Nenda buguruni sokoni, panda ma-bus ya msanga...
Pia kuna option ya Noah ambayo ipo fast sana ila ni kubahatisha pale gongo la mboto au hukohuko Buguruni sokoni...
Kwa pale sijaona guest house ila maneromango kuna guest ya 5000. Pale na Msanga sio mbali sana...
Huu ni muda wa mavuno kwahyo kama unataka kufanya utafiti inabidi uandae kiasi kidogo cha kuweza kuwalipa ili waache shughuli zao wakupe majibu unayoyahitaji...
Utafiti wako wa uchawi haujakufanikisha kutengeneza air transport mkuu?
Lol Lil am kidding...
Nataka kwenda Msanga, nataka kwenda Msanga oooh nauli sina -Gangwe Mobb "Ngangali Kinoma"
Ukitaka kwenda Msanga lazima uwe ngangali kinoma, la sivyo utarudi na binti wa Kizaramo.
Au unaweza kuhamiabusirudi kabisa wakishakupunga madogoli.
Unafahamu usafidi ni nini?Bro we si unasema hayo mambo huyaamini. Vipi tena?
Msanga ...panda GARI had gongolamboto; halafu. Panda za chanika, ukifika chanika panda za kwenda MSANGA ZALALA A.K.A MSANGA, KUNA VUMBI JEKUNDU HATARI, HAKUNA NETWORK LABDA AIRTEL ...UMEME HAMNA KULE NI MWENDO WA SOLAR TU, JUA KALI SODA ZA BARIDI HADI WAPANDE DARADARA KUTAFTA; GARI LIKIKUACHA INABIDI HADI ULISUBIRI LILUDI TENA....Kiwanja wanauza Kwa kurusha jiwe ndio kipimo,
Haha na ndio wanaupenda na kuwaweka mjini!!Sio uchawi mzee, mbona huwa napost na mada nyingine nyingi tu, sema wabonge mmekariri uchawi tu...
Kumbuka hizo gari zote mwendo wake kama za magazeti Gesti ziko sh 5000 mpaka 2000 pamechagamka sana kuliko mahali popote ndani ya hiyo wilaya.Huko Zalala nenda mpaka chanika ndo utapelekwa Msanga Zalala.Karibu sana uzaramoni.Ukija wikiend hii kuwa makini unaweza sahau familia,kuna watu wapo huku hawajarudi kwao.
Mkuu kuna Msanga mbili na zote ziko kisarawe.Moja ni Msanga zalala unapitia chanika na nyingine Msanga sokoni we unaenda ipi?