Nataka kuvunja ndoa

Nataka kuvunja ndoa

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2009
Posts
1,195
Reaction score
232
Wadau wife naona kanichosha, yaani mawasiliano kati yetu yamekuwa hafifu sana. Wakati mwingine nashindwa kumuelewa, mara aje na stori za watu wengine wanafanyaje ktk maisha yao mara alete stori za kasimuliwa na mwanaume mambo ya ngono, ila kikubwa mi nampenda ila conditional love yangu naona imefikia ukomo kwani mimi nina excessive love na siyo selfish ila mwenzangu anaonekana ni selfish na ikija ktk maongezi naona anakosa busara.
 
Na wewe mwaga mboga,anza na stori za ma X Gfriends,kisha anza kuzusha stori kuna mi SUGAR MUM , inakunyemelea,umuone atakavyo react :madgrin:
 
Wedding calculation is one plus one =one ,follow this calculation will help you
 
Ndoa za siku hizi jamani,haya ndio matatizo umeona makubwa saaaaana,sasa nakueleza hayo ni cha mtoto,ongea na mwenza wako mmalize tofauti zenu zinarekebishika, unless hukumpenda toka mwanzo
 
Kama maongezi yanakuboa nasi usi entertain kupiga nae story! Jst muongee vitu vya msingi na mada unabaika muutumie for recreational use kama kuangalia Tv, kusoma gazeti, kusoma kitabu, check movies! Nakadhalika!
 
Pole... Kumbuka ahadi ya ndoa yako... " Till death do us part"...
Hakuna mahali ambapo utapata mtelemko.. ndoa ni kama bustani yahitaji kupaliliwa...nyeshewa maji.. tia mbolea..ondoa magugu , tia dawa ya wadudu na pia weka tuta ili mondo mkali wa amji usije zoa udongo wa bustani yako na mizizi ya mimea yako bustanini ikabaki bila sehemu ya kuegemea/jishikiza
Fikiri sana kabla ya kutenda... au kuchukua huo uamuzi. maranyingi tunawalaumu wenza wetu kumbe tatizo lipo kwetu! Kila la heri katika tafakuri yako
 
Sioni hoja ya kutosha kuvunja ndoa hapa! Kama vijimambo vidogo vidogo kama hivi vingekuwa vinavunja ndoa basi nataka kukuambia hakuna ndoa ambayo ingesimama. Kuna wanawake wengine hawana kero kama hiyo ya huyo wako, lakini wana kero nyingine ambazo ni mbaya kuliko hizo, na bado waume zao wanawavumilia.

Na zaidi ya yote, inawezekana wewe ni kero kubwa kwenye ndoa yenu that is why anajaribu kukupa mifano ya ndoa nyingine na maisha ya wengine ili ubadilike na uige mfano huo. Fikiria kama na yeye angekuona unamkera akaamua kuvunja ndoa? Jiongeze mkuu, ndoa haiendi hivyo.
 
Kuna kawimbo flani hivi kana maneno haya "wenginee amani tulonayo kidogo wanaiomba hawana ......". Ngoja nikwambie mdau tafuta sababu nyingine ya kuacha mke ukitaka kamnasishe kama wenzio ili upate evidence ahahhhahhah ila hiyo me naona si sababu ogopa stereesiiii za kujitakia narudia tena "steresiiii"
 
Sitatoa ushauri wangu kwa vile sioni hoja ya msingi ya kuvunja ndoa. Muhimu zingatia kuwa kama utaendelea kutimiza dhamira yako usianze kulia tena.
 
Wadau wife naona kanichosha, yaani mawasiliano kati yetu yamekuwa hafifu sana. Wakati mwingine nashindwa kumuelewa, mara aje na stori za watu wengine wanafanyaje ktk maisha yao mara alete stori za kasimuliwa na mwanaume mambo ya ngono, ila kikubwa mi nampenda ila conditional love yangu naona imefikia ukomo kwani mimi nina excessive love na siyo selfish ila mwenzangu anaonekana ni selfish na ikija ktk maongezi naona anakosa busara.

Kumbe tupo wengi!!!! Mi nafananishwa kimaendeleo na watu wote walionizidi uwezo! Ambao wengi wake zao wanafanyakazi, wakati mimi ni peke yangu ndio naleta chochote ndani.
 
Tatizo una conditional love. Ilipaswa iwe unconditional. Pole.
 
Ivi kumbe ndoa inavunjwaga kirahisi ivo,mbona mambo madogo hayo yanafaa kurekebika tu,,,
Communicate with ur wife broda!!
 
Maelezo yako bado ni hafifu ukilinganisha na uamuzi unaotaka kuufikia....
Ila nina swali moja tu, "Hiyo ndoa uliiunganisha wewe hata sasa utake kuivunja?"...
 
sijaona jambo la kusema tushauri hapa ama tujadili. kuwa mtu mzima acha utoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom