Nipo dear, nakusoma tu... nilikua taiti kidogo na kazi za nyumbani.
Unanikumbusha ndugu yangu fulani. aliolewa ila hakupata mtoto kwa miaka tatu. yeye kama yeye (hata mume wake pia) hawakuona kua ni shida... ila familia zao ndio zikawa zinalalamika, hasa kina mama. baada ya miaka tano walikua still hawajapata mtoto, wakasafiri kwenda kuwafata wataalamu wa maswala ya uzazi kule uzunguni. Unajua dawa walio pewa? eti waliambiwa waende leave, mbali na familia zao, na waongee mambo mengine yooooote, kasoro ya mtoto. Ilisemeka kwamba ile pressure ya kutaka mtoto kwa udi na uvumba ndio ilisababisha mimba kutoshika (kama ni kweli sijui maana ndugu yangu nae kwa kukoleza story humuwezi!)
Walikaa wiki tatu, alafu wakarudi kwao. kupima tena baada ya mwezi, tayari ndugu yangu alikua mzito!