Nataka nianze kula mjani

Kwa hiyo conclusion yako ni watu wajizimue na mjani au mjani si kitu poa?
Uwepo umakini tu kwenye kutambua kiwango chako, ukizidisha mambo yenyewe ndo kama hayo.
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
Umegundua nn

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Oya wakusoma hzo cookie zinapatikana wap najambo nazo??
 
Pole sana kijana.

Nikiri kuwa nikiwa na Umri kama wako nilikuwa na uchu sana wa kujaribu kuvuta Bhangi kama wewe. Asilimia kubwa ya Rafiki zangu niliokuwa naambatana nao walikuwa wavutaji. Na kila jioni lazima tutoroke kwenda Nje ya Shule kuvuta.

Ajabu ni kwamba mmojawapo Wa wale Marafiki alikuwa mkali sana kwangu kuwa nisijaribu kabisa kuvuta, ilhali yeye alikuwa mvutaji. Kwa sababu yake nikawa Mpasishaji kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine ila sikuthubutu kabisa kuitia mdomoni. Jamaa aliniambia naweza kuchanganyikiwa kabisa nikijaribu kuvuta.

Tulipoingia kidato cha Pili kuna Bro alikuwa mbele yetu, yeye Form 4 akaanza kuonesha Dalili za kuwehuka,, Shule ikamrejesha nyumbani akajiuguze kwanza.

Wazazi wake (wakati huo Walikuwa Wanafundisha Chuo cha Ushirika) wakahangaika naye sana mpaka Mirembe lakini Jamaa hakurejea tena kwenye utimamu. Ikawa tukienda mtoni kufua tunamkuta kule analala tu Juu ya mawe.

Mwaka Jana nimeenda likizo Jamaa yupo yupo tu, hana Familia, anaishi kwenye Nyumba ya Mzee wake na akili sometimes yes, sometimes no. Shule hakuweza kuendelea nayo tena.

Mwingine tena, tukiwa likizo ya kuingia kidato cha tatu akavuta Bhangi akaenda kukabaka Katoto ka Darasa la sita huko kwao, Wazazi Wa yule mtoto wakamkazia Jamaa akapelekwa Jela za watoto zile, miaka miwili.. Aliporudi mtaani inasemekana akatishia kumwua Mamake na panga, akaswekwa Ndani tena (jela ya wakubwa sasa). Naye sasa hivi ni Baunsa kwenye makumbi ya starehe, anailaani Bhangi mpaka Leo.

Mpaka Leo Namshukuru yule Mwamba aliyekuwa ananiletea unoko nisijaribu kuvuta, ilhali Shule nzima ilikuwa inaniweka kwenye kundi la wavutaji kutokana na ile Kampani..
 
Bhangi sio nzuri. Itoshe kusema hivyo.
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
Mama pretty ona watu wanavyoangamia..😂
 
I took a splif this morning..and it make me feel so groove man..thats why i cant refuse it man... INTERNATIONAL HERB-culture
 
Niwe mkweli..(I'm not promoting it though)

Sikuwahi kuvuta bhangi toka utotoni hadi mwaka huu mwezi juzi..nimevuta kama mara 4 kwa interval ya wiki 1 1.

Nimegundua vitu ambavyo pengine nisingevigundua au ingenichukua muda mrefu.
umegundua vitu gan bro tupe maujanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…