Nataka kwenda Dubai au China kununua simu nipeni maelekezo mliowahi kwenda

Mkuu ingependeza nikupeleke
 
Mi naongezea apande ethiopian airline na wakati wa kurudi ashuke nairobi apande basi za dar atasave karibu laki 500.
 
1. Nauli return ticket quanzhou ni usd 850 to 950

2. Hotel ni rmb 150 sawa na usd 22 per day

3.matumizi ya kula, kula vzr utatumia rmb 100 per day sawa na usd 14

4. Simu utaenda kununua dashatou hapo quanzhou unapanda basi kutokea shushanlou no.4 au no.2 ni rmb 7 sawa na usd 1

5. Simu za mill 20 utanunua siku 2 tu, itadepend na aina za simu utakazochukua ila vzr kuchukua simu kubwa kubwa ndo zitakulipa
Nb. Kwenye ndege mwisho simu 15 tu pia usitumie agent kukununulia simu utapata hasara nenda mwenyewe na pesa zako mkononi don't trust anyone




Sent from my HUAWEI MT7-L09 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo mkuu mtu akienda China kwa hizo gharama zote halafu akarudi na simu 15 za smart ambazo Bei yake iwe laki 5 Hadi laki 9 kila moja inaweza kumlipa kweli?
Atoe gharama zote na faida ibaki?
 
Nenda Korea simu used za Samsung, LG na Apple bei cheeeeeeeeee
Sema ndio utenge kama mil 4 ya nauli
 

kiongozi hiyo pesa inatosha kabisa.Mimi naongelea China sababu ndio niko na uzoefu nako.Nauli inategemea na season.Ila ni ina range kwenye 700$ hadi 1200$,pia kumbuka tofauti ya siku unayokata ticketi na siku unayotaka kusafiri ina matter kwenye bei.ukikata mapema bei inakuwa nzuri kiasi.Kama unataka smartphone (iphone) nyingi ni bora uende Shenzhen Ila kama ni android nyingi ama unataka kuchanganya android na iphone basi guangzhou itakufaa.Hautanunua simu mpya kabsa (0 km) bali utanunua refubrished phone ambazo huko Tanzania ndio "mpya" hizi utanunua soko lina itwa dashatou.Kuhusu malazi kuna sehemu mbili ambazo ndizo wa afrika wengi (wa Tz) hupenda kukaa. Eneo moja linaitwa sanyuanli kwa metro ni line 2,(hili wengi wanaishi wanaokuja kununua nguo),na eneo la pili linaitwa xiaobei metro line 5(hapa kulitokea kashkash before ndo wengi wakakimbilia sanyuali).Bei huwa inaanza 120 RMB hadi 200 RMB kwa single room(kuna hotel unaweza pata kwa 100 RMB,ila huko foreigners wanaoishi ni wachache.Kama si mtu wa kujichanganya patakufaa.Ni sehemu ambako kuna soko la spare parts za pikipiki.)
Kwa mizuguko ya town kama ukiweza kutumia metro ama kujua namba za basi itakusaidia sana.Kwa basi ni 2RMB tu kwa route.Ila metro inategemeaa na unakoenda.Metro is much easier sababu hakuna traffic jam.Kama unataka accessories kuna soko ukienda kwa metro kituo kinaitwa cultural park utapata unachotaka.Lakini zaidi sana uwe mzoefu wa simu na ujue kuzikagua.Wachina huwa hawaamini hadi ajue wewe ni mtu wa kudumu otherwise unaweza ukanunua simu 50 na ukawa na return 30.
Kuhusu kutuma mizigo unaweza ukaenda nazo mwenyewe around pc 30,hizi ndo wanaruhusu ku board nazo.Ila kama ni nyingi unaweza nunua baadhi ya vitu (kama mikoba ya wadada,unaweka smu ndani na unacheki in mabegi)Otherwise ni watumie watuma mizigo wa huku(wanapatikana sanyuani siku hizi)Wata kucharge 10$ kwa kila simu na utapokea Tz kuanzia siku 2-5 toka uwakabidhi mzigo.
Hope nimekusaidia kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…