanyaga, unasema mitandao haina faida halafu hapa unatumia mtandao kuomba ushauri.

Mitandao inafaida yake kama utaitumia kwa manufaa, lakini kama utaitumia vibaya, kama kufuatilia udaku na mambo mengine yasiyo na maana hutofaidika hata utumie miaka mia.

Na kingine ni kuitumia kistaarabu sio muda wote unashinda mtandaoni, hayo ndio matumizi mabaya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom