bintishomvi
JF-Expert Member
- Mar 21, 2015
- 1,164
- 832
Unawapataje hao watanzania Apo earport maana mie sijawaona pale jk nataka niende cantona fear mwezi wa nneNauli toka Dar hadi Guangzhou ni kuanzia dollar 1200 hapo inategemea na siku hiyo ni go return
Nashauri pakia Ethiopia maana inatoa Kg nyingi.
Hii waweza book na kulipia mwenyewe au utembelee ofisi za Ethiopia. Mawakala huwa wanaongeza dollar 100 kwa kila ticket.
Ukifika Guangzhou uamuzi ni wako
Ukipakia Taxi utalipa hela nyingi inaweza fika 100 hadi 300yuan kama Laki hivi ili ufike Kati kati.
Au utumie Train yenyewe ni bei rahisi nadhani ni yuani chini ya 50
Hotel pia uchaguzi ni wako zipo ambazo utakuwa watu weusi ndio wengi na hizo bei zake ni ndogo kwa siku na zipo hotel za bei kubwa kazi kwako.
Kuhusu chakula kuna kihotel kwa Mtz wanapika chakula cha Ktz hapo Guangzhou.
Kutembezwa sokoni kuna Watz wako huko ila ndo hivyo ukienda nao wanakuongezea bei.
Kutuma mzigo unaweza kuja nao ila TRA airport hawatakuacha salama.
Au
Unalipia kwa Kg hao watz wanakutolea kwa dollar 10 kwa kila mzigo au 20000 kwa kila simu.
Wao wanajua wanavyofanya huko airport.
Sent using Jamii Forums mobile app