Nataka nijue kusoma Quaran

Huku wapo mawakala wazuri tuuuu.

Kuna mkenya mmoja akiitwa ABOUD ROGO akiwahimiza watu wazi wazi waende somalia kupigana jihadi,wakajiripuee n.k(huyu amekufa miaka ya 2013 aliuliwa na watu wasiojulikana)

Hapa tanzania kuna kijana mmoja wa mwanza alisoma pemba kwa maalim hamza (jina nalihifadhi)huyo kijana alikuwa ana wahimiza waislamau waende somalia wakapigane na kujiripua hapa tanzania ukafiri mtupu.

Na wako weeeengi tanzania ambao wana fikra hizo za kujiripua ndyo maana nakuambia hivyoo mkuu.

Ila wapo watu ambao hawafundishi fujo,hawafundishi jazba japo kuwa ukiwaona utawaona wana ndevuu nyiiingii unaweza sema ni kama kina osama ila ni watu wazurii hawana fikra mbaya za kujiripua ripua.

Khawaarij hawa, kuanzia baba yao usama bin laden na watoto wake ndio hao akina rogo
 
Makazi yangu mara nyingi nipo Moshi, Mbeya mjini na Iringa mkuu...nipe ushauri
Kwa Mbeya nenda Msikiti Mkuu pale upo umbali mfupi kutoka Stendi kuu ya Mabus Mbeya kuna ustaadhi pale na vijana wanaishi pale pale ndani ya eneo la msikiti watakusaidia sana.
 
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.

Moja ya sababu zilizofanya niipende dini hii ni kwamba lugha inayotumika ni ile halisia iliyotumika kuandika hii quaran, Napenda sana napokua kwenye dini nisome kwa maandiko orijino, kusiwe na kitu ambacho kimeongezewa wala kupunguziwa, wala kutafsiriwa.

Kuna makosa madogo katika tafsiri ya lugha iliyotumika kwenye maandiko ya kihebrania ya biblia mfano biblia zetu zilizotafsiriwa zimeandika mama yake Yesu alikua ni bikra na ndicho wengi huamini ila biblia orijino ya kiebrania imeandika kwamba mama yake yesu alikua ni mwanamke mdogo anayeweza kuzaa,

Kwa vile hapa Tanzania ni nadra sana kukuta madarasa ya kiebrania Ningejaribu mbali kujua kihebrania ila jitihada zingegonga mwamba kwa sababu nilifatilia kwamba kwamba huko israel dini ya ukristo ni asilimia 2 tu wanaoiabudu tangu ilioruhusiwa mwa juzi (2016) ambapo wengi huabudu judaism na uislamu.

Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,

Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.

Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.

NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.

ikiwa una nia ya dhati kuujua uislam basi nikupe hongera sana kwa msimamo na maamudhi uliofikia, hilo sio kosa hata waislam wametakiwa kuamini na kusoma vitabu vinne (1-Tawrat - Moses book, 2-Zabour- David, 3-Injil - Issa/Yesu, 4-Quran-Muhammad S.A.W) ikiwa ni katika nguzo ya Imani.
Ushauri wangu tafuta Sheikh ambae amekua akisomesha ndani ya msikiti tafsir ya Quran na ukiwapata wale wazee watakusaidia zaidi. Quran imekuja kwa lugha ya kiarab lakini haina maana kujua lugha ya kiarab ndio kuijua kuisoma Quran
Jaribu kufuatilia mawaidha hasa yanayohusu historia ya dini hizi ili ujiongezee maarifa zaidi mfano huyu Sheikh Othman Maalim:
 
Japo Elimu haina mwisho, kujua na kusoma Qur'an inaweza kuchukua muda gani kwa mtu ambaye ni mweupe kabisa kichwani lakini kila siku anaweza kutenga masaa mawili? Binafsi nahitaji kujifunza nahisi kama naweza kusilimu siku zijazo nafsi yangu inaniambia hivyo...
Ukiwa seriously Sana ni miez mitatu usipokuwa serious miez sita na ukiwa mvivu mwaka
 
Japo Elimu haina mwisho, kujua na kusoma Qur'an inaweza kuchukua muda gani kwa mtu ambaye ni mweupe kabisa kichwani lakini kila siku anaweza kutenga masaa mawili? Binafsi nahitaji kujifunza nahisi kama naweza kusilimu siku zijazo nafsi yangu inaniambia hivyo...

Kama ni mwepesi sana inaweza kukuchukua 3 weeks ukawa tayar umeshaanza kusoma,
Na kuanzia mwaka mmoja ukawa umei memorize yote,kiasi kwamba hata mtu anahubiri au anafundisha akikosea tu,tayar ushajua hapa kakosea.
TANBIHI,jitahidi upate sehem sahihi na mwalimu sahihi
 
Allah Akbar kijana mwenzangu nakukaribisha katika dini ya manabii(mitume)Mwenyezi mungu akufanyie wepesi
19904879_645443425663053_8166245293053142456_n.jpeg
 
Na hii umeisoma?. Mungu ni mmoja na hana mshilika. Nyingine inasema . Mwenyewe umejifanyia mambo, hata yakakufika hayo, nasi tunakutuma kwa watu ukawe mtume kwao. Sasa waulize ivi kama hanashilika ni wakinanani hawa waliokubaliana kumfanya mtume?. Zingatia neno NASI inamaana ni wingi,zaidi ya wawili,na hana mshirika. Tumeondoka dini hiyo. Mwanzoni família ilinitenga badae wote ni wakristu . Asikudanganye mtu yesu ni njia ya kweri na ufufuo wa uzima.
Hebu rudia kuandika tena.
 
Nenda ubalozi wa Saudia kawaambie shida yako au Ubalozi wa Sudani ni rahisi sana kupata short course ya mwaka 1 au kama mhitimu wa degree nenda kauluzie utaratibu wa scholarship za post graduate zikoje utaambiwa
 
Japo Elimu haina mwisho, kujua na kusoma Qur'an inaweza kuchukua muda gani kwa mtu ambaye ni mweupe kabisa kichwani lakini kila siku anaweza kutenga masaa mawili? Binafsi nahitaji kujifunza nahisi kama naweza kusilimu siku zijazo nafsi yangu inaniambia hivyo...
Bila kubamizwa makofi na ustadh utachukua miaka mingi Sana ,mtume mwenyewe alikabwa na jibril
 
Ee naam mkuu,wengine watakuambia kafiri auwawe tuu hakuna kushirikiana naye,alafu anatoa aya mahali ambapo haikukusudiwa hivyo.

Yaani mfano wa watu walioedit ile clip ya magufuli ya you know you know alafu hata uingereza hajaaaaaafika.

Au ile ya injiniaa akibabaika kusoma namba hahahha.

Sasa haya sitaki huyu ndugu yangu yamkute,kuna madhara makubwa sana.

Kuna mtu alimuuwa mama yake kwa kusema ni kafiri,kwa sababu ya fikra ambazo alifundishwa huko madrasani kwake.
Mkuu nimekuelewa sana. Mimi binafsi siyo muumini wa dini yoyote baada ya kukulia katika ukristu nkuufuata tangu nikiwa mdogo. Na nilibahatika kusoma katika shule za seminari nimesoma biblia na nilipata A katika mtihani wa Taifa. Nimesoma Seminarini miaka sita lakini nimeamua kubaki kama mtu ninayeamini Mungu yupo ila sina imani na dini yeyote na wanangu wanalijua hilo ila sina wasiwasi na mtu kuamini anachokitaka na nimeweka wazi kwa wanangu wafuate wanachokitaka. Mmoja kaamua kuwa muislam wengine wakristu.

Ila hua napenda sana kuongea na watu kama wewe ambao wanasema ukweli kwa maana kufundisha watu bila kukashifu ama kujifanya kama wao ndiyo kamili kuliko wengine. Kama Watu wote wa dini wangekua kama wewe sisi wengine tungebaki waumini wazuri lakini ukiona mtu anakshifu mwenzie bila kutoa sababu za kumvutia mtu ahamie kwake hapo ndipo ninakwazika.

Kwanini naita dini ni utapeli sina maana ya kukashifu wanaofuata bali viongozi wengi ni wababaishaji. Hainijii akilini kwanini mkristu wa Roma ajifanye ni bora zaidi ya mkristu m pentecostal vivyo hivyo m pentecostal amuone Mroma si bora. Ukiingia Uislam vilevile Suni anajiona ni bora zaidi ya Shia mpaka kupigana vita na kuuana. Nini unakipata kwa kumuua m Shia sababu wewe ni Suni na vice versa. Ni biaahara pekee watu hugombana. Mwanza waumini walimpiga Askofu Maeneo tofauti misikitini watu wanagombana. Dini si ndiyo ilitakiwa kufanya watu waishi kwa kupendanna sasa ugomvi unalwtwa na nini?
 
Yes mkuu ndyo mana na mimi namsisitizia mtoa mada atafute sehemu salama akasomee na sio kwa kila shekhe tu.

Dini (uislamu)una maandiko mengi ya vita vita,hilo jambo linafanya mtu atakae kupotoa apotoe kwa namna aitakavyo lakini makusudio sio hayo.wale wanaojiripua wale ukweli ni kuwa wanatumia Quran hii hii tunayotumia sisi na aya wanatoa humo humo lakini jeee aya zimekusudiwa kama ambavyo wao wanzitumia? Utakuja kuona ni ufahamu wao mfinyu na jazba walizosoma kwa watu wajinga wajinga wanaojiita waislamu.

Hivyo mkuu naungana na wewe na hata hii dini ninayoiabudu(islam)haiko vile watu wanaifikiria,mfano tuuu ikatokea tanzania ni nchi ya kiislamu basi uislamu umekataza kubomoa makanisa na utawaacha watu waendelee kuabudu humo na ni wajibu kwa dola ya kiislamu kuwapa ulinzi watu hao ambao wanaishi kwa amani na waislamu.

Hizi dini tukiziendea vibaya na kwa pupa ndo tunawatoa watu kama kina OSAMA BIN LADEN na wahuni wengineo ambao wanajivika uisilamu na wattu wanawatizama wao.

Binafsi niliamua kusoma dini na kuichambua kwa Qadri ya akili yangu huku nikiwa sitoki nje ya misingi hyo,na sasa hivi nafurahia maisha na dini yangu kinyume na waislamu wengi leo wanaojipa tabu kutaka kwenda somaliaa,kujiripuaa,kujitoa muhanga,kufanya maandamano n.k.
 
Back
Top Bottom