Nataka kutumia jina tofauti kwenye Kitambulisho cha NIDA

King Savi

Member
Sep 5, 2014
71
262
Heshima Yenu Wakuu,

Hongereni kwa majukumu ya kuijenga mama Tanzania. Nahitaji msaada wa mawazo yenu na pia kwa aliyekutana na hii changamoto anipe usaidizi pia iwafikie wahusika Serikali pamoja na NIDA.

Nipo kwenye mchakato wakupata kitambulisho cha taifa (NIDA). Changamoto yangu iko hapa nataka kutumia jina tofauti na lililopo kwenye vitambulisho vyangu, hatua nilizochukua ni kwenda mahakamani nikapata kiapo pamoja na fomu za utambulisho wa jina jipya (deed poll) baada ya kutoka mahakamani nikaenda kwa msajili wa nyaraka za serikali ili aweze kunisajili kwa majina mapya, msajili wa serikali akaniambia inatakiwa niende kwake na kitambulisho cha nida pamoja na kitambulisho cha kawaida chenye jina ninalotaka kubadilisha.

Shida ikaanza hapa, nida wanataka karatasi za deed poll ziwe certified ndio wanitengenezee kitambulisho, lakini pia nae msajili anataka kitambulisho cha nida ili aweze kucertify hizo karatasi.

Msaada wenu juu ya mkanganyiko hapa, maana sina uhakika kama serikali inaweza kumpangia mtu aitwe jina gani na jina gani asiitwe haya ni maamuzi ya mtu binafsi.
 
Kuna jamaa anaitwa Don Namilison alikua na mchakato kama wako. Mcheki umuulize yupo humu humu anatumia same name.
 
Back
Top Bottom