Nataka nifungue kesi dhidi ya Clouds TV, msaada tafadhali!

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Kwa yaliotokea katika kipindi cha take one na kumhoji yule shoga nakusudia kufungua mashitaka dhidi ya clouds!Kwa wana sheria nitumie njia gani maana nikienda kichwa kichwa sintafanikiwa.

Hebu tafakari kidogo ubaya wa kipindi kile. Yule shoga anasema yeye ni shoga tangu kuzaliwa na hajuti kuwa shoga, anafurahia kuwa bwabwa! Hajawahi kutamani kuwa mwanaume na huku ni mwanaume!Anafundisha nini jamii?Ana mpango wa kupandiza mimba azae! Yani maneno ya hovyo zaidi ya haya nini anafundisha mwandishi katka jamii ya kitanzania?

Je unaweza kumwalika jambazi aeleze anavyowaibia watu na mipango yake ya kwenda kubomoa bank? Unaweza kumwalika gaid akuambie ameua wangap na mipango yake ya kwenda kulipua ikulu akatoka studio salama?Kwanini kama ushoga ni kosa la jinai aruhusiwe mtu kuhojiwa na awe salama? Kwanini tv husika iwe salama?

Nilitaka niende kwa Nape lakini naona yeye na lugha dam dam,. Mmoja amepga simu kupongeza kipindi hicho kiendelee kufundisha ubaya wa ushoga. Means anakubali njia hiyo iendelee kutumika! Kwa mkuu wa kaya ndio kabisa alisema ndio tv anayopendelea kuitizama! Hawezi kukubali ifungiwe!

Lakini kwa kila mzalendo anipe njia niwafungulie mashitaka na clouds wafungiwe! Sioni aliye serikalini aliye na uwezo wa kuigusa hiyo tv nategemea mahakama tu labda ndio watatenda haki! Na wewe mzalendo wa kitanzania fanya uwezalo kukemea upuuzi huu unaonezwa katka taifa letu.
 
Huyo shoga anapaswa kukamatwa na kushitakiwa kwani amikiri kufanya mapenzi kınyume na maumbile.Ni kosa kwa mujibu wa sheria.
 
Watanzania kwa kutafuta kick siwawezi.

Lakini najua hii tabia mmerithi kwa nani.

Wala simsemi!!!!

Sina milioni 7 mie
Wacha ulofa mpiga mdomo,watu wa promote ushoga.mtu akikemea useme wanatafta kiki?mwanao wa kiume alijifunza nini kwenye hicho kipindi cha take one???
 
Wacha ulofa mpiga mdomo,watu wa promote ushoga.mtu akikemea useme wanatafta kiki?mwanao wa kiume alijifunza nini kwenye hicho kipindi cha take one???
Enhee ikifunguliwa kesi inasadia nini.

Acheni umbumbumbu, Ushoga is neither a biological nor a physiological problem ila ni tatizo la kisaikolojia. Huwezi deal nalo kimabavu.

Wenye matatizo ya akili hawapelekwi Gerezani wanapelekwa Milembe kutibiwa...

Fanya utafiti kuhusu chimbuko la ushoga ndo uje ku'comment humu.

Infact kwa kulikandamiza hili tatizo na kulisema vibaya ndo tunalifanya liwe kubwa na lifanyike kwa siri zaidi which is bad cos mwisho wa siku unakuja kushtuka mtoto wako shoga bila mzazi kujua; utampeleka jela au?

1467459130896.jpg
Ni bora kuongea wazi ili kujua tuna'deal nalo vipi.
 
Hiyo ni hatali sana kwa kizazi kijacho kama itaendelea hivo ni wajibu wete kupingana na upumbavu huo!
 
Wateja wa hao mashoga mpo humu humu na wengine ni waheshimiwa sana aliogopa kuwataja.

Ni vema kuchukua tahadhari lisitokee kwa watoto wako,pia ni vizuri ukachukulia kama changamoto katika malezi ya watoto wako hapo nyumbani kwasababu ushoga hauanzi ghafla ni kidogo kidogo.

Kuwa na tabia ya kudadisi watoto juu ya muchezo wanayocheza wanapokuwa shuleni,nyumbani hasa wanapokutana na watoto wenzao.

Huyo anaweza kwenda jela lakini ikawa sio suruhisho la tatizo hilo kama hatutajirekebisha katika mfumo wetu wa kijamii na malezi katika familia zetu,utakuta baba na mama wanatoka asubuhi wanarudi usiku wa manane hawana muda wa kukaa na kujua watoto wao wanaendeleaje na wanajifunza nini pindi wanapokutana na wenzao,malezi wameachiwa mahouse girl na mahouse boy hao ndo wanawalea watoto.

Lazima tubadilike tukitaka tatuzo hili lusiendelee kuitafuna jamii yetu.
 
hiyo yote ni ukosefu wa proffesional maana watu na professional zao hawawezi kufanya upuuzi kama wanaoufanya clouds...hasa huyo zamaradi
 
Back
Top Bottom